Basilio Matei Mbuzi Wa Sadaka?

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Jambo wakuu.
Jana nilibahatika kupitia ofisi fulani, nikakutana na maafande wa polisi, RPC wa Arusha Basilio Matei. Katika maongezi akamtambulisha afande Thomas Andengenye( RPC MORO), akasema ndiye anayechukua nafasi yake, ambapo yeye Basilio anahamishiwa makao makuu dar! Lakini leo katika maongezi na watu nimeambiwa Afande Matei ameondolewa Ars kutokana na kuruhusu ushindi wa mbunge mpinzani Arusha mjini, wakati alikuwa na uwezo wa kutumia nguvu za dola kupindua. Hii mnaichukuliaje wakuu? Inawezekana?
 
Bangusilo Matei.

Kwa habari za uhakika zinasema alipewa amri na mkuu wake aue walau watu 5 wakati wanachi walipokuwa wamekusanyika njee ya jengo la halmashauri ni jiji. Akakubali amri lakini hakuitekeleza kwa kusema yeye ni mcha mungu na Arusha itaendelea kuwepo hata baada ya uchaguzi.

Alichokifanya mkuu huyu ni kumshinikiza mkuu wa Tume (mkurugenzi wa uchaguzi Jimbo laArusha)kutangaza matokeo kabla ya saa 12 jioni la sivyo ataondoa vijana wake kwenye eneo hilo kwa watu ni wengi na hawana uwezo wa kulinda usalama kwa jiji la Arusha itakapotimu usiku.

Nasikia kwa kosa la kukataa AMRI (isiyo halali) kapelekwa benchi makau makuu kwa kosa la utovu wa nidhamu
 
Yeye akaawaambia vijana wake hamwagiwi mtu hata maji ya kuwasha pasipo na sababu ya kweli kufanya hivyo
 
Yeye akaawaambia vijana wake hamwagiwi mtu hata maji ya kuwasha pasipo na sababu ya kweli kufanya hivyo
wakuu ni kweli haya lakini!???
wengine tunaweza kujitoa mhanga jamani semeni ni utani tuu!
 
Kama aliweza ku-absorb pressure kama ile ya "kutanganza" matokeo ya uchaguzi AR Mjini nadiriki kusema "He is truly a great MAN" - Historia itamkumbuka
 
Akistaafu atunge kitabu akiite upolisi wangu na uchaguzi mkuu...atauza sana!!
 
Itamlipa baadaye nchi itakapochukuliwa na mtu mwenye hofu ya Mungu. Nakumbuka Mahita yeye alituzwa kwa kuwagaragaza washimboni kule Moshi 1995, huyu yeye atatuzwa kwa kuepusha mauaji
 
Ni kweli Matei aliwaambia tume ya uchaguzi itakapofika saa 12 jioni atawaondoa vijana wake! Kwa mtizamo wangu siku ile wananchi wakiwa na jazba ya kupata matokeo mimi mwenyewe nilikuwepo pale kweli baba huyu alitumia kitendo cha busara sana na Mungu amzidishie nguvu tunahitaji watu wenye ujasiri kama huo alioutoa kwa tume ya uchaguzi kutangaza matokeo, bila kufanya vile kwa kweli wananchi kwa jazba waliyokua nayo halafu giza likaingia bila matokeo kutolewa hakika mkoa wa Arusha pangegeuka KOSOVO kwakua kulikua na aina za watu mbalimbali wakiwa na jazba na hasira na wengine niliwasikia chinichini wakisema hatutoki hapa mpaka kieleweke na ukizingatia taasisi binafsi na zile za serikali ziko jirani kabisa na eneo la tukio, Namuunga mkono sana huyu baba kokote atakapopangiwa Mungu aendelee kumpa moyo wa ujasiri. Naunga hoja:whoo:
 
ni kweli matei aliwaambia tume ya uchaguzi itakapofika saa 12 jioni atawaondoa vijana wake! Kwa mtizamo wangu siku ile wananchi wakiwa na jazba ya kupata matokeo mimi mwenyewe nilikuwepo pale kweli baba huyu alitumia kitendo cha busara sana na mungu amzidishie nguvu tunahitaji watu wenye ujasiri kama huo alioutoa kwa tume ya uchaguzi kutangaza matokeo, bila kufanya vile kwa kweli wananchi kwa jazba waliyokua nayo halafu giza likaingia bila matokeo kutolewa hakika mkoa wa arusha pangegeuka kosovo kwakua kulikua na aina za watu mbalimbali wakiwa na jazba na hasira na wengine niliwasikia chinichini wakisema hatutoki hapa mpaka kieleweke na ukizingatia taasisi binafsi na zile za serikali ziko jirani kabisa na eneo la tukio, namuunga mkono sana huyu baba kokote atakapopangiwa mungu aendelee kumpa moyo wa ujasiri. Naunga hoja:whoo:
kama ni kweli haya abalikiwe natamani wangekuwepo hata 10hv nchini hapa!
 
history itabaki , inawezekana akawa ni miongoni mwa maafande wachache wenye busara ya maamuzi
 
Mkuu huyu mkubwa alipata shinikizo kubwa sana hata kabla ya uchaguzi
lakini aliapa kufanya kazi proffessionally na alikua tayari kutimiza tu yale
maadili yake ya kazi yanamhitaji kufanya.

Aliongea kitu kimoja ndicho kilichowakera: Kwa nini Mramba yupo mahakami? Kwa nini Zombe alifikishwa mahakami?
na akawapa jibu: Kutumia vibaya madaraka waliopewa na hivyo yeye atatumia madaraka yake kama utaraibu unavyomwelekeza.

hayo ndio yaliyojiri
 
Mungu sio binadamu. Haki aliyoapa kuilinda itamtangulia mbele yake siku zote. Nchi kama hizi tunazoishi, wanasiasa wanapemda kuchukulia mambo mengi to their advantage. Ingawa sijui kama sababu ya kuhamishwa ndio itakuwa hiyo, but who knows!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom