BAVICHA ninayoiota usiku na mchana

Aug 7, 2014
8
0
Kama miujiza ingekuwa jambo la kujiamuria,ningeamuru mara moja mimi Upendo Furaha Peneza niwe mwanachama wa TANU YOUTH LEAGUE. Niwe miongoni mwa kina Nyerere,Sykes,Kawawa nk nishiriki agenda nzito nzito za namna ya kumuondoa kupe,beberu,kabaila,mwizi na mnyonyaji mkoloni. Najua ningepangiwa majukumu mazito yenye kujaribu moyo kwenye mstari wa mbele; vitani na kwenye mauti. NISINGEKUWA MBISHI KAMWE.

Ningemsihi tena Mungu anipeleke nyakati za kina Mandela na umoja wao wa vijana wa ANC,nijiunge nao,nifundishwe uvumilivu wakati wa mateso,tufanye vikao vya siri mafichoni,tujadili ajenda kubwa juu ya mateso ya wazawa,mauaji ya wanaharakati,vifungo kwa wasiokuwa na hatia,utoroshwaji wa rasilimali,ubaguzi wa rangi,uchumi na huduma za kijamii na mwisho tungeamua namna ya kuuweka huru umma wa mtu mweusi.

Kama ningekuwa sijaolewa kama nilivyo leo,ningeutoa muda wangu kikamilifu kwa watu wangu na kama yamkini ningekuwa mke wa mwanaharakati kama Steve Biko au Mandela,bado ningekumbukwa vyema na historia ya taifa hilo. Ingekuwaje kwa mfano kama ningekuwa frontliner pamoja na Patrice Lumumba kule Congo ya zamani? Mimi motto wa kike mimi!!!!!!!!!!!

Wakina Mandela,Steve Biko,Nyerere,Bibi Titi hatunao tena lakini dhuruma,wizi,ubaguzi,ugandamizaji,mauaji kwa wasiokuwa na hatia bado viko hai na vinaendelea. Wanaitajika kina Mandela,Patrice Lumumba,Bibi Titi wapya watakao wapigania umma wa wanyonge na kuwa tayari kuufia.

Leo Mungu kanipa fursa ya kuishi katika nyakati hizi na nimekuwa miongoni mwa wanachama wa wachama cha siasa Imara kuwai kutokea kwa karne hii na chama hicho ni CHADEMA. Natamani roho za waasisi niliowataja hapa juu zizaliwe kwenye mioyo ya vijana mbalimbali watakao kuja kuliongoza baraza hili hapo kesho kutwa. Vijana watakao ipeleka BAVICHA kwenye level nyingine ya kiukombozi wa kifikra kwa watanzania wote bila kujali itikadi zao za kidini,kisiasa,jinsi zao,ukabila,ukanda na mambo mengine yanayoweza kuigawa jamii. Kuwe na baraza moja linaloheshimika nchini.

Naheshimu sana mchango mkubwa wa viongozi wa baraza letu waliotangulia,wamelifikisha baraza letu sehemu ya kuheshimika na kuaminiwa lakini sasa tunapoelekea kutwaa ngome ya adui na kutwaa dola,ni lazima Baraza la Vijana tulikarabati zaidi. Uwezo wake wa kukabiliana na hujuma uongezeke. Bado sijasahau hujuma tulizofanyiwa Kalenga kwenye uchaguzi mdogo,bila kutoa fundisho kali kwa wazandiki hawa,hakika watatumaliza wote siku za usoni. Ni lazima tuwafanye waogope kuua,kuteka,kubaka,kudhurumu,kuhujumu,kuiba n.k.
Haki na Demokrasia ni lazima vilindwe kwa nguvu zote za baraza hili.

BAVICHA imara ndo itatoa muelekeo wa 2015,huo ni mtazamo wangu ndugu watanzania wenzangu.
Nawasilisha.
Upendo Furaha Peneza
0755462298.
 
KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,412
2,000
Wakati mwingine we sholi huwa sikuaminii na nakuona ni mtu mwenye kuamini uamuzi wako,unajua kila kitu na hauko tayari kukoselewa.
Huwa naamini kuna siku utatusaliti tu.
 
Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290
2,000
Najua ningepangiwa majukumu mazito yenye kujaribu moyo kwenye mstari wa mbele; vitani na kwenye mauti. NISINGEKUWA MBISHI

Kama ningekuwa sijaolewa kama nilivyo leo,ningeutoa muda wangu kikamilifu kwa watu wangu na kama yamkini ningekuwa mke wa mwanaharakati kama Steve Biko au Mandela,bado ningekumbukwa vyema na historia ya taifa hilo. Ingekuwaje kwa mfano kama ningekuwa frontliner pamoja na Patrice Lumumba kule Congo ya zamani? Mimi motto wa kike mimi!!!!!!!!!!!

Upendo Furaha Peneza
0755462298.

Hapo penye kuwa "mke" usijewajaribu "akina Steve Biko" wa leo...."watapiga" na kumbuka umeahidi "hautakuwa mbishi"...joke..
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,987
2,000
Hongera dada kwa ujumbe mzuri, walikuwepo kina dada kama wewe ndani ya BAVICHA waliojiita majembe ila wakaanguka, anguko la dhambi, anguko la kishetani ambapo pua hutazama juu na kisogo chini ya ardhi - hawa hawajaamka hadi leo.
 
masanjasb

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
2,364
1,195
Maneno mazuri sana,yamejaa ujasiri,hekima,kujiamini,ni jambo gumu sana kulipata kwa mwanamke hongera kwako na hongera kwa chadema kuzalisha wanawake wanaojiamini kama ww

Nikuombe kitu kimoja tu,ukipigiwa cm inayoishi na 222,9797,888,8484,usipokee ni number za mawakali wa shetani
 
Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
23,928
2,000
Lengo lako kubwa ni kupata umaarufu na jina lako kutamkwa na idadi kubwa ya watu duniani?
Waweza kuwa na busara na hekima ila Chadema wakakuharibu na kuonekana taahira.
 
wabuyaga

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,681
1,225
Kama miujiza ingekuwa jambo la kujiamuria,ningeamuru mara moja mimi Upendo Furaha Peneza niwe mwanachama wa TANU YOUTH LEAGUE. Niwe miongoni mwa kina Nyerere,Sykes,Kawawa nk nishiriki agenda nzito nzito za namna ya kumuondoa kupe,beberu,kabaila,mwizi na mnyonyaji mkoloni. Najua ningepangiwa majukumu mazito yenye kujaribu moyo kwenye mstari wa mbele; vitani na kwenye mauti. NISINGEKUWA MBISHI KAMWE.

Ningemsihi tena Mungu anipeleke nyakati za kina Mandela na umoja wao wa vijana wa ANC,nijiunge nao,nifundishwe uvumilivu wakati wa mateso,tufanye vikao vya siri mafichoni,tujadili ajenda kubwa juu ya mateso ya wazawa,mauaji ya wanaharakati,vifungo kwa wasiokuwa na hatia,utoroshwaji wa rasilimali,ubaguzi wa rangi,uchumi na huduma za kijamii na mwisho tungeamua namna ya kuuweka huru umma wa mtu mweusi.

Kama ningekuwa sijaolewa kama nilivyo leo,ningeutoa muda wangu kikamilifu kwa watu wangu na kama yamkini ningekuwa mke wa mwanaharakati kama Steve Biko au Mandela,bado ningekumbukwa vyema na historia ya taifa hilo. Ingekuwaje kwa mfano kama ningekuwa frontliner pamoja na Patrice Lumumba kule Congo ya zamani? Mimi motto wa kike mimi!!!!!!!!!!!

Wakina Mandela,Steve Biko,Nyerere,Bibi Titi hatunao tena lakini dhuruma,wizi,ubaguzi,ugandamizaji,mauaji kwa wasiokuwa na hatia bado viko hai na vinaendelea. Wanaitajika kina Mandela,Patrice Lumumba,Bibi Titi wapya watakao wapigania umma wa wanyonge na kuwa tayari kuufia.

Leo Mungu kanipa fursa ya kuishi katika nyakati hizi na nimekuwa miongoni mwa wanachama wa wachama cha siasa Imara kuwai kutokea kwa karne hii na chama hicho ni CHADEMA. Natamani roho za waasisi niliowataja hapa juu zizaliwe kwenye mioyo ya vijana mbalimbali watakao kuja kuliongoza baraza hili hapo kesho kutwa. Vijana watakao ipeleka BAVICHA kwenye level nyingine ya kiukombozi wa kifikra kwa watanzania wote bila kujali itikadi zao za kidini,kisiasa,jinsi zao,ukabila,ukanda na mambo mengine yanayoweza kuigawa jamii. Kuwe na baraza moja linaloheshimika nchini.

Naheshimu sana mchango mkubwa wa viongozi wa baraza letu waliotangulia,wamelifikisha baraza letu sehemu ya kuheshimika na kuaminiwa lakini sasa tunapoelekea kutwaa ngome ya adui na kutwaa dola,ni lazima Baraza la Vijana tulikarabati zaidi. Uwezo wake wa kukabiliana na hujuma uongezeke. Bado sijasahau hujuma tulizofanyiwa Kalenga kwenye uchaguzi mdogo,bila kutoa fundisho kali kwa wazandiki hawa,hakika watatumaliza wote siku za usoni. Ni lazima tuwafanye waogope kuua,kuteka,kubaka,kudhurumu,kuhujumu,kuiba n.k.
Haki na Demokrasia ni lazima vilindwe kwa nguvu zote za baraza hili.

BAVICHA imara ndo itatoa muelekeo wa 2015,huo ni mtazamo wangu ndugu watanzania wenzangu.
Nawasilisha.
Upendo Furaha Peneza
0755462298.

Dada Peneza, kusema kweli hii thread na contents zake zimenigusa sana. Ninashukuru kwa kutoa NENO LENYE UZIMA KWA TAIFA LETU, dada asante sana! Lakini nina imani kuwa wewe kama mwana dada bado una nafasi nzuri ya kuchangia ili hiyo BAVICHA unayo iota ili ipatikane. Kwa maneno yako yatakuwa yana mchango mkubwa hata kwa wale ambao wako njiani kuchukua form za kugombea uongozi! Asante sana dada yetu na UBARIKIWE SANA!!!
 
m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,367
2,000
Ubarikiwe dada Peneza na hakika wewe ni hazina kubwa katika chama chetu.Unastahili kutuongoza sisi vijana wenzio katika mapambano haya ya kutafuta haki na kuondoa dhuluma miongoni mwa jamii yetu
 
kisaka victpr

JF-Expert Member
Jul 28, 2014
657
195
Peneza umenena maneno makuu,ujumbe wenye kupenya mishipa yaufahamu wa kilamzalendo.Ndoto zakujitolea,zakujenga uchungu na kuililia Tz yetu kwa kuijenga,ndoto zakuiona nchi inasogea.Ndoto zakuhangaika pamoja na wananchi.Ni ndoto nzuri!IPIGANIE.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
40,448
2,000
Kama miujiza ingekuwa jambo la kujiamuria,ningeamuru mara moja mimi Upendo Furaha Peneza niwe mwanachama wa TANU YOUTH LEAGUE. Niwe miongoni mwa kina Nyerere,Sykes,Kawawa nk nishiriki agenda nzito nzito za namna ya kumuondoa kupe,beberu,kabaila,mwizi na mnyonyaji mkoloni. Najua ningepangiwa majukumu mazito yenye kujaribu moyo kwenye mstari wa mbele; vitani na kwenye mauti. NISINGEKUWA MBISHI KAMWE.

Ningemsihi tena Mungu anipeleke nyakati za kina Mandela na umoja wao wa vijana wa ANC,nijiunge nao,nifundishwe uvumilivu wakati wa mateso,tufanye vikao vya siri mafichoni,tujadili ajenda kubwa juu ya mateso ya wazawa,mauaji ya wanaharakati,vifungo kwa wasiokuwa na hatia,utoroshwaji wa rasilimali,ubaguzi wa rangi,uchumi na huduma za kijamii na mwisho tungeamua namna ya kuuweka huru umma wa mtu mweusi.

Kama ningekuwa sijaolewa kama nilivyo leo,ningeutoa muda wangu kikamilifu kwa watu wangu na kama yamkini ningekuwa mke wa mwanaharakati kama Steve Biko au Mandela,bado ningekumbukwa vyema na historia ya taifa hilo. Ingekuwaje kwa mfano kama ningekuwa frontliner pamoja na Patrice Lumumba kule Congo ya zamani? Mimi motto wa kike mimi!!!!!!!!!!!

Wakina Mandela,Steve Biko,Nyerere,Bibi Titi hatunao tena lakini dhuruma,wizi,ubaguzi,ugandamizaji,mauaji kwa wasiokuwa na hatia bado viko hai na vinaendelea. Wanaitajika kina Mandela,Patrice Lumumba,Bibi Titi wapya watakao wapigania umma wa wanyonge na kuwa tayari kuufia.

Leo Mungu kanipa fursa ya kuishi katika nyakati hizi na nimekuwa miongoni mwa wanachama wa wachama cha siasa Imara kuwai kutokea kwa karne hii na chama hicho ni CHADEMA. Natamani roho za waasisi niliowataja hapa juu zizaliwe kwenye mioyo ya vijana mbalimbali watakao kuja kuliongoza baraza hili hapo kesho kutwa. Vijana watakao ipeleka BAVICHA kwenye level nyingine ya kiukombozi wa kifikra kwa watanzania wote bila kujali itikadi zao za kidini,kisiasa,jinsi zao,ukabila,ukanda na mambo mengine yanayoweza kuigawa jamii. Kuwe na baraza moja linaloheshimika nchini.

Naheshimu sana mchango mkubwa wa viongozi wa baraza letu waliotangulia,wamelifikisha baraza letu sehemu ya kuheshimika na kuaminiwa lakini sasa tunapoelekea kutwaa ngome ya adui na kutwaa dola,ni lazima Baraza la Vijana tulikarabati zaidi. Uwezo wake wa kukabiliana na hujuma uongezeke. Bado sijasahau hujuma tulizofanyiwa Kalenga kwenye uchaguzi mdogo,bila kutoa fundisho kali kwa wazandiki hawa,hakika watatumaliza wote siku za usoni. Ni lazima tuwafanye waogope kuua,kuteka,kubaka,kudhurumu,kuhujumu,kuiba n.k.
Haki na Demokrasia ni lazima vilindwe kwa nguvu zote za baraza hili.

BAVICHA imara ndo itatoa muelekeo wa 2015,huo ni mtazamo wangu ndugu watanzania wenzangu.
Nawasilisha.
Upendo Furaha Peneza
0755462298.
Nyie Chadema, hebu acheni ujinga wenu, pelekeni majina ya wabunge wenu 19 wa viti maalum, pimeni pros na cons za kususa muone nini kina faida zaidi, hata kama sio kwa Chadema as chama, then waachieni fursa za ajira wanawake wenu 19, tena nashauri priority iwe ni kwa wale waliogombea majimboni.

Just imagine, mtu kama huyu kukosekana Bungeni?.
Acheni hizo, pelekeni majina.

P
 
MACHONDELA

JF-Expert Member
May 7, 2018
343
1,000

Nenda wewe kwa ajili yake,Badala ya huyu si umewapeleka babu tale na kibajaji?sasa shida iko wapi?
 
jamvimoto

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,021
2,000
Binafsi nakukubali sana uzuri wako,elimu yako,na jukwaa unalotumia ni tunu toshack Mungu ametujalia,kwani hufanani unafiki hata punje,Mr wako akupe moyo katika hilo kwani umechagua jukwaa la washindi lila mtu anajua hata wana ccm wanajua ni swala la muda,umeamua kisimama upande wa haki
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom