BAVICHA waijia juu UVCCM kwa kauli zao dhidi ya wazee

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
TAMKO LA AWALI JUU YA KAULI ZA UVCCM DHIDI YA WAZEE.

UVCCM MUWE NA NIDHAMU,ADABU NA HESHIMA KWA WAZEE.

BAVICHA imesikitishwa Sana na kauli zilizotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu ambaye Amejipa jukumu la kuwajibu wazee wa CHADEMA ambao walilaani kauli iliyotolewa na Rais mstaafu Ali H.Mwinyi ya kuchochea uvunjifu wa Katiba ya Nchi yetu.

Kauli ya UVCCM ni kauli iliyotolewa na mtu mlevi ama ambaye amevimbiwa !

Ulevi unatokana na ama Madaraka na mazoea ya huyu Kijana ambaye amekuwa mlevi Kitambo kirefu Kwani mara nyingi amekuwa Akitoa kauli dhidi ya wazee wake huko ZNZ kutokana na Ulevi huu wa Madaraka na anataka kuendeleza tabia hii ya kilevi maeneo yote ya Jamhuri.

Ni kauli za Kijana aliyevimbiwa ndio maana anajipa ujasiri wa kuwajibu wazee wake ambao walimuonya mzee mwenzao Tena kwa kutumia maneno ya Mwl.Nyerere ambaye ni baba wa Taifa letu.

Vijana wa CHADEMA tunampuuza na kumuonya kuwa aache tabia hizi za kilevi na kuvimbiwa Kwani haya sio maadili ya kitanzania hata kidogo.

Tunamuonya Shaka ambaye anabeza hata maneno ya Mwl.Nyerere aache mara moja tabia hii ya hovyo na ambayo inatuvunjia heshima Vijana wa kitanzania Kwani huu sio utamaduni wetu watanzania hasa Vijana kujibizana na wazee wetu.

Tunawataka vijana wa UVCCM waueleze UMMA kama sasa wanapingana na maneno ya Mwl.Nyerere na waueleze msimamo wao hadharani kuwa wanafuata misingi ipi na iliyowekwa na Nani.

Sisi Vijana wa CHADEMA tunaendelea kuwaunga mkono wazee wetu ambao wameishi na Kuona mengi Katika Taifa letu na wanapotoa maonyo Hatuna budi kuwasikiliza kwa umakini mkubwa na kamwe Hatutakuwa sehemu ya walevi na waliovimbiwa.

Wazazi wake huyu kijana hawana budi kumkanya na kumuonya aachane na tabia hizi za kilevi na kuvimbiwa Madaraka ili asijejichumia laana Katika umri huu mdogo.

BAVICHA tunaishangaa CCM kwa kutowafunda vijana wake , na tunaitaka imuonye kijana huyu na waanze kumfunda, ili kumuepusha na zile tabia tulizoshuhudia miaka Michache nyuma ya Kijana mmoja aliyekuwa na tabia kama hizi kujaribu kumpiga mzee hadharani.

Kwetu BAVICHA WAZEE ni kisima cha Hekima na Busara.

Imetolewa Leo tarehe 30 Juni, 2017 .

Julius Mwita
Katibu Mkuu BAVICHA.
 
Tatizo hapa ni kwamba BAVICHA yenyewe inapuuzwa sana na wananchi hivyo haina hata hadhi ya kupuuza kiongozi wa UVCCM.
 
Kwa bavicha hii useme ndo mtaji wa chadema wa vijana kuendeleza chama? Hata kundi la bavicha ambalo tungedhani lina vijana vibrant wa kujenga hoja wanaishia kuja na vi-hoja mfu hivi eti tamko. Hiki chama kinakufa kifo kibaya sana aisee
 
Bavicha try to plan policy strategic than waiting ruling part through Uvccm what are talking...people will not understand well you.find a coherent policy to consolidate your organization...be creativity stick on doing perfect.. You will be strong
 
Say what?????
 
Hii Bavicha ndo nini mbona sionagi la maana walilonalo..!! Sisi Watanzania kwa mwendo huu Magufuli atakuwa Rais wetu kwa kipindi kirefu sana maana katiba ni yetu na tunao uwezo wa kuifanyia marekebisho kumuongezea muda wa kuongoz nchi hii
 
What is uvccm's policy?? Angalau ya Chadema sasa hivi inatekelezwa na Rais wetu bila kujali chama.
 
Bavicha inaonekana strong kwa kuwa jeshi la polisi liko nyuma yenu? Na kwa kuwa mko na watawala wanaonea wapinzani?
 
Bavicha badala ya kujibu hoja,nimeona kwenye tamko lao wanamshambulia Shaka tu,hakuna cha maana
 
Back
Top Bottom