BAVICHA mkoa wa Mwanza kufanya kikao cha maamuzi mazito leo

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
0
Ndiyo Wakuu , heshima kwenu ! Kwa mujibu wa taarifa toka kwa Mwenyekiti BAVICHA Mkoa wa Mwanza, ndg Liberatus Mulebele ni kuwa muda huu kikao cha Baraza Vijana CHADEMA mkoa wa Mwanza kinaendelea katika ofisi ya CHADEMA mkoa,maeneo ya Nyamanoro-Ilemela.

Katika kikao hicho mada kuu ni kutoa maamuzi na tamko rasmi dhidi ya uzushi na upotoshaji uliofanywa na Salvatory Magafu kwenye vyombo vya habari akimushinikiza Dkt Slaa kujiuzulu. Ki msingi huu ulikuwa utashi na mtazamo wake na wala si maamuzi ya BAVICHA Mwanza kama alivyokaririwa akisema. Kwa mujibu wa maelezo ya Liberatus, ni kwamba saa 10 jioni leo ndo muda ambao Baraza hilo litatoa tamko na msimamo wake kama taarifa kwa umma mbele ya vyombo vya habari .

MY TAKE :- NAPE CHINI YA LUMUMBA PROPAGANDA FM ACHA KUPOTEZA RASLIMALI ZA WATANZANIA KUNUNUA VIJANA HAWA WAPIGA DILI NA WACHUMIA TUMBO AMBAO WENGI WAO WAMEISHA TILIWA MASHAKA KWENYE VYAMA VYAO BADALA YAKE WEWE NA CHAMA CHAKO NUNUENI DAWA HOSPITALINI,VITANDA,VITABU,MADAWATI,MAABARA,MISHAHARA YA WALIMU,POLISI ,MADAKTARI,DADA ZETU WANAJIUZA VYUONI KWA ELFU 1, WATANZANIA WANAKUFA NJAA NGORONGORO.
 

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,223
2,000
Wachumia tumbo wapgwe stop ili wananchi waamini MABADILIKO YA KWELI
kwa bahati mbaya hawa jamaa kwa Tz ni wengi mno kila mahali na sio rahisi kuwaondoa. Ndio maana ni mara chache kusikia watu wakiongelea idadi ya wasiokuwa na ajira kwa maana ndio percentage kubwa kuliko walioajiriwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom