Jewel
Senior Member
- May 1, 2008
- 176
- 62
mlevi mmoja kila siku akirudi nyumbani anampiga mkewe bila sababu, kila siku anamwambia kesho nikirudi nikukute haupo na ubebe kila kitu chako unacho kipenda humu ndani, basi siku mbili zimepita anasema maneno hayo hayo, siku ya tatu amerudi amelewa hajitambui, mama akawaambia watoto wake hela ya chakula hiyo hapo mimi naondoka na baba yenu tatizo lolote muende kwa bibi, basi mke akambeba mumewe mpaka kwao(kwa upande wa mke) mumewe alipo zinduka akamuuliza "niko wapi hapa" mke akajibu: upo kwetu si uliniambia ni ondoke na kila ninachokipenda na hakuna kingine zaidi yako wewe.. ndio maana upo hapa.... kuanzia hapo na mume pombe akaacha na mapenzi yakarudi kwa familia yake.... (kuna watu tunapenda vibaya.....lol....)