Bata ni fursa ila nakwama

card78

Member
Sep 22, 2018
47
47
Ni namna gani naweza kupata ongezeko kubwa la bata, nimekuwa nikishuhudia watoto wa bata wakifa ovyo katika maeneo niliyowahi kukaa na kushindwa kuelewa ni kwa namna gani naweza kuzuia hiyo hali.

Bata akifika umri fulani wa kubadilika rangi inakuwa ni ngumu sana kufa kama anavyokuwa mtoto, naombeni msaada wa kisayansi zaidi juu ya ufugaji wa mnyama huyu
 
Ushauri wangu mimi ni

1. Bata wanapototolewa usiwachie wazurule ili kupunguza risk za vitu kama magnjwa, kunguru, mwewe n wanyama wengine .subiri wakue kidogo uweze kuwaachia.

2. Banapotolewa wapatie antibiotics kwenye maji zile za kuanzishia vifaranga kama tetracolivit au neoxychick zitasaidia kupunguza infection zinazowakumba mara kwa mara.

3. Hakikisha usafi wa mabanda vyombo maji na chakula chao bata wako sensitive sana kwenye sumu kuvu (aflatoxicosis), magonjwa kama aspergilosis, botulisim, avian cholera yoote haya kuyaepuka yanaitaji usafi

4. Zaidi kuepuka magonjwa yatokanayo na vyakula watengenezee starter yako wapatie mpka wakishafika umri wa kuanzia mwezi mpaka miwili unaweza anza kuwapatia mavyakula mengine kama mabaki n.k.

5. Kuna magonjwa kama duck viral hepatitis na duck viral interitis haya yanashambulia sana mashamba na hua kuna chanzo zake lkn tz bado.

Naona wafugaji wa bata wanaenda kununua chanjo kwenye maduka ya mifugo wanapewa newcasttle ngumburo ndui n.k hapo hua mnapigwa bata awana hz case kbsa
 
Mimi nimefuga bata sana na hii wiki ya tatu naendelea kula majogoo tu.

Kinachowaua bata ni mvua, baridi wakiwa wadogo. Wakinge na mvua. Bata wangu hawajapewa dawa hata siku moja na wanatembea tu hovyo nyumbani.

Bata wengine wakubwa ni sumu kwa vifaranga vya wenzao, hakikisha umewatenganisha wakiwa na vifaranga vidogo mpaka vifikishe umri fulani.
 
Ukitaji bata wa Kienyeji ( Muscovy) , mallard, jumbo perkin, khaki Campbell, Indian runner, Rouen, bukin, black Swedish wa umri wa kutaga na vifaranga tunapatikana chanika
Call 0746696878

Kwa swala la mtoa mada hapo juu pia unatikiwa kubalisha madume kila baada ya generation 1 bata waliozaliwa sehem moja hawatikiwi wapandane , mama atakiwi apandwe na mtoto wala mtoto atakiwi apandwe na mtoto

Pia watoto wape antibiotics na vitamin ,chakula chao kiwe starter Pia watunze sehemu kavu .

A7E7EF90-E6D3-44AD-89E2-EED99305158C.jpeg

8EDAC7C2-A871-40A1-BE18-9A2EF022216B.jpeg

3C12C99A-598A-4D73-BF84-D6A04C40F4A3.jpeg

5FA2142F-5391-4082-92DA-C1CD0716E9CB.jpeg

B60C5BCB-307B-4A9D-A4C1-D7E39E5BBA75.jpeg
 
Attachments

  • IMG_7741.MOV
    9.8 MB
Asante
Ukitaji bata wa Kienyeji ( Muscovy) , mallard, jumbo perkin, khaki Campbell, Indian runner, Rouen, bukin, black Swedish wa umri wa kutaga na vifaranga tunapatikana chanika
Call 0746696878

Kwa swala la mtoa mada hapo juu pia unatikiwa kubalisha madume kila baada ya generation 1 bata waliozaliwa sehem moja hawatikiwi wapandane , mama atakiwi apandwe na mtoto wala mtoto atakiwi apandwe na mtoto

Pia watoto wape antibiotics na vitamin ,chakula chao kiwe starter Pia watunze sehemu kavu .
View attachment 2018329
View attachment 2018329

View attachment 2018330

View attachment 2018337

View attachment 2018338

View attachment 2018339
Asante kwa uzi
 
Fata ushauri uliopewa na wadau..!bata ni ndege asiepata maradhi hovyo..!hivyo ni rahisi kuwafuga..!hakikisha vifaranga hawaloi kwa namna yeyote ile eidha kwa kunyeshewa au kugusa maji..!pili wape watoto wa bata matunzo kama unavyolea vifaranga vya kuku..!ongezeko la bata ni kwa kuhakikisha unalea vifaranga pasipo kufa..!pia hakikisha unawajengea kibwawa kwa ajili ya kuogelea hii inawasaidia bata wanaolalia kupeleka unyevu kwenye mayai na kuangua mayai yote..!usiruhusu bata wadogo kuogelea mpaka watakapofikisha miezi 3
 
Ushauri wangu mimi ni

1. Bata wanapototolewa usiwachie wazurule ili kupunguza risk za vitu kama magnjwa, kunguru, mwewe n wanyama wengine .subiri wakue kidogo uweze kuwaachia.

2. Banapotolewa wapatie antibiotics kwenye maji zile za kuanzishia vifaranga kama tetracolivit au neoxychick zitasaidia kupunguza infection zinazowakumba mara kwa mara.

3. Hakikisha usafi wa mabanda vyombo maji na chakula chao bata wako sensitive sana kwenye sumu kuvu (aflatoxicosis), magonjwa kama aspergilosis, botulisim, avian cholera yoote haya kuyaepuka yanaitaji usafi

4. Zaidi kuepuka magonjwa yatokanayo na vyakula watengenezee starter yako wapatie mpka wakishafika umri wa kuanzia mwezi mpaka miwili unaweza anza kuwapatia mavyakula mengine kama mabaki n.k.

5. Kuna magonjwa kama duck viral hepatitis na duck viral interitis haya yanashambulia sana mashamba na hua kuna chanzo zake lkn tz bado.

Naona wafugaji wa bata wanaenda kununua chanjo kwenye maduka ya mifugo wanapewa newcasttle ngumburo ndui n.k hapo hua mnapigwa bata awana hz case kbsa
Heshima yako Mkuu, hongera kwa mchango mzuri ambao umeutoa hapa, umeelezea vizuri Sana na naamini kwa mfugaji ambae atafata ushauri wako bila shaka ataona mafanikio ndani ya muda mfupi

ila ninapenda kuchangia katika hoja ya bata kutopata magonjwa ya Newcastle,Gumboro na Ndui, kuna sehemu nitaungana na wewe ila kuna sehemu nitapingana na wewe

Nianze kwa kuungana na wewe kuwa bata hawapati Gumboro, na ata wakipata inakuwa ni Gumboro serotype 2 ambayo sio pathogenic kwa bata hivo haitawadhuru

Tukirudi kwenye NDV na NDUI hapo nakupinga Mkuu, Bata pia wanaugua Newcastle pamoja na Ndui, ispokuwa utofauti unakuja kwenye strain ipi ambayo wameathirika nayo ili waoneshe dalili, kwa strain 1 na 2 ya Newcastle inaathiri Sana kuku kuliko bata, kwenye hizo strains bata wanakuaga na Natural immunity

hivo sikatai kwamba Bata wana sifa kubwa ya kuwa resistant dhidi ya Newcastle ila haina maana kwamba hawaugui au hawafi kutokana na Newcastle issue jnakuja ni Newcastle ipi? na kumbuka strains za hawa virus zinaendelea kuongezeka na Ndv 4 inaathiri Bata vizuri na hasa bata ambao ni vifaranga, na ubaya unakuja pale ambapo mfugaji anachanganya Bata na Kuku, maana Kama pandemic ya Newcastle itatokea it means Bata watakuwa carrier na Kuku ndio watakuwa wahanga wakubwa kutokana na uwezo wao mdogo wa kupambana na Newcastle ilihali bata wao wako vizuri, so bata atakuwa anafanya kazi ya kuambukiza tu Kuku

Kuhusu case ya Ndui kwa bata ata haiitaji kuifungulia mjadala kama ushafuga Bata au unakaa na jamii inayofuga bata, siku hizi imekuwa kawaida Ndui kwa bata, hiyo case inatokea Mara kwa Mara na wafugaji wanadeal nayo either pasipo kujua kuwa ni Ndui na wengine wanajua fika kuwa ni Ndui ila utofauti wake na Kuku ni kwenye Mortality na Morbidity

Ni sawa na case ya Corona tu, kuna strain ingine inaathiri sana America na ingine inaathiri sana Asia au Europe ila unakuta hizo zote athari zake zinakuwa ni ndogo endapo ataugua Mwafrika, so huwezi kusema mwafrika haugui Corona maana nawao wanakufa japokuwa kwa idadi ndogo compared na Europe na kwingine, hadi hapo natumai utakuwa umenielewa mkuu, na karibu kwa Hoja
 
Uzi mziri ila sijaona anayesungumzia soko la Bata ,
Kuna lipindi niliwafuga zaida ya 100 ila nikakosa soko lake nikaishia kuwala na kuwagawa kwa ndugu jamaa na marafiki ...

Wekeni soko la Bata nirudi kuwaguga
 
Back
Top Bottom