Upendo Furaha Peneza
Member
- Aug 7, 2014
- 8
- 95
Kama miujiza ingekuwa jambo la kujiamuria,ningeamuru mara moja mimi Upendo Furaha Peneza niwe mwanachama wa TANU YOUTH LEAGUE. Niwe miongoni mwa kina Nyerere,Sykes,Kawawa nk nishiriki agenda nzito nzito za namna ya kumuondoa kupe,beberu,kabaila,mwizi na mnyonyaji mkoloni. Najua ningepangiwa majukumu mazito yenye kujaribu moyo kwenye mstari wa mbele; vitani na kwenye mauti. NISINGEKUWA MBISHI KAMWE.
Ningemsihi tena Mungu anipeleke nyakati za kina Mandela na umoja wao wa vijana wa ANC,nijiunge nao,nifundishwe uvumilivu wakati wa mateso,tufanye vikao vya siri mafichoni,tujadili ajenda kubwa juu ya mateso ya wazawa,mauaji ya wanaharakati,vifungo kwa wasiokuwa na hatia,utoroshwaji wa rasilimali,ubaguzi wa rangi,uchumi na huduma za kijamii na mwisho tungeamua namna ya kuuweka huru umma wa mtu mweusi.
Kama ningekuwa sijaolewa kama nilivyo leo,ningeutoa muda wangu kikamilifu kwa watu wangu na kama yamkini ningekuwa mke wa mwanaharakati kama Steve Biko au Mandela,bado ningekumbukwa vyema na historia ya taifa hilo. Ingekuwaje kwa mfano kama ningekuwa frontliner pamoja na Patrice Lumumba kule Congo ya zamani? Mimi motto wa kike mimi!!!!!!!!!!!
Wakina Mandela,Steve Biko,Nyerere,Bibi Titi hatunao tena lakini dhuruma,wizi,ubaguzi,ugandamizaji,mauaji kwa wasiokuwa na hatia bado viko hai na vinaendelea. Wanaitajika kina Mandela,Patrice Lumumba,Bibi Titi wapya watakao wapigania umma wa wanyonge na kuwa tayari kuufia.
Leo Mungu kanipa fursa ya kuishi katika nyakati hizi na nimekuwa miongoni mwa wanachama wa wachama cha siasa Imara kuwai kutokea kwa karne hii na chama hicho ni CHADEMA. Natamani roho za waasisi niliowataja hapa juu zizaliwe kwenye mioyo ya vijana mbalimbali watakao kuja kuliongoza baraza hili hapo kesho kutwa. Vijana watakao ipeleka BAVICHA kwenye level nyingine ya kiukombozi wa kifikra kwa watanzania wote bila kujali itikadi zao za kidini,kisiasa,jinsi zao,ukabila,ukanda na mambo mengine yanayoweza kuigawa jamii. Kuwe na baraza moja linaloheshimika nchini.
Naheshimu sana mchango mkubwa wa viongozi wa baraza letu waliotangulia,wamelifikisha baraza letu sehemu ya kuheshimika na kuaminiwa lakini sasa tunapoelekea kutwaa ngome ya adui na kutwaa dola,ni lazima Baraza la Vijana tulikarabati zaidi. Uwezo wake wa kukabiliana na hujuma uongezeke. Bado sijasahau hujuma tulizofanyiwa Kalenga kwenye uchaguzi mdogo,bila kutoa fundisho kali kwa wazandiki hawa,hakika watatumaliza wote siku za usoni. Ni lazima tuwafanye waogope kuua,kuteka,kubaka,kudhurumu,kuhujumu,kuiba n.k.
Haki na Demokrasia ni lazima vilindwe kwa nguvu zote za baraza hili.
BAVICHA imara ndo itatoa muelekeo wa 2015,huo ni mtazamo wangu ndugu watanzania wenzangu.
Nawasilisha.
Upendo Furaha Peneza
0755462298.