Basil Mramba amtaja Mkapa mahakamani; Asema ndiye anayejua Kampuni ya Alex Stewart ilivyosaini mkata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Basil Mramba amtaja Mkapa mahakamani; Asema ndiye anayejua Kampuni ya Alex Stewart ilivyosaini mkata

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Aug 24, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ALHAMISI, AGOSTI 23, 2012 04:30 NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

  *Asema ndiye anayejua Kampuni ya Alex Stewart ilivyosaini mkataba
  *Ajitoa, asema hajui chochote kuhusu kampuni hiyo ilivyosaini mkataba
  *Andrew Chenge, John Cheyo kutinga mahakamani kutoa ushahidi

  ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba, amedai kwamba, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ndiye aliyeagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itafute kampuni ya ukaguzi nje ya nchi na alimruhusu aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Balali, kusaini mkataba na Kampuni ya Alex Stewart.

  Mramba alidai hayo jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, alipokuwa akitoa utetezi mbele ya Jopo la Mahakimu, John Mtemwa, Saul Kinemela na Sam Rumanyika, huku akiongozwa na wakili wake, Hurbert Nyange.

  Mshitakiwa huyo wa kwanza katika kesi ya kutumia madaraka vibaya na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart, kabla ya kuanza kujitetea alitaja majina ya mashahidi watakaofika mahakamani kwa ajili ya kumtetea.

  "Waheshimiwa nitakuwa na mashahidi sita na wengine watatu watawasilisha nyaraka, mashahidi hao ni aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati huo, ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), aliyekuwa Gavana wa BoT au yeyote atakayeteuliwa naye, Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) na Mshauri wa Masuala ya Kodi, Florian Msigara," alidai Mramba.

  Akizungumza wakati wa utetezi wake, Mramba alidai chimbuko la kesi yake kulikuwa na malalamiko kutoka bungeni na kwa wananchi, kwamba Tanzania kuna migodi ya dhahabu lakini Watanzania hawanufaiki na migodi hiyo na Serikali ilikuwa inaibiwa.

  Mramba alidai kwamba, alishitakiwa kwa sababu alitoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart, ambayo Serikali iliikaribisha nchini kufanya kazi ya kukagua migodi ili kupata maelezo ya kutoa kwa wananchi.

  "Serikali iliiteua BoT kufanya mchakato wa kuileta kampuni hiyo na baada ya kufuata taratibu na kuipata Kampuni ya Alex Stewart, waliingia mkataba nayo.

  "Wakati huo nilikuwa waziri, Rais Benjamin Mkapa ndiye aliyeagiza BoT kuitafuta kampuni hiyo, Rais Mkapa pia aliniagiza kuhakikisha gharama za kuilipa kampuni zinapatikana kutoka serikalini, BoT au kotekote," alidai.

  Mshitakiwa huyo alidai katika ushahidi wake, kwamba hakuhusika katika mchakato wa kutafuta kampuni wala kuiingiza nchini zaidi ya kazi aliyopewa na Rais Mkapa ya kuhakikisha gharama za kuilipa zinapatikana baada ya kufika.

  Akielezea utaratibu uliotumika kuipata kampuni hiyo, alidai BoT walitangaza katika mtandao, kampuni zikajitokeza wakazishindanisha na kubakisha mbili.

  Wakati wa mchakato huo, alidai wakati wa kuzijadili kampuni hizo mbili pamoja na gharama za kumlipa mshauri ambaye ni Kampuni ya Alex Stewart, Wizara ya Fedha ilituma mwakilishi ambaye aliombwa na wana kamati kushughulikia msamaha wa kodi.

  "Juni 14, 2003, mkataba kati ya BoT na Kampuni ya Alex Stewart ulisainiwa, waliosaini ni Daudi Balali na mwakilishi kutoka Alex Stewart kwa maagizo ya Mkapa," alidai.

  Mramba alidai kwamba, hakumruhusu Gavana kusaini mkataba huo, kwani aliwahi kufika kwake kwa ajili ya ushauri ili mkataba huo usainiwe, lakini alimkatalia na kumpa sababu. Kesi hii itaendelea tena leo ambapo Mramba ataendelea kujitetea.

  Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

  Washitakiwa hao walipotakiwa kuwataja mashahidi wao, walisema watatetewa na mashahidi waliotajwa na Mramba.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Misamaha ya kodi kwa MIGODI toka kwa MKAPA yanamrudia MKAPA kwa KASI YA HATARI; Itabidi wamuondolee Immunity then

  Abdallah Kigoda na Team yake ya Kuuza Government Industries Itawagonga na kuwashika WIZI WAO
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,943
  Trophy Points: 280
  Kumshtaki Mramba na kumwacha bosi wake aliyempa maagizo ndo usanii wenyewe huu.

  Linchi letu bana utadhani halina mwenyewe.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mkapa atasimama kizimbani kama shahidi na 'kuwashangaa' waliomkamata Mramba wa watu, manake kila kitu kilikuwa kwenye mpango; kama alivyofanya kwa Mahalu! Mkapa officially ni shahidi wa mafisadi.

  Balali atajuta kufa mbona! Kila issue ya kwake sasa!
   
 5. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  [Abdallah Kigoda na Team yake ya Kuuza Government Industries Itawagonga na kuwashika WIZI WAO ]huyundiye alishiriki kwa kiasi kikubwa kuuza viwanda vya serikali ambavyo sasa hivi havifanyi kazi.Alipoteuliwa waziri wa viwanda kauli yake ya kwanza ni kuzungumzia ufufuaji wa viwanda vya serikali vilivyokufa.Niliwashangaa hata waandishi walioripoti hiyo habari kwanini hawakumwambia wewe uliyeshiriki kuviua utawezaje kuvifufua
   
 6. morphine

  morphine JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 2,566
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  booongo eeehh...
  bongo dar-es-salaaaaamm....
  utalia lia lia liaaaaaaa.....
  ndani ya dar-es-salaaamm...
  kaa chonjo eeeeehh......
  ndani ya dar-es-salaaamm...
  :music:


  naosha kinywa tu wakuu :israel:
   
Loading...