BAVICHA watoa salamu za rambirambi kwa Jeshi la Polisi na Mwandishi wa Habari Isango

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA POLE KWA VIFO VILIVYOTOKEA JANA NA LEO VYA POLISI NA NDUGU JOSEPHAT ISANGO- MWANDISHI.

CHADEMA tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari wa Jeshi la Polisi wanane vilivyotokea jana huko maeneo ya Rufiji Mkoani Pwani kwa kile kilichoelezwa awali kuwa ni kutokana na shambulizi la kuvizia linalosemekana limefanywa na Jambazi/ Majambazi.

Taarifa hizi sio tu kuwa ni za kuogofya bali pia ni za kuhuzunisha na kusikitisha hasa ikitiliwa maanani kuwa ni miezi michache tu iliyopita tukio la kihalifu kama hili lilitokea maeneo hayohayo na taifa likapoteza Askari wake wengine.

Tunachukua nafasi hii kulaani kitendo hiki ambacho kimefanywa na watu au mtu mwoga na ambacho kimepelekea kukatiza maisha ya Askari wetu ambao walikuwa kwenye majukumu yao ya kuimarisha ulinzi wa raia na Mali zao.

CHADEMA tunatoa salamu za pole na Rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Ernest Mangu kwa msiba huu mkubwa ambao sio tu kuwa ni pigo kwa taifa bali ni muendelezo wa matukio ambayo yanaashiria kuwa usalama wetu uko katika mtikisiko au mashaka makubwa .

Tunamtaka IGP afanye uchunguzi wa kina na achukue hatua stahiki juu ya matukio yote ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa raia na Mali zao hapa Nchini kwa muda mrefu sasa na yaweze kukomeshwa mara moja kwani watanzania hatujazoea matukio ya kihalifu kama yanavyoendelea kutokea nchini mwetu.

Jeshi la Polisi linatakiwa kujipanga upya ili kuzuia matukio kama haya kutokea ama kwa Polisi wenyewe au kwa raia wengine kwani hili ni jukumu Lao la msingi na wasiogope kuchukua hatua kwa yeyote anayepanga na kiratibu matukio ya kihalifu kama utekaji, utesaji na hata mauaji kama tunavyoendelea kushuhudia nchini kwa kipindi sasa kwani uhalifu hauna cheo, hakuna aliye juu ya sheria nchini mwetu.

Josephat Isango.

CHADEMA inapenda kutoa pole kwa msiba mwingine mkubwa uliolikumba taifa kwa kuondokewa na Mwandishi mwandamizi wa Habari na ambaye alikuwa na ujasiri wa aina yake katika kuchunguza na kufichua maovu mbalimbali Ndugu Josephat Isango Nghimba.

CHADEMA daima tutamkumbuka katika harakati zake mbalimbali tangu alipokuwa mmoja wa waasisi wa CHASO katika Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza alipokuwa mwanafunzi na hata alipohitimu alikuwa Mwenyekiti wa Vijana (BAVICHA ) Mkoani Singida.

Atakumbukwa kwa ujasiri wake ndani ya Chama aliposimamia kamati ya maadili ya Baraza la Vijana CHADEMA , wakati wa kushughulikia nidhamu ya waliokuwa wanachama wa Baraza hilo akina Juliana Shonza na wenzake .

Tunatoa salamu nyingi za pole kwa waandishi wote wa Habari nchini na wamiliki wa vyombo vya Habari vyote nchini kwa kuondokewa na mmoja wa mwanafamilia mwenzenu katika tasnia ya Habari.

Zaidi sana tunatoa pole kwa waliowahi kuwa waajiri wake ambao ni kampuni za Freemedia, Mwanahalisi Publishers, Victoria Media (Mawio) na Jamii Media (Jamii forums) alikowahi kufanya kazi .

Hakika sote tumeondokewa na kijana mahiri na ambaye alikuwa hana woga katika kutimiza majukumu yake na katika kupigania uhuru na haki ya kupata Habari nchini.

Mwisho tunatoa pole kwa watanzania wote kwa msiba huu ambao umetukumba sote , tunaungana na Ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu kwa familia zote zilizoguswa kwa njia moja ama nyingine na msiba huu katika Dua zetu.

John Mrema -Mkurugenzi wa Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje CHADEMA .

Imetolewa Leo Ijumaa, Aprili 14, 2017.
 
Haya mmesikika. Maana wenzetu watanzania wamekatishwa maisha yao wakiwa ktk kazi ya ulinzi. Hili hakika halina itikadi....
 
Uungwana na Vitendo. Big Up.
Namshangaa Yule Àyattollah wa ACT hanàga hizi yeye anasubiri kumkosoa JPM eti sababu aliwahi kumwambia Kinyozi akitaka kunyoa anaweza kuanzia hata kisogoni na siyo lazima mbele reference ni barabara ya Nyàkanazi hadi Kidawe Kigoma.
 
r.i.p isango tutakukumbuka kwa harakati zako
 

Attachments

  • 17884168_10207138830029461_1750986155687256515_n.jpg.jpeg
    17884168_10207138830029461_1750986155687256515_n.jpg.jpeg
    36 KB · Views: 29
Huyu Isango aliyegombea Ubunge mkoani Kagera au mwingine. Namjua yule alishitakiwa pamoja na akina TL kule Mawio na aligombea Ubunge Jimbo moja kule Kagera kama sikosei.
 
Ameni,wamekufa kishujaa wakiwa wanalitumikia taifa na hao ndio waliowekeza uhai wao kwenye taifa.
 
Isango umeniuma sana,ulikuwa unajua sana kujenga hoja,hasa kwenye midahalo.R.I.P
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

BARAZA LA VIJANA CHADEMA ( BAVICHA)

SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA POLE KWA NDUGU JOSEPHAT ISANGO- MWANDISHI,PAMOJA NA JESHI LA POLISI NCHINI.

BAVICHA tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari wa Jeshi la Polisi wanane vilivyotokea jana huko maeneo ya Rufiji Mkoani Pwani kwa kile kilichoelezwa awali kuwa ni kutokana na shambulizi la kuvizia linalosemekana limefanywa na Jambazi/ Majambazi.

Taarifa hizi sio tu kuwa ni za kuogofya bali pia ni za kuhuzunisha na kusikitisha hasa Ukizingatia kuwa ni miezi michache tu iliyopita tukio la kihalifu kama hili lilitokea maeneo hayohayo na taifa likapoteza Askari wake wengine kadhaa,kwa wakati huo.

BAVICHA Tunachukua nafasi hii kulaani kitendo hiki cha Kinyama ambacho kimepelekea kukatiza maisha ya Askari wetu ambao walikuwa kwenye majukumu yao ya kuimarisha ulinzi wa raia na malii zao.

BAVICHA tunatoa salamu za pole na rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Ernest Mangu kwa msiba huu mkubwa ambao sio tu kuwa ni pigo kwa taifa bali hata familia za polisi hao waliopoteza maisha na ni muendelezo wa matukio ambayo yanaashiria kuwa usalama wetu uko katika mashaka makubwa mno.

Tunamtaka IGP afanye uchunguzi wa kina na achukue hatua stahiki juu ya matukio yote ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa raia na Mali zao hapa Nchini kwa muda mrefu sasa na yaweze kukomeshwa mara moja kwani watanzania hatujazoea matukio ya kihalifu kama yanavyoendelea kutokea nchini mwetu.

Jeshi la Polisi linatakiwa kujipanga upya na kuboresha mahusiano zaidi na raia ili kuzuia matukio kama haya kutokea ama kwa Polisi wenyewe au kwa raia wengine kwani hili ni jukumu Lao la msingi na wasiogope kuchukua hatua kwa yeyote anayepanga na kuratibu matukio ya kihalifu kama utekaji, utesaji na hata mauaji kama tunavyoendelea kushuhudia nchini kwa kipindi kama hiki,ambacho matukio kama haya yametuacha njia panda juu ya ndugu yetu Ben Saanane.

"JOSEPHAT ISANGO"

BAVICHA inapenda kutoa pole kwa msiba mwingine mkubwa uliolikumba taifa kwa kuondokewa na Mwandishi mwandamizi wa Habari na ambaye alikuwa na ujasiri wa aina yake katika kuchunguza na kufichua maovu mbalimbali,sisi kama vijana Isango alikuwa ni mfano mzuri kwetu.

BAVICHA daima tutamkumbuka katika harakati zake mbalimbali tangu alipokuwa mmoja wa waasisi wa CHASO katika Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza ulipokuwa mwanafunzi na hata alipohitimu ukuwa Mwenyekiti wa Vijana (BAVICHA ) Mkoani Singida.

Tutakukumbuka kwa ujasiri wako ndani ya Chama na hasa pale uliposimamia kamati ya maadili ya Baraza la Vijana CHADEMA , wakati wa kushughulikia nidhamu ya waliokuwa wanachama wa Baraza hilo akina Juliana Shonza na wenzake kwa wakati huo.

Tunatoa salamu nyingi za pole kwa waandishi wote wa habari nchini na wamiliki wa vyombo vya Habari vyote nchini kwa kuondokewa na mmoja wa mwanafamilia mwenzenu katika tasnia ya Habari.

Na kwakipekee tunatoa pole kwa waliowahi kuwa waajiri wake ambao ni kampuni za Freemedia, Mwanahalisi Publishers, Victoria Media (Mawio) na Jamii Media (Jamii forums) alikowahi kufanya kazi enzi za uhai wake.

Mwisho tunatoa pole kwa watanzania wote kwa msiba huu ambao umetukumba sote , tunaungana na Ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu kwa familia zote zilizoguswa kwa njia moja ama nyingine na msiba huu katika Dua na sala zetu.

Imetolewa Leo Ijumaa, Aprili 14/2017

Edward Simbeye

Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa.r
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Huu ndio wakati wa kuonesha mshikamano wetu kama Taifa, naomba wananchi wote tutoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi.
Tunaacha tofauti zetu za vyama, kazi iwe ni kusaka hawa magaidi mpaka tuhakikishe tunawamaliza ndipo turudi kwenye mijadala ya usalama wa raia na nchi
 
Back
Top Bottom