BAVICHA wanakutana Kibaha kupanga mikakati ya chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAVICHA wanakutana Kibaha kupanga mikakati ya chama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jan 7, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wajumbe wa BAVICHA chini ya kamanda John Mnyika leo wako Kibaha Mjini katika warsha inayofanyika kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yahusuyo mustakabali wa vijana nchini. Warsha hiyo ya siku tatu ambayo inajumuisha sekretarieti na viongozi wengine wakuu wa BAVICHA, imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kujadili na kuweka mpango kazi wa baraza hilo, kwa mwaka 2012-2013 na maandalizi ya mkakati wa miaka mitano (2012-2016).

  Katika siku hizo tatu za warsha, baraza litajadili Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana, Sera ya CHADEMA ya Vijana, Kanuni/Mwongozo wa Baraza, utendaji kazi wa vijana wa CHADEMA 2006-2010, katiba ya CHADEMA, utendaji kazi na rasilimali za chama pia Mpango Mkakati wa CHADEMA kwa mwaka 2011-2016.

  Hongera BAVICHA Hongera Chadema.
   
 2. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera vijana wa CHADEMA kwa kutambua kuwa tunahitaji mikakati makini ili kujipanga vema kukijenga chama. Kila la kheri.
   
 3. DIALLO

  DIALLO Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  safi sana mwanzo mzuri na iwe nchi nzima
   
 4. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakitoka hapo waende vijijini kujenga chama, wasilewe na vikao vya kupanga mikakati isiyo kakatuliwa kama ya magamba
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​gud to go
   
 6. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  BAVICHA WAJIFUNGIA KUJADILI NA KUPANGA MIKAKATI KWA MAENDELEO YA VIJANA

  WAJUMBE wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), wameendelea kukutana leo katika warsha inayofanyika mjini Kibaha kwa siku ya pili, wakijifungia kujadili masuala kadhaa, wakijikita katika kuangalia mstakabali wa vijana nchi nzima, bila kujali kujali tofauti za itikadi zozote.


  Warsha hiyo ya siku tatu mfululizo ambayo inajumuisha sekretarieti na viongozi wengine wakuu wa BAVICHA, imeandaliwa maalum kwa ajili ya kujadili na kuweka mpango kazi wa baraza hilo, kwa mwaka 2012-2013 na maandalizi ya mkakati wa miaka mitano (2012-2016).


  Katika siku ya kwanza nay a pili, vijana hao, chini ya mwezeshaji na mwongoza warsha, John Mnyika, wamechambua mapungufu na udhaifu mkubwa ulioko katika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Taifa, kisha kutoa mawazo mbadala kuboresha sera hiyo kwa nia ya kuwasaidia vijana nchi nzima.

  Wametumia fursa hiyo kujadili kwa kina masuala kadhaa yanayotatiza na kukwamisha maendeleo ya kundi kubwa la vijana, hususan ukosefu wa ajira na ujira bora na wenye staha, elimu bora inayowasaidia vijana kupata utaalam na taaluma, wajibu wa vijana katika kushiriki na kushirikishwa masuala ya uongozi wan chi yao, hususan kusimamia matumizi ya rasilimali za nchi kwa manufaa ya umma.


  BAVICHA pia wamejadili namna ambavyo vijana wanaweza kuingizwa katika uchumi ulio imara na shirikishi, endapo kutapatikana uongozi bora na mfumo mpya wa utawala, ambao utaweza kuangalia sekta muhimu, kama vile kilimo, viwanda, fedha (mikopo) ambazo zikipata uwekezaji wenye maslahi kwa nchi, kundi la vijana linaweza kuinuka na kuchukua nafasi yake muhimu kwa maendeleo ya jamii.


  Katika siku hizo tatu za warsha hiyo, BAVICHA watajadili Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana, Sera ya CHADEMA ya Vijana, Kanuni/Mwongozo wa BAVICHA, utendaji kazi wa Vijana wa CHADEMA 2006-2010, Katiba ya CHADEMA, Utendaji Kazi na rasilimali za chama pia Mpango Mkakati wa CHADEMA kwa mwaka 2011-2016.


  Mbali ya hayo, vijana hao wa CHADEMA pia watatumia warsha hiyo, kujadili na kuandaa Dira (Vision), Dhima (Mission) na Misingi ya Vijana ya BAVICHA, kuandaa lengo kuu na malengo mahususi ya BAVICHA kwa miaka mitano, 2012-2016, malengo na vipaumbele kwa mwaka 2012 na kupanga bajeti.


  Imetolewa leo Dar es Salaam, Ijumaa, Januari 6, 2012
  Deogratias Mushi
  Katibu Mtendaji wa BAVICHA
   
 7. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kila la kheri
   
 8. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hongereni sana BAVICHA,siyo siri CCM wanapaswa kujizatiti vilivyo kuelekea 2015 vinginevyo hali ni tete kama spidi ya cdm itaendelea hivi
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  USHAURI WANGU KWA VIJANA WA CHADEMA:
  Mna changamato kubwa sana ktk kukijenga chama hiki kwani ukiangalia vijana nchi nzima wameamasika sana kisiasa kupitia
  chama cha chadema cha msingi cha kufanya kwa hivi sasa ni kutengeneza mtandao wa nguvu utawaunganisha vijana wote
  wa chadema nchi nzima mkifanikiwa ktk hili basi mtakuwa mmepiga hatua kubwa sana ktk harakati za kisiasa hapa nchini.

  how
  kuna kundi kubwa la vijana hapa ambao ni mashabiki na wakereketwa wa chadema lakini hawana kadi wala mawasiliano yeyote
  ya kiutendaji na chadema. kinachotakiwa kufanyika ni kuzunguka Tanzania nzima kutengeneza jeshi kubwa la vijana wa chadema kwa kuakikisha kila kijana anayo kadi na wale ambao hawana uwezo wa kununua kadi basi kuna haja ya kutumia sehemu ya pesa
  za ruzuku kuwawezesha.

  Kumpa kadi mtu sio mwisho bali kuakikisha mna uwezo wa kuwasiliana naye au yeye kuwasiliana nanyi wakati wowote kwa kupitia
  njia yeyote ile ambao ni inapatikana mfano lazima kuwa na data base ambayo itakuwa na namba za simu, email, p.o.box n.k
  na pia ni muhimu kuwa na biography ya mhusika kama elimu yake, kazi yake n.k. hii inabidi ifanyike kwa vijana wote ambao
  mtaweza kuwafikia kwa nchi nzima. hii itawasaidia sana hasa wakati wa kutafuta mawakala na kupata taarifa zozote kuhusiana
  na eneo usika kuhusiana na hali ya kisiasa kutoka moja kwa moja kwenye ground badala ya kupitia kwenye media.

  swala la media hili ni muhimu mno lazima ujumbe wenu uweze kuwafikia walengwa kwa namna mnavyotaka nyie na key ni kuwa na media zenu wenyewe ili muweze ku control message mkiteendelea kutegemea media zingine basi habari zenu zitaendelea
  kupotoshwa na hakuna wa kulaumiwa kwahiyo anzisheni harambee ya kuchangisha watu ili ujumbe wenu uweze kuwafikia watu wengi hatupendi namna vyombo vya redio na hasa TVs zinavyofikisha message zenu kwetu sisi wengine tunao uwezo wa kuwaelewa lakini wengi hawaelewi wanafikiri kuwa TV's haiwezi kudanganya. hili linawezekana mnao mda mzuri sana kuanzia sasa
  mpaka uchaguzi ujao.
  ni hayo kwa leo mkitaka servers na cheap redio system kampuni yangu inaweza kuwasaidia kuwatafutia(optional).
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Thanks mr. politiki you have said all, in addition to that, they should keep party news on air all the time, wananchi wajue chama kinafanya nini sio kusubiri wakati wa mikutano pekee, wawe wanakwenda kwenye media kutoa ratiba ya matukio muhimu ya chama.
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwanini kibaha safari hii na siyo arusha?
   
 12. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wakifanya Arusha tabu wakifanya Kibaha tabu, ulitaka wafanyie wapi au WAWI?
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mkuu nakuunga mkono asilimia mia.s
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  bado una hangover za mwaka mpya?
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  tarehe tu imebadiliki mambo ni yaleyale..
   
 16. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mkuu mie nikupongeze sana kwani umeongea kwa moyo wa uzalendo kabisa sasa tunaomba uongozi wa CDM jaribuni kufuatilia michango mizuri ya kama ya mkuu Politik
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Suala la kuanzisha media zao lipewe special paramount!
   
 18. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #18
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BAVICHA inazidi kusonga mbele, mtupe taarifa ya mipango mliyoweka.

  serayamajimbo
   
 19. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #19
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  watu wa kaskazini wanaenda kujadili mambo ya kaskazini kuhusu pasaka.kila siku majina ni yale yale ya akina mushi,lema,mnyika na mrema.hakuna wengine?wachaga bana.
   
Loading...