BAVICHA Mkoa wa Njombe kuhusu mbunge Sugu na Katibu wa Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga kuwekwa rumande

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
TAMKO LA BAVICHA MKOA WA NJOMBE KUHUSU MBUNGE SUGU WA MBEYA MJINI NA KATIBU WA KANDA YA NYASA EMMANUEL MASONGA KUWEKWA RUMANDE BILA SABABU ZA MSINGI.

Baraza la Vijana Chadema Mkoa Njombe tunalaani vikali tabia na kitendo kilichofanywa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya Cha kuwaweka rumande Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu na Katibu wa Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.

Baraza la Vijana Chadema Mkoa wa Njombe tunaamini ktk Mahakama huru, zenye Majaji na Mahakimu huru wenye Weledi na uwezo wa kutenda haki.

Aidha Bavicha tunaamini na tunajua kwamba Jaji au Hakimu wanao wajibu kisheria wa kulinda Mamlaka ya Mahakama isiingiliwe Wala kuchezewa na mamlaka au mtu yeyote. Hii n pamoja na kuhakikisha kuwa inatenda haki kwa kufuata sheria.

Dhamana ya mtuhumiwa yeyote ktk Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni HAKI YA MTUHUMIWA NA SIYO HISANI KUTOKA KWA HAKIMU AU MWANASHERIA WA SHERIA.

Tunajua pia kwamba mtuhumiwa anaweza kunyimwa dhamana endapo kuna tishio juu ya usalama wake kutokana na kosa alilotenda kutoka ktk jamii husika. Mathalani mtuhumiwa anayetuhumiwa kusababisha ajali na kupelekea vifo inategemewa akae rumande ili kulinda usalama wake kutoka kwa raia weny hasira Kali.

Lakini Bavicha Mkoa wa Njombe tumeshangazwa kusikia kuwa Mbunge wa wananchi tena aliyechaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge yeyote mwaka 2015 akiwa ndani ya Jimbo lake eti anawekwa rumande kwaajili ya usalama wake.!! Tunajiuliza ni usalama upi??

Katibu wa Kanda ambaye ni Kiongozi wa Chama anayehudumia mamilioni ya wanachama katika mikoa mitano (5) ya Kanda ya Nyasa anaambiwaje akiwa nche kwa dhamana hakuna usalama?

Bavicha Mkoa wa Njombe tunahoji kwani watuhumiwa hawa kwa muda wote wanaishi wapi mpaka wakose usalama leo?

Tunajiuliza Hakimu mwenye Weledi wa sheria anahitaji muda wa nini kuamua uhalali wa hoja hii dhaifu?

BAVICHA MKOA WA NJOMBE tunaamini kuwa;
1. Hakimu ametumia vibaya mamlaka ya Mahakama au hajui anachokifanya au ametumwa au amejituma kuwanyima haki watuhumiwa kwa malengo ambayo anayajua mwenyewe!

2. Tunalaani vikali tabia na vitendo vya aina hii ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mbeya.

Kama alivyo sema Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mh.Jaiji Luanda katika kesi ya Gobless Lema Dhidi ya Serikali (Republic) ya mwaka 2016 kule Arusha; Hakimu Mkazi wa Mbeya asitufanye Wanasheria wote ni wajinga. Kwani vitendo vyake vinaishushia hadhi Mahakama ya Tanzania na kudhalilisha wanasheria nchini.

3. Vitendo vya Hakimu Mkazi wa Mbeya vinachochea wananchi kuichukia Mahakama na kujenga tabia ya watu kulipa visasi siyo tu kwa raia wenyewe kwa enyewe lakini pia kwa Maofisa wa Mahakama wakiwemo Mahakimu na Mawakili wa serikali wanaonajisi Mahakama.

Mwisho.
Ni rai yetu kuwa Jaji mkuu akomeshe vitendo hivi vya kutumia vibaya Mahakama kwa kuumiza viongozi na wananchi wasio na hatia kwa kutafuta visingizio vya uongo na visivyo na maana. Kumnyima dhamana mtuhumiwa na kumuweka rumande ni kumpa hukumu mtuhumiwa kabla hajasilikizwa! Na hii ni kuvunja
Katiba ya nchi kuwa mtu hata tendewa Kama mwenye Hatia mpaka asikilizwe.

Tunawaomba vijana popote Tanzania kuungana kwa pamoja kukataa na kupinga vikali bila woga utamaduni huu mpya wa Mahakama kutumika vibaya dhidi ya raia na viongozi hasa wa vyma vya upinzani.

Edwin Enosy Swalle
M/KITI BAVICHA MKOA WA NJOMBE!

https://www.facebook.com/photo.php?....396072227132097.91634.100001879700897&type=3
 
Tumefika kubaya kama taifa. This is unacceptable

Kilichofanyika ni hiki! hakimu ameamua kumpa punishment akijua fika kuwa anamuonea!
Malawi Court: It is to, be observed that once a person has been charged with an offence, he is expected to be
prosecuted for that offence, and the law requires that the accused shall be available to stand his or her
trial until the case has been concluded.) accused is presumed by law to be innocent until his or her guilt
has been proved in court and bail should not ordinarily be withheld from him as a form of punishment."
The court should, therefore, grant bail to an accused, unless this is likely to prejudice the interests of
justice.
 
Back
Top Bottom