Bavicha wafika Gereza la Ruanda kumsalimia Mdude Nyagali , yeye awapa neno

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,562
217,873
Nguzo kuu ya Chadema kwa miaka yote ya uhai wa chama hiki ni umoja wao , hawa watu kwa kushirikiana kwenye mambo yao ni wa kupigiwa mfano .

Leo Viongozi wa Bavicha Wakiwemo Pambalu na mfungwa mstaafu Mwaipaya wamefika kwenye gereza la Ruanda huko Mbeya na kuonana na Mfungwa wa kisiasa Mdude Nyagali .

Mdude ametuma ujumbe kwa watu wote kwamba HAKUNA KUOGOPA WALA KUKATA TAMAA , ameomba sana kwamba mapambano ya kusaka haki lazima yaendelee

Twaha__Mwaipaya_on_Instagram:_“TAARIFA__Nje_ya_gereza_la_Ruanda_muda_huu_na_Mh._@johnpambalu__...jpg


Mungu ibariki Chadema
 
Acha aendelee kunyea debe kwa nini auze madawa!
Mwenye haki hata ateseke vipi, ataishi LAKINI mdhulumaji hataishi wala mbingu hataiona. Yupo kwa wakati mfupi ili kwa ujinga wake ajisifu kuwa ameweza kuwadhulumu haki wasio na nguvu.

Furahini mnaoteseka kwaajili ya kuitafuta haki kwa sababu majina yenu siyo madogo mbele ya Mfalme wa haki. Mafanikio baada ya dhuluma ni yenye furaha kubwa kuliko mafanikio yaliyozoeleka. Na taharuki ni kubwa kwa wanaodhulumu pale anayedhulumiwa anapofanikiwa kumshinda mdhulumaji kwa wakati usiotarajiwa.
 
Back
Top Bottom