BAVICHA kuzunguka nchi mzima kufanya mikutano ya ndani

. je nilipi nilishawai leta hapa la wongo je ujaona hata magazeti yameandika

Magazeti mbona yamekuwa yakiandika uongo wa kutungwa wa humu ndani mara nyingi tu.HIVI KARIBUNI MAGAZETI yaliandika habari iliyokuwa humu ya kusema Raisi kachagua meneja wa hotel kuwa mkurugenzi wa halmashauri!!! Uongo uliokuwa humu Jamiiforums.
 
Hawa nao inaelekea hawana washauri wazuri...kuna haja ya kutangaza kuwa watafanya mikutano ya ndani nchi nzima??...Why can't you learn you people?? Siasa za ujivuni zimepitwa na wakati...Kwa maoni yangu kadri mnavyozidi kupambana na dola ndivyo mnavyozidi kuonekana kuwa ni chama cha fujo....Kama mnafanya mikutano ya ndani hamna haja ya kutangaza kwani hiyo ni mikutano ya ndani...Ila ikiwa hiyo mikutano ya ndani inageuka kuwa ya uchochezi, sasa hapo ni tatizo...
Umewapa ushauri mzuri sana. Hata ile mikutano ya hadhara wangeweza kuifanya bila kuingiliwa kama hawakukurupuka na matamshi ya ovyo ya kupambana na Magufuli.
 
Habari zilizotufikia punde, Lowasa ataongozana na viongozi wakuu wa BAVICHA kwenye mikutano ya ndani ya nchi nzima
 
Sasa kama mikutano ya kikatiba imeruhusiwa kuna haja gani ya kutangaza kuwa 'sisi' tutafanya mikutano????!!!! Kwa hakika mimi CHADEMA huwa siwaelewi kabisa, kwanini mnalalalamika lalamika sana?? Yaani siku zote your drive ni kujenga picha kuwa mnaonewa why???
Pita vileeeeeeee
 
Magazeti mbona yamekuwa yakiandika uongo wa kutungwa wa humu ndani mara nyingi tu.HIVI KARIBUNI MAGAZETI yaliandika habari iliyokuwa humu ya kusema Raisi kachagua meneja wa hotel kuwa mkurugenzi wa halmashauri!!! Uongo uliokuwa humu Jamiiforums.
Sitaweza kumzungumzia mtu mwingine mimi najizungumzia mimi na taluma yangu hii habari inaukweli na soon utaona huu ukweli mdaa utatamalaki
 
Habari zilizonifikia mdaa si mrefu ni kuwa Baraza la Chama cha Demokrasia na Maendeleo BAVICHA, linatarajia kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya ndani ya kikatiba.

kwa utaratibu wataanza na Mkoa gani watotoa taarifa siku za karibuni.

Stay tune..
hivi kuna watu ajira yao siasa...hapa ndio wanapo kosea.Hawana kazi nyingine za kufanya...Rai namba moja kaongea kwa-uzuri sana,watu wakafanye kazi!
 
Hivi ukiwa kwenye siasa uruhusiwi kuwa na ajira au kujiajiri? Ni muda gani hawa watu watakuwa wanaandaa future za familia zao?
"Dont fight for success Fight to be Significant then Success will come automaticaly"
 
na huu ndo wakati muafaka wa kujenga chama tayari kwa kuchukua dola kwa uchaguzi ujao 2020,mikutano ya ndani itasaidia sana
 
Hawa nao inaelekea hawana washauri wazuri...kuna haja ya kutangaza kuwa watafanya mikutano ya ndani nchi nzima??...Why can't you learn you people?? Siasa za ujivuni zimepitwa na wakati...Kwa maoni yangu kadri mnavyozidi kupambana na dola ndivyo mnavyozidi kuonekana kuwa ni chama cha fujo....Kama mnafanya mikutano ya ndani hamna haja ya kutangaza kwani hiyo ni mikutano ya ndani...Ila ikiwa hiyo mikutano ya ndani inageuka kuwa ya uchochezi, sasa hapo ni tatizo...

Mbona UVCCM wanatangaza hamuwatolei maneno??Au hawa vijana wa UPINZANI ni wanaotokea nchi jirani??
 
Hawa nao inaelekea hawana washauri wazuri...kuna haja ya kutangaza kuwa watafanya mikutano ya ndani nchi nzima??...Why can't you learn you people?? Siasa za ujivuni zimepitwa na wakati...Kwa maoni yangu kadri mnavyozidi kupambana na dola ndivyo mnavyozidi kuonekana kuwa ni chama cha fujo....Kama mnafanya mikutano ya ndani hamna haja ya kutangaza kwani hiyo ni mikutano ya ndani...Ila ikiwa hiyo mikutano ya ndani inageuka kuwa ya uchochezi, sasa hapo ni tatizo...
Mkapa amututukana wananchi kuwa wapumbavu na malofa mbona hujasema mchochezi? Haya mwingine amesema watoto wetu ni vilaza mbona hajaitwa mchochezi?
 
Mkapa amututukana wananchi kuwa wapumbavu na malofa mbona hujasema mchochezi? Haya mwingine amesema watoto wetu ni ****** mbona hajaitwa mchochezi?

Sijaelewa hoja yako hapa Ndugu yangu...Retired President Mkapa aliwatukana akina nani??? Unaweza ukawataja hapa waliotukanwa??? Kama umefika Chuo Kikuu na hasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, neno lile lenye herufi sita alilotamka JPM siyo tusi kabisa....isipokuwa humu JF limekuzwa makusudi na detractors kwa lengo la kumchafua Rais...Sisi tukiwa pale MLIMANIupo wakati tulikuwa tunaitana kiutani kuwa wewe ni ......na hakuna aliyekuwa akichukia ...

Sasa nije kwenye hoja yako ya msingi kuhusu hili la BAVICHA...mimi nadhani (ni maoni yangu) hawa BAVICHA wanajitakia matatizo bure, kwani siasa haziendeshwi hivyo wanavyotaka wao...Huwezi kuendesha siasa kwa kuandaa mikakati ya kupambana na kushindana na dola na mamlaka ya nchi...wanachofanya BAVICHA ni uanaharakati, lakini nchi hii haiko katika mazingira ya kisiasa yanayomlazimisha mtu au watu kuendesha vitendo vya uanaharakati...Uanaharakati ulifanywa na vijana wa TANU wakati wa mapambano ya kumuondoa mkoloni...Nchi hii ilishakombolewa zamani...utawala wa mabavu wa mkoloni ulishaondolewa...sasa tunajitawala sisi wenyewe tena hivi sasa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa...Sisi watanzania hatuongozwi kwa mabavu, hatuna mauaji ya kisiasa wala ya kikabila hapa TZ...mauaji yaliyopo pekee ni yale yanayofanywa na majambazi na wale wanaowaona wenzetu albino kuwa ni 'dhahabu' kwao...

Kwa kuwa CCM iko madarakani kwa muda mrefu huwezi kusema eti chama hiki kinaongoza kwa mabavu...ukienda SINGAPORE chama kinachoongoza au kutawala kilikuwepo tangu wakati wa uhuru miaka ya 60...

Kutangaza hadharani kuwa /sisi akina Fulani' tumedhamiria kutembea nchi nzima kuandaa na kufanya mikutano ya kumchongea Rais kwa wananchi kuwa ni dikteta huyo ndiyo uchochezi wenyewe.... Kuulinganisha utawala wa sasa wa Tanzania na wakati ule wa Hitler huko Ujerumani, huo ndiyo uchochezi wenyewe tunaousema...Kama ukiwa ulaya iwe ni uingereza, ufaransa na hata huko Marekani na ukatangaza Fulani ni sawa na Hitler, hutaachwa, utashughulikiwa kikamilifu....Huko ulaya na Marekan ni almost taboo kutamka hovyo masuala ya NAZI na kufananisha na vyama vya siasa au uongozi wa nchi....

Bila shaka mikutano ya siasa ya ndani hapa Tanzania inaruhusiwa, lakini anatokea mtu anasema 'sisi akina fulani' tutatembea nchi nzima kuandaa mikutano ya siasa ya ndani...sasa sisi wengine ndipo tunaposhangaa, kwani ipo haja ya kutangaza hayo???? Mkutano wa CCM unatangazwa kwa kuwa ni mkutano mkubwa ni congress na umelenga kukabidhiana madaraka...sasa huu ni tofauti na mkutano wa ndani wa kisiasa huko Namtumbo, Mbinga, Manyara, kahama na kadhalika....CCM nao wakija humu na kutangaza kuwa watafanya mikutano ya ndani huko Karagwe, Hai sijui na wapi...tutawashangaa pia....
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom