Bastola ya Aden Rage na CCM

sheria iseme isiseme kuonyesha silaha hadharani tena kwenye mkutano wa kampeni ni UGAIDI, na huyu amekuwa akisaidia al shabab moja kwa moja toka Tanzania.Ni mwenyekiti wangu Simba ila nina wasiwasi sana na nyendo zake. Afuatiliwe huyu si mwema kwa Taifa. Anajificha nyuma ya michezo na siasa kutimiza azma zake.

Nafikiri sheria imekupiga chenga.

Sasa na wale polisi wanaotembea na silaha khadharani kwenye mabenk na mitaani ni magaidi?

Kifupi kinachokatazwa na Sheria ni kumtishia mtu silaha au kumlenga (kumuonyeshea kuelekea ulipo mwili wake) ni kosa. lakini kuihifadhi kiunoni na watu wakaioana hakuna kosa llolote.
 
Sheria zinasema watu wote ni sawa,
ila (unwritten) kuna walioko sawa zaidi kuliko wengine!!

Mkuu kama kwenye kitabu cha animal farm." All animals are equal but some are more equal than others"
 
Kwenye gazeti la Mwananchi la Leo Ijumaa tarehe 23 September 2011 limeweka Picha ya rage akiwa na "kipaja cha Jogoo" kwenye kampeni za Igunga, nimepata shida kuelewa dhamira yake ni ipi hasa; je anathibitisha madai ya Bosi wake Mukama kuwa Usalama wa Taifa wamelala usingizi au ni kuthibitisha madai ya wanyonge kuwa Usalama taifa ni kwa ajili ya CCM? Je na mimi nitafute hata sanamu tu ya Bastola nipite nayo mtaani kwa stayle kama ile? je kuna wachache wako juu ya sheria? Nimeuliza tu jamani..
View attachment 37704

Rage ni mbunge lakini ni raia. Raia wanapewa vibali vya kumiliki silaha lakini hata wakiwa nazo mwilini hawaruhusiwi kuzionyesha hadharani, kinyume na askari polisi, wanajeshi na watu wengine wenye majukumu ya ulinzi. Sasa huyu Rage labda anafikiri tuko Somalia au kwenye nchi nyingine ambako ma cowboy wanatembea tu na silaha waziwazi. Akiwa mbunge na mtunga sheria, anatakiwa kuwa wa kwanza kuheshimu sheria za nchi hii. Kama hili ni gumu basi. We have one cowboy in the form of CCM, we don't need other cowboys brandishing arms in public!
 
hawa jamaa huwa ni culture yao kuembea na 'kasiraha' kadogo kama bakora, lakini naona hapa anaonyesha picha halisi ya 'pembe ya Africa'!
Rage mgeni wa mambo hayo.kakipata juzi tu.analingishia watu na kuwapiga mkwara watu.
 
Ugeni una tabu kweli. Nimekumbuka ile ya mmasai na chupi mpya.
 
I have see the photo it speaks volumes...this is no accident....he is tryna send a message...
 
Once a convict..........always a convict no matter what

rage270308.JPG
 
hivi mna uhakika gani kama ni bastola ile?,..pengine simu...mimi nilidhani alibust shot moja hewani sababu hiyo ndio proof
 
Kwa hio Rage nae ni askari? naona kama vile umechanganya mada Mpwa, kama aliebeba silaha ni askari tusingehoji japo tungehoji tu kutokana labda/pengine na mazingira aliyomo ila sio kama Rage jamani tuwe wawazi Mpwa
Nafikiri sheria imekupiga chenga.

Sasa na wale polisi wanaotembea na silaha khadharani kwenye mabenk na mitaani ni magaidi?

Kifupi kinachokatazwa na Sheria ni kumtishia mtu silaha au kumlenga (kumuonyeshea kuelekea ulipo mwili wake) ni kosa. lakini kuihifadhi kiunoni na watu wakaioana hakuna kosa llolote.
 
tena 'kwao' hivi vibastora wanatembea navyo watoto tu na nadhani ukiingia zaidi ndani kwake huwezi kosa AK47 na SMG kadhaa, usijekuta Al-Shaabab wana active wing ndani ya TZ
Mkumbuke huyu si mtanzania ni msomali lolote aweza fanya
 
Jamani anafuta nyayo.! Kama mnafuatilia vizuri mkutano unaoendele U.S. Hivi ni kiongozi gani anayegandamana na walinzi hadi kwa choo kama sio Jk.?
 
Anahc watamfuata km DC!huyo msomali anapenda sana kuongoza kwa mkono wa chuma,i had worked with hm somewhere.
 
nimeshtushwa na picha iliyopo kwenye ukurasa wa mbele wa moja ya magazeti ya leo. Mbunge wa tabora mjini ismail aden rage anapanda jukwaani na libastola kiunoni. Mungu amejibu swali gumu ni nani anaeleta vurugu kwenye kampeni za igunga? Bastola ya nini kwenye mikutano wakati kuna wanausalama weengi hivyo? Ccm ni hatari jamani ni kifo..

ushahidi umekamilika, nani waleta fujo hapa nchini.
Ni kweli kwa hadhi yake anaweza kuomba na kukubaliwa kumiliki silaha, lakini siyo kutembea nayo kila kona na kuionesha hadharani, kufanya hivyo ni kuwatishia wananchi
 

Huyu Rage, si ndiye Yule jambazi aliyeiba milioni 3 na vifaa mbalimbali vya TFF mwaka 1999, na hatimae 2005 akatiwa ndani kabla ya kutolewa na msamaha wa Rais Mkapa!!.. jambazi huwa hajiamini.. mara zote huwa chonjo lolote laweza kumkuta.. au hao ndio makomandoo Mzee Mukama (aka ongeakinyume) aliosema wameingizwa Igunga?.. maana jamaa anasema cdm imeingiza makomandoo kumbe ni ccm.. jamani hebu nifunulieni sheria za kumiliki silaha na ubebaji wake kwa raia zikoje!! kama vipi nasi tuzibebe kama cm za mkononi..
 
Back
Top Bottom