Bavicha: Inalaani Kitendo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Itigi kufanya mauaji ya Kijana Isaka Petro Ndani ya Kanisa la Adventisti Wasabato

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
18,648
2,000
Yale masaa 48 waliyopewa na mkubwa wao yamezaa uuaji maana sheria kwao wanategemea zitapinda.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
75,943
2,000
Bavicha ndio taasisi pekee ya vijana inayokemea mauaji kwenye eneo la maziwa makuu , hongereni sana vijana
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
7,014
2,000
Walijidai kuleta sinema, eti aliyefyatua risasi alikuwa askari wnanyamapori.

Huyu jiwe anatuharibia nchi kwa kweli
 

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,598
2,000
ilikuaje alienda kufanya unyama huo na askari wa wanyamapori? majikumu ya hao askari ni yapi? au ndio akina henry masanduku (BTW good job masanduku, post zako zote na picha zimefagiwa online)
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
145,627
2,000
Maswali 10

1. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi alifuata nini kanisani?

2. Je, ni kweli mkurugenzi huyo ana ugomvi na baba wa marehemu?

3. Je, mkurugenzi ndiye aliyetoa bunduki na kumfyatulia Isaka Isaka na kumuua?

4. Polisi wanasema tukio la mauaji lilitokea wakati mkurugenzi akiwa amekimbia je, ni nani aliyefanya mauaji hayo?

4. Polisi wanasema mkurugenzi huyo alikimbia na kufunga mlango, kwa nini alifunga mlango wa kanisa?

5. Baba wa marehemu anasema alishuhudia mkurugenzi akifyatua risasi, nani anazungumza ukweli, baba au polisi?

6. Je, ni kweli kuna kesi mbili mahakamani kati ya mkurugenzi na baba wa marehemu?

7. Kulikuwa na ulazima wowote wa mkurugenzi na msafara wake kwenda kudai ushuru wa mashamba kanisani?

8. Je, ni kawaida kwa mkurugenzi kupita mtaani kudai ushuru kwa wananchi?

9. Ni kwa nini Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo ameshiriki mazishi ya Isaka Isaka na kutoa ubani wa Sh1 milioni?

10. Je, ni kwa nini polisi, uongozi wa Singida haukutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kuzungumzia sakata hilo lilipotokea siku hiyo?

Jr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom