BAVICHA watii agizo la Mbowe. Viongozi wao kufikishwa Mahakamani Dodoma leo


Weston Songoro

Weston Songoro

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2014
Messages
2,793
Likes
494
Points
180
Age
38
Weston Songoro

Weston Songoro

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2014
2,793 494 180
1.JPG

Jeshi la Polisi limekwama kuwafikisha mahakamani viongozi wanne wa Taifa wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya kukosea hati ya mashtaka.

Wanaoshikiliwa ni Mwenyekiti wa Taifa, Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, Julius Mwita, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Joseph Kasambala na Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, George Tito.

Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema makosa yametokea wakati wa uandaaji wa hati ya mashtaka.

“Mahojiano yameisha, charge sheet (hati ya mashtaka) ikaandaliwa, lakini ikarudishwa tuifanyie marekebisho. Muda umepita wa Mahakama watapelekwa kesho (leo),” alisema.

Hata hivyo, alisema kesi hiyo haina dhamana kwa upande wa kituo cha polisi na hivyo kuwalazimu watuhumiwa hao kuendelea kukaa rumande.

“Wasubiri kesho (leo) wataka- poenda mahakamani kama wataamua kuwapa dhamana,” alisema Mambosasa.
Kuhusu baadhi ya watuhumiwa hao kugawanywa katika selo tofauti za Chamwino na wengine kuachwa Kituo Kikuu cha Polisi, Mambosasa alisema huo ni utaratibu wa kawaida ambao unalenga kupata maelezo ya kila mmoja.

“Hayo ni mahojiano tu ili kila mmoja upate anasema nini ndipo unawaweka sehemu tofauti. Hizo ni taratibu za mahojiano ili wasiendelee na mawasiliano,” alisema.

Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick Ole Sosopi alisema kisheria watuhumiwa hawatakiwi kukaa rumande kwa zaidi ya saa 24.

“Cha kusikitisha siku ya leo (jana) ambayo walisema wangewaleta mahakamani kwa kile wanachoamini wametenda kosa, lakini hadi sasa muda wa mahakama unaisha viongozi wetu hawajaletwa,”alisema na kuongeza:

“Na sisi tunataka kuondoka ili tuone taratibu nyingine ambazo zinaweza kutuhakikishia usalama wa viongozi wetu. Hadi sasa viongozi wetu hawajaletwa mahakamani.”

Alisema hata kama polisi wanawaona viongozi wao wanamakosa, kisheria hawawezi kukaa na mtu kwa muda wa siku tatu bila kumfikisha mahakamani.

Alisema utendaji wa polisi nchini ni tofauti na wa nje ya nchi ambapo kwa nchi za wengine, polisi ni sehemu ya huduma na si ya mabavu.

Alisema hali hiyo inaleta kadhia na masumbuko kwa Watanzania na hivyo kupunguza imani yao kwa jeshi hilo.
Wakili wa watuhumiwa hao, Fred Kalonga alisema wamekuwa na wateja wao tangu siku walipokamatwa kwa kuhakikisha wanahojiwa kwa mujibu wa sheria.

“Kwa mujibu wa ahadi za polisi kuwa leo (jana) wanaletwa mahakamani. Kuanzia saa 1.30 asubuhi tuko mahakamani na sasa inakwenda saa 9.30 alasiri hakuna mtuhumiwa aliyeletwa. Kimsingi muda wa mahakama umeisha,” alisema.

Alisema yeye na wakili mwenzake, Azack Mwaipopo walikuwa wanakwenda kufuatilia taratibu nyingine za kisheria za kuwawezesha kupata dhamana.

“Tunakwenda kufuatilia taratibu nyingine lakini sisi tupo tayari muda wowote wakiletwa tutawadefend (tutawatetea) kwasababu tunaamini kwa mujibu wa maelezo ya wateja wetu wapo sahihi kuliko tuhuma zinazowakabili,” alisema.

Wanachama wa Chadema walikuwa katika viwanja vya mahakama tangu saa 2.00 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri baada ya kuelezwa na wakili wa watuhumiwa kuwa viongozi wa Bavicha hawatapelekwa mahakamani tena.
Viongozi hao walikamatwa Ijumaa usiku katika baa ya Capetown walipokwenda kunywa na kula chakula. Wanadaiwa kwa tuhuma za kukusudia kuikashfu Serikali.

Akizungumzia mpango wa vijana wa Chadema kuzuia mkutano wa CCM utakaofanyika Julai 23 mjini hapa, Sosopi alisema wanaiheshimu kauli ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ya kuwataka kutokwenda kuzuia mkutano huo.

“Tunaiheshimu kauli ya mwenyekiti na tunatambua kuwa vijana wengi nchi nzima wamejiandaa kwenda kuzuia mkusanyiko huo, lakini sasa tunashughulika na hili la viongozi wetu kukamatwa kwanza,”alisema.

Alisema baada ya viongozi wao kupata dhamana wataitisha kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha haraka ili kujadili suala hilo na watatoa msimamo kama wanakuja na mkakati mwingine ama kuendelea na huohuo.
 
TataMadiba

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2014
Messages
9,662
Likes
4,011
Points
280
Age
35
TataMadiba

TataMadiba

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2014
9,662 4,011 280
Nilicheka sana baada ya kusoma sababu alizozitoa kupelelekea kuahirisha zoezi hilo. Nimejifunza shule ni muhimu sana
 
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,502
Likes
27,400
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,502 27,400 280
Kama wamewashika inamaana pia kuwapeleka mahakamani kusingechelewa
 
G

geraldkowero1

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2014
Messages
1,841
Likes
298
Points
180
Age
39
G

geraldkowero1

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2014
1,841 298 180
Nilicheka sana baada ya kusoma sababu alizozitoa kupelelekea kuahirisha zoezi hilo. Nimejifunza shule ni muhimu sana[/QUO
Shule gani uliyojifunzia?Madrassa au shule gani na ulimalizia darasa la nne mwaka gani hadi kujiona ulijifunza vya kutosha hadi uone sababu za mwenzio kuwa ni kichekesho? Nae anaechekwa ni nani mbona hatajwi na mkumbuka umuhimu wa shule kipindi hiki?
 

Forum statistics

Threads 1,236,309
Members 475,050
Posts 29,253,708