Elections 2010 Batilda Burian karibia anadata jamani... Mlio karibu naye msaidieni

Mwanazuoni

Member
Nov 12, 2008
69
12
Nilikua nasikiliza BBC mcahan huu huyu mama mgombea wa Arusha alikua anahojiwa na BBC kuhusu green guards wa CCM.
Ajabu ameshindwa kujibu lolote...anongea kwa panic na anachodai ni kuwa hata Chadema wana Red Brigades ambao wamefundishwa mafunzo ya kijeshi.

Anadai yeye tayari ana kura 9000 za maoni hivyo ana 50% ya kura za Arusha. Lema yeye kateuliwa tu na mwenyekiti wake na kupachikwa Arusha.

Duh! anavyoongea utadhani hana PhD

Nadhani baada ya uchaguzi hospitali nyingi zitajaa wagonjwa wengi wanaosumbuliwa na pressure including huyu mama

Kazi nzito
 
Keshatumika na wajanja sasa anaona anaukosa ubunge hivi hivi ilhali watu washamlamba kwa saaaaaaaaaaaaana tu
 
Nilikua nasikiliza BBC mcahan huu huyu mama mgombea wa Arusha alikua anahojiwa na BBC kuhusu green guards wa CCM.
Ajabu ameshindwa kujibu lolote...anongea kwa panic na anachodai ni kuwa hata Chadema wana Red Brigades ambao wamefundishwa mafunzo ya kijeshi.

Anadai yeye tayari ana kura 9000 za maoni hivyo ana 50% ya kura za Arusha. Lema yeye kateuliwa tu na mwenyekiti wake na kupachikwa Arusha.

Duh! anavyoongea utadhani hana PhD

Nadhani baada ya uchaguzi hospitali nyingi zitajaa wagonjwa wengi wanaosumbuliwa na pressure including huyu mama

Kazi nzito

Kwani Jimbo la Arusha Mjini lina wapiga kura 18,000 tu? Mbona anajibu as if hajaenda shule kabisa?

Ninaona dalili zote za mchezo mchafu kwenye kura za maoni, maana hayo majibu yake yanaashiria kwamba alitarajia akishapitishwa na CCM kuwa mgombea basi angepashinda kwenye uchaguzi mkuu.
 
Mimi namshauri tu asubiri viti maalum atapoteza maisha bure kwa pressure, siyo kila aliyesoma anao uwezo wa kuongoza jamani.
 
Mimi namshauri tu asubiri viti maalum atapoteza maisha bure kwa pressure, siyo kila aliyesoma anao uwezo wa kuongoza jamani.

Viti Maalum ameishachelewa maana vyote vimejaa. Alishauriwa vibaya na Lowassa akitarajia kwamba angeshinda kirahisi. Sasa labda asubiri vya kuteuliwa iwapo JK atabahatika kushinda vinginevyo ndo imekula kwake.

Hata wale walio shinda viti maalum nao kwa sasa matumbo yako moto, maana hawataweza kupata viti 100 kama walivyozowea, mwaka huu imekula kwao. Kwa hiyo wale walioshika nafasi za pili kwenye uwakilishi wa mikoa kuna hatihati ya kwenda mjengoni.
 
Kwa historia ilivyo, kinamama wengi wamekuwa waoga kugombea.

Mimi naomba nimpongeze mama Buriani kwa moyo huu wa kishujaa, tukumbuke kuwa hakusubiri vitu maalu...oh sorry viti maalum.

Kwa heshima kwa wanawake na kuwaunga mkono kwa kuingia kwenye mapambano siwezi kumshambulia.

Mwisho naamini CHADEMA imeshachuka jimbo la AR mjini, tunasubiri kuthibitisha tu 31 October.

TUACHANE NA HAWA KINAMAMA JAMANI, TURUDI KWA FISADI JK DAKTARI WA UFISADI.
 
Nilikua nasikiliza BBC mcahan huu huyu mama mgombea wa Arusha alikua anahojiwa na BBC kuhusu green guards wa CCM.
Ajabu ameshindwa kujibu lolote...anongea kwa panic na anachodai ni kuwa hata Chadema wana Red Brigades ambao wamefundishwa mafunzo ya kijeshi.

Anadai yeye tayari ana kura 9000 za maoni hivyo ana 50% ya kura za Arusha. Lema yeye kateuliwa tu na mwenyekiti wake na kupachikwa Arusha.

Duh! anavyoongea utadhani hana PhD

Nadhani baada ya uchaguzi hospitali nyingi zitajaa wagonjwa wengi wanaosumbuliwa na pressure including huyu mama

Kazi nzito

Mtasema sana mwaka huu. Lakini Shemeji etu ndio MBUNGE hapo Arusha.
 
Anadai yeye tayari ana kura 9000 za maoni hivyo ana 50% ya kura za Arusha. Lema yeye kateuliwa tu na mwenyekiti wake na kupachikwa Arusha.

Wapigakura waliojiandikisha mwaka 2005 walikuwa ni zaidi ya 120, 000 na hivi sasa waliojiandikisha ni zaidi ya 150, 000. Kwa hiyo kama anategemea kura 9,000 basi afadhali ajitoe...maana amekwisha kushindwa tena vibaya......Lema mwaka 2005 alipata kura 45, 000 na bado alishindwa na Mrema aliyepata 47, 000.................
 
Eti akihojiwa na BBC leo tena amesema atashinda kwa 90% na ushahidi anao kwa sababu eti anakubalika na hata watoto wanamfahamu teh teh!!

Tusimzuie kujifariji jamani wewe unataka anywe sumu, au ungekuwa wewe ungesemaje? Hakuna mwanasiasa anayesema jamani ninaona ninashindwa sasa . Huwa ni wakaidi sana huwa wanategemea kipenga cha mwisho hata kama wanaona wamefungwa magoli 10 bila wanahisi kuna muujiza pale mwisho. ILA KWA BATILDA MCHEZO UMEISHA KABSA HANA KITU
 
Fame ya Batilda Arusha inashuka kwa kasi ya kutisha, na wala asidhani waliompa kura za maoni watampa kura za uchaguzi Mkuu...tofauti ni kama Mbingu na Nchi!!

Jana nilikuwa kwenye eneo linalomilikiwa na ccm, nilishuhudia wanaccm kibao wakimponda na kusema kuwa hawawezi kupoteza kura zao kwa mtu wanayeona wazi kuwa hawezi ubunge!..baadhi yao wakavua tshirt za kijani na kuelekea NMC kuliko na mkutano wa Lema!
 
Back
Top Bottom