R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,571
*Viongozi wa juu waandaliwa maandamano nchi nzima
*Yadaiwa wameshindwa kutatua kero zinazowakabili
HALI imeendelea kuwa si shwari ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya Makatibu wa Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA), kuandaa maandamano makubwa ya nchi nzima yenye nia ya kuwangoa viongozi wa juu wa umoja huo.
Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana, zinasema sababu kubwa ya kuwangoa viongozi, inatokana na kukosa mwelekeo.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Tanga, Deogratius Kisandu, ilisema hivi sasa makatibu wa umoja huo nchi nzima, wanaandaa mkakati mzito wa kuandamana.
Tumejipanga na tupo kwenye mkakati mkali wa kuitisha maandamano ya nchi nzima, ili kwanza tuhakikishe Katibu wa BAVICHA Deogratius Mushi na wenzake wanangoka kwenye nafasi ya ukatibu.
Hii ni kutokana na wao kushindwa kututetea katika matatizo yanayotukabili, tumejikuta makatibu tunafanya kazi kwa kuletewa taarifa na wenyeviti, tumechoka sasa.
Tulitarajia angetusaidia kushiriki vikao vya BAVICHA kwa mjibu wa mwongozo wa mabaraza, kwani ibara ya 6.8.6 wajumbe wa Kamati Tendaji, ambapo Katibu huyu na safu yake wamekuwa wakikiuka Katiba ya chama na kuwaita wenyeviti wa mikoa kwenye vikao vya Kamati Tendaji kama kilichofanyika Morogoro mwaka huu.
Kikao hiki, kilitakiwa kushirikisha makatibu wa BAVICHA wa mikoa kwa mujibu wa katiba na mwongozo wa mabaraza, lakini waliitwa wenyeviti wa mikoa kama fadhila ya uchaguzi uliofanyika mwaka 2011. Katika uchaguzi huo mimi nilikuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa BAVICHA.
Namshangaa sana bosi wangu huyu na inabidi nihoji hata uwezo wake wa kuliongoza baraza, maana anaposema hakuna migogoro wakati kwenye mitandao ya kijamii kama Jamiiforum, tunasoma vijana wakilumbana na hata Makamu Mwenyekiti wetu, Juliana Shoza kuonekana hafanyi kazi na safu yake, kisa ikionekana hakuna maelewano baina ya viongozi wa juu wa baraza hilo.
Kwanza katibu huyu, hatuoni alichokifanya tangu amekamata wadhifa huo, ametembelea mkoa gani nchini akaomba kukutana na viongozi wote wa majimbo na wilaya na kufanya nao vikao kwa maendeleo ya BAVICHA? Sioni kama tuna baraza ila tuna jina la baraza.
Kashindwa hata kuwatetea viongozi wa mikoa wa umoja wetu, kushiriki Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), badala yake kila anayetoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo anaingia kwenye ziara za M4C na wakongwe kuwekwa pembeni au kutokufikiriwa katika baraza.
Hapa kuna vijana waliogombea ubunge, wana uwezo mzuri kabisa wa kuwa kwenye ziara za M4C, lakini hawafikiriwi, badala ya kuwatetea leo anasema eti kuna virusi.
Alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo, Katibu wa BAVICHA Taifa, Deogratius Mushi, alisema hawezi kuzungumzia chochote kuhusiana na taarifa hiyo.
Jamani siwezi kusema lolote kuhusu madai ya huyo Katibu, andikeni alichosema tu, alisema Mushi.
KUTOKA CHADEMA TO NCCR