Battle: Dar es Salaam vs Nairobi

HIFADHI YA TANZANIA YA SERENGETI YATANGAZWA KUWA BORA DUNIANI

4 Machi 2021


Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania imechaguliwa kuwa mshindi wa vivutio vya utalii duniani na kampuni ya Tripadvisor.

Tuzo hizo hutolewa na kampuni hiyo inayoshushughulika na kutoa mrejesho wa mahoteli na vivutio mbalimbali duniani.

Hifadhi tatu nchini Tanzania zimeibuka kidedea kati ya hifadhi 25 zilizotajwa kwenye tuzo hizo Serengeti ikishika nafasi ya kwanza duniani Hifadhi ya Masai Mara ya nchini Kenya imeshika nafasi ya tatu huku mbuga ya wanyama Tarangire ikishika nafasi ya 14 na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikishika nafasi ya 12.

Akizungumza na BBC Dira ya dunia Waziri wa Mali Asili na utalii nchini Tanzania Dkt Damas Ndumbaro amesema tuzo hiyo ni yenye umuhimu mkubwa kwa Serengeti na secta ya utalii nchini Tanzania na Afrika Mashariki.


"Tuzo hii tumepata ushindi kutokana na kazi nzuri tunayo ifanya ya kuhifadhi mbuga hii maarufu ya Serengeti,lakini pia na huduma bora ukiwa Serengeti unaweza ukaona Wanyama kwa urahisi na vizuri zaidi"

Serengeti pekee kwa mwaka hupokea wastani wa wageni laki tatu na nusu hadi laki tano ambao huja kushudia maajabu yaliyoko kwenye eneo hili ambalo ni urithi wa dunia ikiwa na na ukubwa wa kilomita za mraba 14750 kila mwaka hushuhudia mamilioni nyumbu ambao wanahama kutoka hifadhi Masai mara nchini Kenya ambayo nayo kwenye tuzo hizi imeshika nafasi ya tatu.

Utalii kama zilivyo sekta nyingine kote duniani umeathirika na uwepo wa maradhi ya Covid-19.

Mamlaka ndani ya hifadhi zimejiwekea mkakati maalumu kuhakisha wageni wanakuwa salama muda wote wawapo hifadhini ikiwa ni Pamoja na kuweka kituo cha ukusanyaji wa sampuli, kwa ajili ya upimaji wa virusi vya corona ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti mamlaka zinasema lengo ni kuharakisha upimaji lakini pia kuwapatia muda wakutosha wageni kuwa hifadhini.


Mhifadhi mkuu wa Serengeti Masana Mwishawa anasema kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kituo hicho maalum ndani ya hifadhi hukusanya sampuli ambazo hutumwa kwenye maabara ya taifa jijini Arusha kila siku na wageni kutumiwa majibu na vyeti vyao vya uthibitisho kwa njia ya mtandao.

Tanzania imekuwa ikikosolewa kwakutotoa hadharani takwimu za maambukizi ya virusi vya corona nchini humo toka ilipofanya hivyo mwezi aprili mwaka 2020 na hata msimamo wake juu ya chanjo ya maradhi hayo ambayo inaendelea kutolewa maeneo mengine duniani.

Kwa sasa Serengeti inasheherekea ushindi wake katika kipindi hiki kigumu duniani huku ikiendelea kujizatiti kuhakikisha usalama wa wageni wake jambo ambalo linawapa watalii Imani ya kuendela na mipango yao ya kutembelea mbuga za wanyama Tanzania na hata visiwa vya Zanzibar.

Screenshot_20210305-084834.jpg
 
Khaaa🙄🙄Wivu utawaua wakenya he is the best and the most respected president in the whole of Afrika 🙂kama ulikua hujui soon atakua mpatanishi wa vita vya uchaguzi Kenya🙂
Anaheshimiwa na nani? The guy is a joke. Nobody takes him seriously. He is a clown 🤡🤡🤡🤡. The only good thing about him ni kwamba anajenga miundombinu. Ni rais mzuri kwa kujenga infrastructure lakini ni rais mbovu sana likija kwenye suala la uhuru na demokrasia na pia kwenye suala la corona amefanya upuzi sana kusema kwamba corona haipo ilhali Malazy wanakufa left right kama nzi. Mjikinge kwa kuvaa mask na mkubali chanjo. Wacheni ushamba.
 
Anaheshimiwa na nani? The guy is a joke. Nobody takes him seriously. He is a clown . The only good thing about him ni kwamba anajenga miundombinu. Ni rais mzuri kwa kujenga infrastructure lakini ni rais mbovu sana likija kwenye suala la uhuru na demokrasia na pia kwenye suala la corona amefanya upuzi sana kusema kwamba corona haipo ilhali Malazy wanakufa left right kama nzi. Mjikinge kwa kuvaa mask na mkubali chanjo. Wacheni ushamba.
Na atawanyoosha hadi mnyooke (mmeanza kunyooka)
Na akimaliza muda wake anawekwa kama yeye yaani tunatoa chuma tunaweka chuma
 
Anaheshimiwa na nani? The guy is a joke. Nobody takes him seriously. He is a clown . The only good thing about him ni kwamba anajenga miundombinu. Ni rais mzuri kwa kujenga infrastructure lakini ni rais mbovu sana likija kwenye suala la uhuru na demokrasia na pia kwenye suala la corona amefanya upuzi sana kusema kwamba corona haipo ilhali Malazy wanakufa left right kama nzi. Mjikinge kwa kuvaa mask na mkubali chanjo. Wacheni ushamba.
Si ni wewe uliyesema kwamba Magu alitumia mbinu nzuri sana kutangaza covid haipo na ndiyo maana watalii wanamiminika au sio wewe nikuletee evidence
 
Si ni wewe uliyesema kwamba Magu alitumia mbinu nzuri sana kutangaza covid haipo na ndiyo maana watalii wanamiminika au sio wewe nikuletee evidence
kashageuka huyo....

wakenya huwa hawajui kuongea speech na kuzichanganua kiundani....

hata ukiwaambia kauli kama hii..."YA KALISALI MWACHIE KALISALI,,,,"..

wataelewa hivyo hivyo kama jinsi neno lilivyo,,,Na kuchukua action watatoa kila kitu ndani kisha watampelekea kalisali
 
Back
Top Bottom