BAVICHA inakabiliwa na nakisi viongozi mahiri au "smart" katika kujenga hoja na ushawashi kwa jamii, BAWACHA wako vizuri

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,356
45,706
Baraza la vijana CHADEMA( BAVICHA) limejulikana muda mrefu kwa kutoa vijana mahiri na wajuzi wa kujenga hoja na ushawashi katika jamii lakini kipindi cha kuanzia mwaka 2015 viongozi wake wengi na vijana wake maarufu walianza kuwa wa kiwango cha kawaida sana wasioweza kujenga hoja vizuri zikaleta fukuto katika jamii japo wamekuwa wakizungumzia mambo ya msingi kama Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Huenda hali hii ilisababishwa kwa kiasi kikubwa na uminyaji wa haki za kidemokrasia ikiwemo kuzuiliwa mikutano ya nje ya kisiasa na sheria onevu za mawasiliano,habari na takwimu lakini hata nafasi kidogo waliyopata vijana hawa wengi wao hawakuonyesha umahiri na ushawashi waliokuwa nao wenzao waliowatangulia.

CHADEMA wanapaswa kufanya mikakati makini, ya muda mrefu na endelevu kupata au kuvutia vijana wengi wenye kaliba ya John Mnyika, John Heche, Zitto Kabwe, Upendo Peneza, Rose Mayemba, Hemedi Ally, Ole Sosopi, Ephata Nanyaro, Joshua Nassari na wengine wengi wa aina hiyo katika nafasi za uongozi na uhamasishaji wa baraza hilo vinginevyo kitaenda kuwa chama dumavu kama vingine vingi kabla hata lengo lake la kushika madaraka halijatimia.

Upande wa BAWACHA wao wanaoenekana kuzidi kuimarika kila uchao japo wamepitia wimbi kubwa la kuondokewa na viongozi wake kwa mkupuo, wanazidi kuwa nguzo muhimu kwa chama ikiwaacha BAVICHA taratibu. BAVICHA isukwe upya.
 
FNUD674XsAIV0o-.jpeg

Dada wa Peter Kibatala

Kaa kweli hawa kina dada wa Chadema huwa naawaangalia kwa jicho la kipekee sana. Inatia moyo kwa mwanamke kuendelea kujitoa pamoja na mambo ya kijinga ya PolisiCCM
 
Back
Top Bottom