Bavicha kutoa malezi ya kihanaharakati ya Mbowe hadi ya malezi ya kisanii ya Lowassa


K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,064
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,064 280
Ndugu zangu,

Nalazimika kujadili kujadili umuhimu wa Jumuiya za Vijana katika vyama vyovyote vya siasa, lakini maana ya Jumuiya yenyewe hiyo katika uongozi wa chama na Taifa kwa ujumla, kutokana na hali ninayoiona ikiendelea ndani ya Baraza la Vijana, wa Chadema.

Kwa maoni yangu sasa na mtazamo wangu, Bavicha ya sasa, hasa ngazi ya taifa, imeathiriwa kwa kiasi kikubwa kimtazamo tofauti wa kisiasa iliyopo baina kati ya viongozi wakuu wawili Mwenyekiti Freemani Mbowe na Mgombea wa wa urais katika uchaguzi ujao 2020, Edward Lowassa.

Bavicha yay a sasa, ipo kwenye kipindi cha mpito, kutoka umoja wa vijana wanaharakati chini ya malezi ya Mbowe kwenda kwenye umoja wa vijana wa wasanii chini ya Lowassa. Ni kipindi kigumu sana kwa vijana wanaopitia katika makuzi ya mabadiliko ya mwili, ya kutoka utotoni kwenda ukubwani, kwa maana ya balehe.

Viongozi wa sasa wa Bavicha wameamua kuendesha siasazao kisanii, kwa kumwigiza mgombea urais wao mtarajiwa wa mwaka 2020, Lowassa, pengine baada ya kubaini kwamba siasa za kihanaharakati za kina Mbowe, haziwezi kuwafikisha Ikulu mwaka 2020 kama ambavyo qwalivyoshindwa kuingia Magogono katika uchaguzi wa mwaka wa jana 2015.

Wote tumeshuhudia hivi karibuni mvutano wa jeshi la polisi na bavicha ambao waliazimia kwenda Dodoma kuisaidia polisi kuzuia mkutano wa CCM kwa madai nya kuungamkono kauli ya Rais Magufuli ya kuzuia mikusanyiko haramu hadi 2020 inakiukwa na chama chochote.

Kutoka upeo mdogo wa Bavicha na kushindwa kumwelewa Rais Magufuli wakatafsiri ndivyo sivyo kauli ya rais, kwamba haiwezekani CCM ifanye mkutano wake wa ndani tena mkutano mkuu maalum unaoruhusiwa kikatiba.

Usanii wa Bavicha ninaousema unapatika hapa, kuwa Bavicha hawajui tofauti ya kimaudhuikati ya mkutano wa ndani na mkutano wa hadhara, wakati huo huo viongozi hao hao wa Bavicha tena kwa nafasi zao ndani ya umoja wao huo walikuwa wametoka Mwanza katika mkutano mkuu na baraza kuu la Chadema kujaza nafasi katibu mkuu wa chama chao, iliyoachwa wazi na Dr. Slaa, bila bugugha yeyote kutoka kwa vyombo vya dola kwa kuwa ulikuwa mkutano wa ndani na sio mkutano wa hadhara na mkutano huo ndipo alipopatikana Dr. Mashinji.

Bavicha wanaleta usanii kwa kuwa mkutano maalum uliompata Dr. Mashinji ulikuwa wa halali ila mkutano wa CCM wa kukabidhiwa kijiji Rais Magufuli na Mwenyekiti wa sasa wa CCM na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ni haramu na unapswa kuzuiwa?

Bavicha hii ya sasa inayohamanika kujitoa katika siasa za kiuhanaharakati za Mbowe na kwenda katika siasa za maigizo za Lowassa hawana budi kujitazama upya na staili yao ya maigizo kwani wanajiondolea credibility kwa watanzania na kuonekana kama kundi la wahuni Fulani au wapiga porojo mbele ya kamera za wana habari kwa kutafuta kick kwa kulumbana na vyombo vya dola.

Rais Magufuli hajakataza mikusanyiko wala mikutano ya kisiasa yenye lengo la kujadili na kufanya shughuli za kisiasa kwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Alichokataza Rais Magufuli ni mikusanyiko ya wahuni na mikutano ya kihuni kwa kisingizio cha demokrasia.

Bavicha wanapaswa kuelewa alichopiga marufuku Rais Magufuli ni mikusanyiko na mikutano ya hadhara ya kisiasa inayobeba maudhui yaliyotangazwa na Benson Kigaila katika makao makuu ya chadema, kwamba Chadema kinaandaa mikutano na maandamano ya nchi nzima kwqa lengo la kuizuia Serikali ya Magufuli isitekeleze wajibu wake.

Rais Magufuli hajatangaza mahala kokote wala kupiga marukufu kwa chama cha siasa kutangaza sera zake, kutangaza itikadi yake kuhamasisha na kushawishi wananchi waliowengi zaidi kujiunga na vyama vyao vya soiasa kutumia soiasa za kiustaraabu.

Alichokikataa Rais Magufuli, ambacho kimsingi ndicho watanzania wanachokikataa zaidi, ni siasa za kiababe, za kutafuta shari na kusuguana na vyombo vya dola kama walivyokuwa wanataka kufanya Bavicha.
 
swissme

swissme

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Messages
13,339
Likes
17,335
Points
280
Age
18
swissme

swissme

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2013
13,339 17,335 280
UV CCM KAZI YENU NI HII.
26a60b6f31909c38b344dd447378ea47-jpg.366042


swissme
 
DuppyConqueror

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2014
Messages
9,156
Likes
4,416
Points
280
DuppyConqueror

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Joined Mar 30, 2014
9,156 4,416 280
Tusipokuwa makini muda si mrefu BaVicha tutageuka kuwa Baraza la vichaa baadala ya Baraza la Vijana chadema.
 
kivava

kivava

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Messages
5,799
Likes
4,567
Points
280
kivava

kivava

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2013
5,799 4,567 280
Mapambano hapa si hivyo ufikiriavyo,CDM inapambana kisiasa na Chama Dola ambacho hutumia dola kuisadia
Hapa panahitaji njia mbili kufanikiwa, kisiasa na kiharakati (multi pronged approach)
South Africa ANC iliendesha siasa na UMKHONTO WE SIZWE harakati na ushindi ukapatikana
 

Forum statistics

Threads 1,238,902
Members 476,226
Posts 29,336,217