Battle: Magufulians vs Anti-Magufuli

Binafsi mwanzo alivyoingia madarakani ki ukweli kabisa sikumpemda nikawa nasema huyu ni Rais gani mbona mmbabe lkn baada ya mwaka mmoja ki ukweli nilimpenda bure nilimwelewa sana..

Kilichonifanya nimwelewe ni haki sawa kwa wote. Wenye nacho na wasiokuwa nacho. Ni kweli binadamu hatuwezi kuwa sawa kwenye suala zima la kipato kikubwa wapo wenye vidogo bali sote ni binadamu heshima iwepo. Unaenda kupata huduma anaangaliwa yule mwenye nacho wewe usiyenacho unasubiri benchi.

Ukipelekea kesi yako polisi anayesikilizwa na kuaminiwa ni yule mwenye pesa. Kipindi cha utawala wake hayo hayakuwepo una hela basi uwe na nidhamu na pesa zako.

Japo kila binadamu ana mapungufu yake,, yalikuwa machache kuliko mazuri aliyofanya. Mungu amrehemu kule aliko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi sikumpigia kura mwaka 2015 kwani nilichoshwa na CCM pia niliamini Magufuli asingekuwa na power ya kupambana na watabe wa CCM, pia nilikuwa na mentality ya kusema hapa Tanzania Rais hata awe nani hatuwezi kubadilika, kumbe bhn nilikuwa najidanganya, aisee Rais ni mtu mwenye mchango mkubwa sana katika kuamua kuleta ama kutoleta maendeleo ndani ya nchi. Tumeona uwepo wa Magufuli ulibadilisha kila kitu na ukaleta mwanzo wa Tanzania mpya.

Leo hii tunaona serikali inavyopambana kufanya makubwa ili tu ioneshe wananchi kwamba inaenda na speed ile ile ya Magufuli, kwa kifupi Magu ameenda lkn ameacha alama kubwa sana ndani ya nchi yetu ambayo pengine ingechukua hata karne kuitimiza, tumshukuru Mungu kwa uwepo wake na hakika mtu yule hajatuacha watupu, mana hawa viongozi kila wanapotaka kupiga lkn wanakumbuka SGR bado haijaisha, ndege bado hatujamaliza deni, bwawa halijaisha, Dodoma haijakamilika, Busisi bado haijakamilika, n.k n.k

Kwa pamoja tumuombe mwenyezi Mungu ampumzishe mzee wetu kwani taifa halimdai kabisa mzee yule.
 
Hakika tuendeleee tu kumuombea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kumkubali huyu mtu kabisa
Sikuzielewa sera zake za kiuchumi
Na nyinginezo
 
Kwenye ukweli usemwe tu Magufuli alikuwa mwanaume na nusu. Yaaan yule angetuongoza miaka kumi maendeleo tungeweza kufikia nchi zilizoendelea.

Enzi za Magu ilikuwa ukienda ofisi za umma huwezi kumkuta mtu yupo nje wakati wa kazi. Lkn sasa hizi mtu kafika saa mbili ,,,saa tatu yupo nje anapiga stori. Na wale wanaolia oooh mara kawafilisi wafanyabiashara wengi wakubwa huwa hawana utamadumi wa kulipa kodi kwa sababu ya connection zao. Mzee baba akaona ujinga kama unafanya biashara risiti za kulipa ushuru si unazo kama hazipo unapigiwa kuanzia pale ulipanza biashara.

Ni rais aliyeacha alama kwenye mioyo ya watu. Hata CCM wote waliompenda na hata wale ambao walikuwa hawampendi wanajua Magu alikuwa Rais anayependwa kuliko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom