BAVICHA leo saa 5 kutangaza msimamo wao kuhusu Wabunge 19 wa Viti Maalum

Status
Not open for further replies.

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Kamati tendaji ya Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) usiku wa kuamkia leo imefanya kikao chake cha dharura kilichoongozwa na Mkiti wake John Pambalu.

Leo saa 5 asubuhi kinatarajia kuongea na waandishi wa habari kutoa msimamo wake juu ya kinachoendelea kuhusu wabunge wa Viti Maalumu.

“BAVICHA tumemaliza kikao cha Kamati ya utendaji taifa sasa saa 10:30 usiku. Msimamo wetu tutautangaza kesho saa 11:00 Asubuhi mbele za waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Kinondoni”. - JPambalu.

BAWACHA iko wapi?

 
Yaani BAVICHA wanakaa na wanataka kutoa 'msimamo wao' kabla ya kikao kilichoitishwa na KM tare 27 Nov 2020?

Hili saga usishangae BAWACHA nao wakakaa kikao na kutoa 'msimamo wao'. Troubled times!
Ndiyo maana nasema Mbowe alitolee msimamo ambao ni final and conclusive
 
CDM hawaishi vituko, ila hii yote inaonyesha kuna ombwe kubwa la uongozi kutoka juu ndio maana kila kiongozi wa ngazi yoyote CDM anajaribu kuropoka.
Kama CCM msivyoisha vituko kupelekeshwa na mtu mmoja Jiwe mpaka mnamuita Yesu
Kama anahusika na wale akina mama wana baraka zake, ataendelea kupiga kimya tu mpaka siku wanachama watiifu wakishakubali matokeo. Siasa ni sayansi. Siasa ni ajira. Siasa ni biashara
una hoja ya msingi, Time will tell
 
Akili gani hizi? Madhali kamati kuu itakaa kesho kwa ajili ya kujadili jambo hilo hilo, wao kutaka kuzungumza leo ni kama utovu wa nidhamu, bila kujali wanataka kuongea nini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom