Battle: Watu wenye akili ya maisha na watu wenye akili za darasani

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,179
3,539
Kuna sehemu nimepita ndugu nimekutana na mjadala mkali miongoni mwa vijana.

Mjadala unahusu watu wenye akili za darasani yaani wale wasongo au vichwa darasani na watu wenye akili ya maisha lakini darasani hawako vizuri.

Wale wenye akili darasani wanajisifu kwa usomi wao na ndio wanaoongoza nchi na wanawaponda wasioenda shule na kwamba hawaijui dunia vizuri.

Wenye akili za maisha wanawaponda wenye akili darasani licha ya usomi wao wengi wako mtaani na majumbani kwao Bado wanasubili ajiraa na wengine wameenda mbali zaidi wanasema wasomi wengi wakishastaafu elimu yao ndio inaishia hapo na wanarudi katika hali ya kawaida.

Je wewe upande wako unasemajeee
 
Hii mada ni maumivu kwangu, nimekomaa na elimu pesa hamna, kuna jamaa nilimaliza nae darasa la saba yupo vizuri kweli kipesa. Zaidi tena baada ya kumaliza my first degree niliajiriwa na mtu aliyeishia form two na sasa ni tajiri, inauma sana.

Vyovyote iwavyo elimu lazima itafutwe sana tu kwani huwa najiuliza sana mbona hao matajiri wasio na elimu huwa wanasomesha sana watoto wao tena kwa gharama yoyote, iwe nchini au nje ya nchi
 
Akili ya maisha ni directly proportion na akili ya darasani. Ni suala la mtumizi tu ya hiyo akili na kuzidiana ujanja
 
Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida Ukiona Mwenye elimu Yupo Yupo anasubiri ajira bas anauwakika wa pakula na kulala. wapo wenye elimu na wana Akili za Maisha. Na wasio na elimu wasio na Akili ya Maisha.

Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida. Haijalishi umesoma au hujasoma

Shida huleta maarifa
 
Hata Lipumba ana akili za darasani lakini hana akili za maisha.(kutatua matatizo yake)

Watu waliokuwa na akili za darasani wana maisha ya kawaida au hata ya kimaskini (hii ni kwa huku africa) kuliko wale waliokuwa na akili za kawaida au (vilaza)
 
Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida Ukiona Mwenye elimu Yupo Yupo anasubiri ajira bas anauwakika wa pakula na kulala. wapo wenye elimu na wana Akili za Maisha. Na wasio na elimu wasio na Akili ya Maisha.

Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida. Haijalishi umesoma au hujasoma

Shida huleta maarifa
smart
 
Kila kiumbe kita teremshewa rizki na pato maalum kadri ya uhai atakao ishi...
( elimu haidhamini... na wala Nguvu za mwili hazi thubutu kufikia matakwa )
KM:-
Mmiliki wa azam hakusoma zaidibdarass la nne!!
Profesaz wengi ni mafukara wa kutupa!!

just trust you creator
 
Hii mada ni maumivu kwangu, nimekomaa na elimu pesa hamna, kuna jamaa nilimaliza nae darasa la saba yupo vizuri kweli kipesa. Zaidi tena baada ya kumaliza my first degree niliajiriwa na mtu aliyeishia form two na sasa ni tajiri, inauma sana.

Vyovyote iwavyo elimu lazima itafutwe sana tu kwani huwa najiuliza sana mbona hao matajiri wasio na elimu huwa wanasomesha sana watoto wao tena kwa gharama yoyote, iwe nchini au nje ya nchi
Daaa mkuu aiseee huyo jamaa uliyemaliza nae la saba saivi mkikutana huwa mnazungumza maongezi ya aina gani
 
Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida Ukiona Mwenye elimu Yupo Yupo anasubiri ajira bas anauwakika wa pakula na kulala. wapo wenye elimu na wana Akili za Maisha. Na wasio na elimu wasio na Akili ya Maisha.

Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida. Haijalishi umesoma au hujasoma

Shida huleta maarifa

Ukweli usiopingika!!
 
Akili ni ile ile - hakuna akili ya darasani na akili ya Maisha. Kinachotegemea ni jinsi gani unaitumia hiyo akili - kama ulikuwa tu na akili ya darasani - halafu ukawa mvivu kuitumia akili hiyo hiyo kwenye maisha - ni lazima utafeli tu. Na huyu ambae alikuwa mvivu darasani kuitumia akili yake - na akaenda kuitumia vizuri akili ile ile kwenye maisha - lazima atafanikiwa tu. Lakini kama uliitumia akili vizuri darasani - na ukaitumia akili hiyo hiyo vizuri kwenye maisha - lazima utafanikia. Wako watu wengi tu waliokuwa wanafaulu darasani na wana maisha mazuri tu. Hivyo "determining factor" ni jinsi gani unaitumia hiyo hiyo akili.
 
Acha uvivu kijana.. piga shule.. maisha ya ujanja ujanja tunakoelekea yanapotea..
 
Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida Ukiona Mwenye elimu Yupo Yupo anasubiri ajira bas anauwakika wa pakula na kulala. wapo wenye elimu na wana Akili za Maisha. Na wasio na elimu wasio na Akili ya Maisha.

Akili ya Maisha inakuja Ukipata shida. Haijalishi umesoma au hujasoma

Shida huleta maarifa
Kula like Lasagna
 
Acha uvivu kijana.. piga shule.. maisha ya ujanja ujanja tunakoelekea yanapotea..
Baada ya kumaliza unaenda kuajiriwa na usipoajiriwa unakuwa na maisha ya ujanjaujanja vilevile?

Mfumo wa elimu ni mbovu only kama unatambua unachokitafuta shule au kujua kwanini unasoma at least unakuwa useful kwa 50%.

Kama unasoma mradi umepelekwa shule basi mfumo unakuharibu mara mbili bila wewe kujua kama wasomi wetu.
 
Huo mjadala inabidi na joseph msukuma ashiriki atwambie kuhusu wale maprofesa wanane aliowabwaga huko geita

Babu tale nae hata form 4 hana cheti. Ila kaangusha professor na wasomi kibao katika kura za maoni tu...na ubunge kashinda...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom