Baraza la vijana CHADEMA leo linatarajiwa kuweka kila kitu hadharani katika mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika makao makuu ya CHADEMA leo.
BAVICHA ambalo kwa sasa ndiyo baraza bora kabisa la vijana nchini litaweka msimamo wake kuhusiana na ombi la Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kuwataka kusitisha msimamo wao wa kwenda Dodoma kuzuia mkutano mkuu wa CCM.
BAVICHA ambayo inaungwa mkono na maelfu ya vijana kote nchini tayari ilikwishaandikisha vijana zaidi ya 5000 kutoka sehemu mbalimbali nchini kwenda Dodoma kwa kazi hiyo.
Mkutano huo na waandishi wa habari utafanyika leo makao makuu kuanzia saa 6 nchini na utahutubiwa na viongozi wake wakuu Mwenyekiti Patrobass Katambi,Makamu Mkiti Patrick Sosopi,Katibu Mkuu Julius Mwita na Mratibu wa Baraza hilo kitaifa Edward Simbeye.
Waandishi wote mnakaribishwa!