Bavicha: Taarifa kwa umma mwisho wa kurudisha fomu ni trh 26 April. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bavicha: Taarifa kwa umma mwisho wa kurudisha fomu ni trh 26 April.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Apr 24, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  TAREHE YA UCHAGUZI: Uchaguzi utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 28 Mei 2011.

  NAFASI ZINAZOGOMBEWA: Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina, Wawakilishi wa BAVICHA kwenye Mkutano Mkuu wa chama na wawakilishi wa BAVICHA kwenye Baraza Kuu la chama.

  UMRI UNAORUHUSIWA KUGOMBEA: Kwa mujibu wa Katiba umri wa ujana ni kati ya Miaka 18 na 35. Mgombea anatakiwa kugombea kwenye umri unaomruhusu kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa bado na umri wa Ujana; hivyo wagombea wenye umri wa zaidi ya miaka 30 hawataruhusiwa kugombea ili kufanya viongozi wa vijana wasiwe zaidi ya miaka 35 katika kipindi chao chote cha utumishi katika BAVICHA.

  TAREHE ZA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU: Wagombea watachukua na Kurudisha Fomu kuanzia tarehe 4 Aprili hadi tarehe 26 Aprili. Fomu zitatolewa kuanzia ngazi ya Mkoa, Makao Makuu ya chama na zinaweza kupatikana kwa kubofya hapa.

  GHARAMA ZA FOMU: Kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watalipia Shilingi Elfu Thelathini Tu (30,000) kwa Fomu.Kwa nafasi za Ujumbe watalipia Shilingi Elfu Kumi tu (10,000).

  Taarifa kwa Umma

  Kauli mbiu ya BAVICHA-Vijana; Nguvu ya Mabadiliko


  John Mnyika (Mb)
  Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Vijana
   
 2. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Asante.
   
 3. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mradi wa rushwa unaanza sasa, ngoja tujipange !
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mbona mapema? TUONGEZEENI MUDA TAFADHALI!
   
 5. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  yap mkuu tupo pamoja na tutafanya kweli
   
Loading...