Batuli actres aka Cleopatra atoa siri za waigizaji wenzake wa kike.

father-xmas

JF-Expert Member
Mar 23, 2010
788
615
batuli..png

MWIGIZAJI wa kike wa filamu Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefunguka kwa kuongelea ugomvi na chuki ambazo zimekuwa zikiripoti kwa akina dada kutoka Bongo movie sababu kubwa ni ugomvi wa kuibiana wanaume mapedeshee ambao wamekuwa wakiwaweka mjini kwa kuwapangia majumba na kuwapatia magari wakitanua nayo mjini.

“Chuki yetu wasanii wa Bongo movie ni kuchukuliana mabwana yaani mtu ukiwa na mtu anayekusaidia huwezi kabisa kumtambulisha kwa shoga yako kwani ukimpa mgongo tu si wako huyo tena, naongea bila uoga tunahitaji maisha mazuri lakini filamu hazilipi hivyo ukiona msanii wa kike anafanya kitu lazima ujue nyuma yake kuna mtu na si kwa ajili ya malipo ya filamu ni mapedeshee hao,”
anasema Batuli.

Lakini pia Batuli anawalaumu sana wasanii wenzake wa kike kwa kukosa ubunifu na kutotumia fursa wanazopata kutoka sehemu mbalimbali hata serikali pia, msanii huyo amedai kuwa kuna msanii aliwahi hata kupata mwariko kwa rais wa nchi nyingine lakini kutokana na uwezo wake wa kutokufiri hakwenda kuonana na rais, hivyo Batuli anasisitiza kuwa hakuna msanii wa kike anayeweza kusimama kama yeye zaidi ya kuwategemea mapedeshee waliojificha nyuma yao
 
Swali langu kwa dada BATULI actress aka Cleopatra ni;

1. umesema filamu hazilipi ndio maana wenzio wana mapedeshee ili wajikimu kimaisha,sasa wewe dada yangu unatumia mbinu gani ktk kujikimu na maisha ilihali kazi uliyo nayo ni uigizaji ambao umesema haulipi? Batuli aka Cleopatra
 
Last edited by a moderator:
Hakuna uongo kwenye hili kila mtu nishahidi kwenye hili.
 
Swali langu kwa dada BATULI actress aka Cleopatra ni;

1. umesema filamu hazilipi ndio maana wenzio wana mapedeshee ili wajikimu kimaisha,sasa wewe dada yangu unatumia mbinu gani ktk kujikimu na maisha ilihali kazi uliyo nayo ni uigizaji ambao umesema haulipi? Batuli aka Cleopatra

Mkuu kama umemsoma vizuri na yeye maisha yake yanategemea hao wanaoitwa mapedeshee. Kaeleza ukweli bila kumung'unya maneno.
 
Last edited by a moderator:
Utawasikia mbali na sanaa mimi nina biashara zangu nyingine zinazoniweka mjini.kumbe hakuna lolote. Siku mapedeshee tukigoma kuhonga hakika maisha ya watu wengi yataathirika.
 
Hiyo picha yako ni mtego wa kuwapata mapedeshee wa JF.

.
 
Why she's still quiet till now? She was Online today, and I know this is her favorite Forum.

[h=5]Total Posts[/h] Total Posts 63 Posts Per Day 0.81 [h=5]Visitor Messages[/h] Total Messages 0 Most Recent MessageNever
  • Visitor Messages for Batuli aka Cleopatra
  • Post a visitor message for Batuli aka Cleopatra
[h=5]User Notes[/h]
[h=5]General Information[/h] Last Activity Today 09:39 Join Date 16th September 2013

Cc: @Batuli aka Cleopatra

I think this is just a Kick...
 
batuli..png

MWIGIZAJI wa kike wa filamu Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amefunguka kwa kuongelea ugomvi na chuki ambazo zimekuwa zikiripoti kwa akina dada kutoka Bongo movie sababu kubwa ni ugomvi wa kuibiana wanaume mapedeshee ambao wamekuwa wakiwaweka mjini kwa kuwapangia majumba na kuwapatia magari wakitanua nayo mjini.

“Chuki yetu wasanii wa Bongo movie ni kuchukuliana mabwana yaani mtu ukiwa na mtu anayekusaidia huwezi kabisa kumtambulisha kwa shoga yako kwani ukimpa mgongo tu si wako huyo tena, naongea bila uoga tunahitaji maisha mazuri lakini filamu hazilipi hivyo ukiona msanii wa kike anafanya kitu lazima ujue nyuma yake kuna mtu na si kwa ajili ya malipo ya filamu ni mapedeshee hao,”
anasema Batuli.

Lakini pia Batuli anawalaumu sana wasanii wenzake wa kike kwa kukosa ubunifu na kutotumia fursa wanazopata kutoka sehemu mbalimbali hata serikali pia, msanii huyo amedai kuwa kuna msanii aliwahi hata kupata mwariko kwa rais wa nchi nyingine lakini kutokana na uwezo wake wa kutokufiri hakwenda kuonana na rais, hivyo Batuli anasisitiza kuwa hakuna msanii wa kike anayeweza kusimama kama yeye zaidi ya kuwategemea mapedeshee waliojificha nyuma yao

Hivi JF nako kuna mapedeshee

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom