BAVICHA: Tumesikitishwa sana na walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika. Wataka hatua kali zichukuliwe

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Leo baraza la vijana wa CHADEMA Taifa limetoa msimamo kufuatia wabunge 19 ambao wamekwenda kuapa bungeni kinyume na msimamo wa chama.

MWENYEKITI: BAVICHA tulikutana katika kikao chetu tulichokifanya kwa njia za kidijitali kujadili mustakabali wa chama chetu kufuatia kadhia hii iliyotokea katika chama.

Jambo la kwanza ambalo BAVICHA tumekubaliana ni kuunga mkono msimamo wa chama chetu, kwanza kutotambua matokeo ya uchaguzi, kutoutambua uchaguzi wote na matokeo yake yote. Huo msimamo wa kwanza ambao umekuwa ukitangazwa na chama chetu kuanzia mwanzo huo ndio msimamo wa BAVICHA.

Pili tunaunga mkono msimamo wa chama juu ya hawa ambao walienda kuapa, walioenda kinyume na muongozo wa chama chetu, tunaunga mkono msimamo wetu wa chama kwamba watu hawa waitwe hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Tunaunga mkono msimamo wa chama kwasababu kamati kuu ya CHADEMA ambayo ina uwakilishi wa vijana kwenye kamati hiyo na muwakilishi wa vijana hao ni mimi, katika vikao vya kamati kuu ya chama hatukuwahi kujadili, hatujawahi kupitisha orodha yoyote ya wabunge wa viti maalum.

Hatujawahi kujadili, hatujawahi kupitisha orodha yoyote ya wabunge wa viti maalum. Vijana wa CHADEMA tumekubaliana kuitaka tume ya uchaguzi ijitokeze hadharani iseme waziwazi orodha ya viti maalum ambayo tume inasema eti ni ya CHADEMA imetoka kwa nani katika mamlaka za chetu chetu.

Sisi kama BAVICHA kwanza tumesikitishwa sana na hawa watu walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika na taasisi yoyote na kwakuwa katibu mkuu amesema wanaruhusu maoni na mapendekezo ya wanachama ili chama kiweze kuchukua hatua, sisi kama kamati ya utendaji tumekaa na tumeamua kwa kauli moja tuishauri kamati kuu ya chama ichukue hatua kali za kinidhamu kwa watu hawa kwa ajili ya mustakabali wa chama chetu.

Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa ajili ya hawa 19 ambao walienda kuapa kama wabunge wa viti maalum, nitawakilisha mapendekezo hayo ya BAVICHA lakini kwa sasa tunaungana na wanachadema wote na watanzania ambao wanataka hawa watu 19 bila kujali nafasi, bila kujali wamefanya nini katika chama hiki lakini kwasababu ya usaliti huu lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe na chama chetu.

 
Dram drama drama, mnazidi kufanywa wajinga ili msijue nani yuko nyuma ya haya yote ambao ni Tundu Lissu na Mbowe, ...
Chadema ni Strong Party, kweli haiwezi kufa hata kwa nini. Inapitia kila njama; real party, The Going is getting tough, but as it is Tough by itself, it is still going, towards the emancipation of the motherland!!
 
Halima James Mdee Wala si MSALITI.

Kilichopo kinafichwa.

Mnyika ANAJUA kuwa SAFARI HII...BAWACHA wamekataa kuwa STAMP ya kupitisha majina "ya wabunge WANAOTAKIWA NA MWENYEKITI TU...na inner circle yake".
 
Back
Top Bottom