Bavicha Moro kuandamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bavicha Moro kuandamana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by OSOKONI, Feb 26, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) mkoa wa Morogoro limeandaa maandamano makubwa ya amani yatakayofanyika Machi 5, mwaka huu mkoa wa Morogoro.
  Madhumuni ya maandamano hayo ni kupinga vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya wananchi wasio na hatia.
  Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa BAVICHA, Morogoro ilisema maandamano hayo yatafanyika katika wilaya zote za mkoa wa Morogoro na kushirikisha wafuasi wa Chadema, wanaharakati, wasomi pamoja na wananchi wanaoguswa na vitendo vya unyanyasaji vya Jeshi la Polisi.
  Katika manispaa ya Morogoro, maandamano yataanzia katika ofisi za Chadema mkoa wa Morogoro, mtaa wa Konga na kupita katika mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo na kuishia katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
  Wilayani, maandamano yataanzia katika ofisi za chama hicho wilaya na kuishia katika ofisi za wakuu wa wilaya husika.
  Lengo kuu ni kufikisha ujumbe kwa Serikali na Jeshi la Polisi kiujumla juu ya vitendo hivyo vya unyanyasaji ambavyo vimekuwa chanzo cha mauaji ya wananchi wasio na hatia na hivyo kuhatarisha amani ya nchi.
  “Maandamano hayo yanafanyika huku tukirejea mauaji ya makusudi yaliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Januari 5, mwaka jana dhidi ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana kwa amani.
  Hali hiyo ilisababisha vurugu kubwa ambapo mbali ya mauaji hayo, wananchi kadhaa walijeruhiwa na wengine kupoteza mali zao.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wataambiwa hakuna kibali siunajua tena Hilo linawahusu wao?
   
 3. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Best wishes..."CHADEMA chama cha musimu"..by Jakaya M.Kikwete.
   
 4. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Yule mama RPC wa morogoro ameshapokea taarifa za kiintellegencia kuwa al-shabab watakuwepo pia so kibali hamna labda wajaribu tena mwakani!!
   
 5. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hahahah mkuu unanichekesha kweli,na ni lazima itakua hivyo,taarifa za ki intelejensia ni kwa maandamano ya amani tu,ila kwa wahamiaji haramu kama wasomali wanaingia mpaka ndani ya mikoa ya nchi lakini taarifa za kiintelejensia hazifanyi kazi!
   
 6. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  wakitoa sababu hiyo ntacheka sana kuwa wao ndo wanaogomewa
   
 7. c

  chama JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna njia nyingine ambayo mnaweza kuitumia zaidi ya maandamano? Tumieni hekima

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 8. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Nawaunga mkono
   
Loading...