BAVICHA Taifa
Senior Member
- Jul 25, 2013
- 117
- 661
Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) tumesikitishwa na tunalaani kitendo cha Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA) kuufungia wimbo uitwao ‘MAMA’ ulioimbwa na Msanii wa Mziki wa Kizazi Kipya, Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego).
Mbali ya kuufungia wimbo huo, Basata limemwagiza kusitisha mara moja kupeleka wimbo huo katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwa madai ya kwamba unakinzana na Kanuni za Basata za mwaka 2018, kanuni ya 25 (6) (d) na (i);
“Baraza katika kuhakiki maadili katika maudhui ya kazi za sanaa, litajiridhisha kuwa kazi ya sanaa;
(d) Haina maneno ya uongo, uchochezi au yanayokashifu watu wengine.
(i) Haidhoofishi umoja, ushirikiano na ustawi bora wa jamii.”
Bavicha baada ya kuusikiliza wimbo huo wa
Huu ni mwendelezo wa Serikali kuweka taratibu za kisheria kwa makusudi ya kuminya uhuru wa maoni, fikra, mawazo ya kisanaa na kuwapangia maudhui wasanii katika kazi zao.
Aidha, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusu uhuru wa mawazo, Ibara ya 18 (1) ”Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.”
Uamuzi wa Basata umevunja haki hiyo ya Katiba na umeingilia haki na uhuru wa Msanii Ney wa Mitego kutoa maoni yake.
Bavicha tunatambua kuwa, Wabunge wa Chadema wakati wa Bunge la 11, walipinga kutungwa kwa taratibu hizo kwa sababu zinaminya na kuua ubunifu katika kazi za sanaa. Lakini kutokana na nia ovu ya Serikali iliyopita na wingi wa Wabunge wa CCM, sheria hizo zilipitishwa na sasa tunaona matokeo yake.
Bavicha tunawataka wasanii washikamane na kuwa wamoja katika suala hili na kupinga matumizi ya kanuni hizi mbovu ambazo zitaua vipaji vya sanaa, kuua ndoto za vijana wengi, kuhatarisha ajira za vijana wengi na mapato yanayotokana na kazi za sanaa.
Imetolewa leo Mei 06, 2021 na,
Twaha Mwaipaya
Mratibu wa Uhamasishaji,
Bavicha Taifa.
Mbali ya kuufungia wimbo huo, Basata limemwagiza kusitisha mara moja kupeleka wimbo huo katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kwa madai ya kwamba unakinzana na Kanuni za Basata za mwaka 2018, kanuni ya 25 (6) (d) na (i);
“Baraza katika kuhakiki maadili katika maudhui ya kazi za sanaa, litajiridhisha kuwa kazi ya sanaa;
(d) Haina maneno ya uongo, uchochezi au yanayokashifu watu wengine.
(i) Haidhoofishi umoja, ushirikiano na ustawi bora wa jamii.”
Bavicha baada ya kuusikiliza wimbo huo wa
MAMA
wa Msanii Ney wa Mitego hatujaona uongo, uchochezi wala kashfa yoyote zinazodaiwa na Basata kuwa sababu za kuufungia wimbo huo. Wala haudhoofishi umoja, ushirikiano na ustawi bora wa jamii yetu.Huu ni mwendelezo wa Serikali kuweka taratibu za kisheria kwa makusudi ya kuminya uhuru wa maoni, fikra, mawazo ya kisanaa na kuwapangia maudhui wasanii katika kazi zao.