Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Kwa niaba ya Baraza la vijana chadema (Bavicha) Wilaya ya Geita ninalaani kitendo cha mkuu wa Wilaya Wa hai Bw Gelasius Byakanwa kuvamia na kuharibu shamba la Mwenyekiti Wa Chadema taifa Bw Freeman Mbowe.
Sisi vijana wa chadema wilaya ya Geita sio tu tumeudhunishwa na kitendo hicho cha kinyama Bali tumefedheshwa na kitendo hicho ambacho wamefanyiwa wananchi wa hai kwa pitia Muwakilishi wao na watanzania kwa jumla ambao walikuwa wanategemea chakula na Ajira, ambapo watu zaidi ya 500 walikuwa wameajiliwa kwenye kwenye shamba hilo ambapo
Mwenyekiti wetu alikuwa anaonyesha dhana na maana halisi ya uongozi bora, maana ya uongozi inasema uongozi ni mamlaka au karama ya kuonyesha njia kwa vitendo. Kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa. Uongozi kwa vitendo ulitakiwa kuungwa mkono na kila mtanzania mpenda maendeleo Wa nchi hii na sio kumdhoofisha kama wanavyofanya.
Kwa maana hiyo tulitegemea Serikali ya awamu ya tano kupitia kauli mbiu yake ya *Hapa kazi tu* wangeenda kupata darasa kwa Mwenyekiti huyo wa Chadema ambae kwa mda mwingi amaeamua kufanya kazi kwa vitendo na sio wafanyavyo viongozi wa ccm hulisemea neno hilo jukwaani na sio shambani, kwa namna hiyo tungeweza kupambana na Njaa ambayo inalikabiri taifa letu.
Lakini kwa sababu ya chuki, visasi pamoja na wivu binafsi na upeo mdogo wa uongozi wa ccm ambao wanaona kujifunza kwa kiongozi wa upinzani ni dhambi na ni kumtengenezea sifa, kutokana na dhana hiyo imesababisha kuchochea kwa umaskini kwa wananchi wetu kwa sababu ya kutokuthamini wadau wa maendeleo kwa sababu ya utofauti wa kiitikadi.
HATUA ZA HARAKA NA MAKUSUDI ZILICHUKULIWA NA BAVICHA WILAYA YA GEITA.
1)- Tunalaani kitendo hicho cha kishetani kilichofanya na mkuu wa Wilaya ya Hai maana kimeenda nje ya ubinadamu na udugu wetu kama nchi
2)- Kwa sababu suala hili linagusa kila Mtanzania kwani mazao hayo wasingetumiwa na wanachadema pekee yao Bali watu wote, wote kwa pamoja tuungane kulaani na kukemea kitendo hicho ambazo ni cha kwanza Tanzania.
Tulizoea kuona bangi zinachomwa moto sio kabeji, Nyanya Mchicha na spinachi wote kwa pamoja tukemee jambo hili lisijitokeze tena.
3)-kuanzia Leo tunamtangaza mkuu wa Wilaya wa Hai ni mtu ambae amekosa sifa za kuwa kiongozi ambazo ni ufahamu, Mwaminifu, mwenye maadili mema, Mcha Mungu, mwenye kuwaongoza watu katika msingi bora ya uongozi bila kujali itikadi, Jinsia, rangi wala ukabila.
4)-Mamlaka ya uteuzi ichukue hatua dhidi yake isipo Fanya hivyo Vijana wa Geita tutajua kuwa ile kauli mbiu ya Hapa kazi tu yalikuwa ni style ya kuombea kura ya viongozi wa ccm na Usanii kama ile kauli mbiu ya 2005 ya maisha bora kwa kila Mtanzania na tutawaka kuipuuza.
Kwa sababu ya Umuhimu (serious) ya hili jambo tuumeamua kuitisha kikao cha haraka cha Kamati ya Uratibu ya Bavicha Geita ambacho kitakuwa ni jumamosi ili kuona ni hatua gani za makusudi na haraka ya kuchukua ili kukomesha kitendo hiki kisije kikatokea tena.
imetolewa na; Ni Mimi Mhere Mwita,
M/kiti wa Bavicha (W) Geita,
Tarehe 15/06/2017.
Mawasiliano 0742530600