BAVICHA: Hatuwezi kumpongeza Magufuli kwa lolote. Kauli aliyoitoa Lowassa ni yake, sio yetu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898


- Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) wajibu mapigo kwa UVCCM. Wasema Katibu wa UVCCM huenda ana matatizo ya akili kutokana na kupotosha umma wakati akizungumzia sakata la Tundu Lissu.

- Shaka Hamdu Shaka (UVCCM) anasema Tundu Lisu anatafuta umaarufu baada kupigwa risasi? Tunataka atuambie katika shambulizi la kupigwa risasi Tundu Lisu nani alihusika. Nimwambie tu huyu na hao wenzake wajitathimini - BAVICHA

- Katika mazingira ya sasa tunategemea kuona vijana wanajitegemea kiuchumi lakini tunamshangaa Shaka (UVCCM) anashindwa kutoa hata takwimu za vijana waliofanikiwa na wenye changamoto. Anapata wapi muda wa kuzungumzia mgonjwa aliye kitandani. Tunamuonya asirudie tena - BAVICHA

- Kuhusu mzozo unaoendelea juu ya kitendo cha Mh. Lowassa kutembelea Ikulu, sisi BAVICHA msimamo wetu haupingani na uongozi wa Chama. Hatuwezi kumpongeza Rais Magufuli kwa jambo lolote lile. Kauli aliyoitoa Mh. Lowassa ni yake, sio yetu - BAVICHA

- Mh. Lowassa akiamua kurudi CCM sisi hatutaogopa wala kutetereka. Isipokuwa tutamtakia tu maisha mema ya huko CCM. Walishaondoka wengi, hata Mwenyekiti wetu aliyepita. Hatujatetereka - BAVICHA

- Sisi tunamuuliza Lowassa yeye kama Mjumbe wa kamati kuu ya chama anapata wapi uhalali wa kumpongeza Magufuli katika mazingira ambayo msaidizi wa mwenyekiti wake Ben Saanane amepotezwa na vyombo vya dola?

- Shaka atoke aseme Mhe. Tundu Lissu ametibiwa kwa pesa za Serikali kiasi gani? tulitegemea Uvccm watoke waseme tunakitaka chama chetu kiiagize Serikali kumtibu mgonjwa ambaye yuko hospitali kwa kushambuliwa akiwa kwenye majukumu yake ya Ubunge" Julius Mwita.

- Shaka anapingana na kauli ya Mh Tundu Lissu kwa uhongo na kwa ushahidi usiokuwa na uthibitisho wowote, Shaka anawadanganya Watanzania kwamba katika nchi hii Lissu sio wa kwanza kushambuliwa kwa risasi

- BAVICHA tukikaa kimya tutakuwa tunafanya Shaka aendelee kuwa kichaa,hatutaki aendelee kuwa kichaa, Kleruu hakushambuliwa kwa sababu za kisiasa

- Mh Tundu Lissu amesema ameshambuliwa kwa sababu amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli

- Tumkumbushe Shaka, Abeid Karume hakuuawa kwa sababu za kisiasa na wala hajawahi kuwa mpinzani wala mkosoaji wa Serikali iliyokuwepo madarakani wakati huo, uweze kusema aliuawa kwa sababu za kisiasa" Julius Mwita.
 
Anhaaa basi sawa wajitahidi kuongea pointi maana Siku zngne wanaongea point siku zingine pumba kama uvccm
 
Mnashindwa hata kupiga rangi hizo ofisi zing'ae kila siku mpo kwenye matamko. Na huu ugonjwa alioambukiza Lissu chama kizima wa kusema hakuna cha kuipongeza serikali ya awamu hii utawagharimu sana. Tukutane 2020, mtakapoibuka na wabunge 4 na madiwani 6 nchi nzima, na baada ya hapo hakuna cha UKIWA,BAWACHA wala BAVICHA.
 
Hapa hakuna mjadala Lowassa afukuzwe tu arudi alikotoka hatutaki watu wenye ndimi mbili. Arudi ccm akamsifu na kumuimbia nyimbo za mapambio Pogba
.
Itapendeza zaidi akiungana na familia ya mzee Nguza vikin kuimba pambio za kusifu na kuabudu.
 
Bavicha rip kazi yenu n kurecycle tu mawazo ya mbowe hata akiongea pumba ati hamuwez pongeza maendeleo yanayoonekana kwasababu mmenyimwa kuandamana (demokrasia yenu)
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom