Basi laacha njia na kugonga magari saba Moshi, watu 15 wajeruhiwa

Watu 15 wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi nchini Tanzania kwa ajili ya kupata matibabu, baada ya basi la kampuni ya Harambee kudaiwa kufeli Breki na kuparamia magari mengine saba katikati ya mji wa Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo jioni Jumanne Desemba 17, 2019 na kueleza imehusisha magari saba likiwamo basi la hilo la Harambee.

"Ni kweli kuna ajali imetokea jioni hii eneo la Benki ya NBC, iliyopo katikati ya mji wa Moshi na kwa sasa nipo Mawenzi hospitali, ambapo majeruhi wapo 15 na mmoja ndiye aliyeumia sana lakini wengine wamepara majeraha madogo ya kawaida na mishtuko na wanaendelea kupewa huduma ya kwanza," amesema Kamanda.

Kamanda Hamduni amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea na atatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.

"Ni mapema sana kuelezea chanzo cha ajali, kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea, lakini pia sijapata taarifa ya idadi ya abiria waliokuwepo kwenye basi na magari mengine madogo yaliyohusika katika ajali hiyo" amesema.

Tukio hilo la kuogofya lilinaswa na camera za CCTV, zikionyesha namna basi hilo lilivyoshindwa kuzunguka katika mzunguko huo wa magari na kuparamia magari saba kabla ya kusimama.

View attachment 1295572
Very bad, IST ya blue imesukumwa na kugeuka ilikotoka
 
Hatari sana

Kuna abiria kwenye hiyo IST navy blue iliyogongwa , baada tu ya kushuka kaanza kukimbia, inawezekana kachanganyikiwa hivi baada ya kunusurika kifo
Nilikuwa narudisha hio clip hapo nihakikishe tu kama ni yeye abiria ama kulikuwa na mtu mwengine. Mana alivoondoka ni kama vile hataki ushahidi na kumuacha dereva wake mule mule
 
Hatari sana

Kuna abiria kwenye hiyo IST navy blue iliyogongwa , baada tu ya kushuka kaanza kukimbia, inawezekana kachanganyikiwa hivi baada ya kunusurika kifo
Hata ingekuwa ni wewe kama ulikuwa na chupi tu umetoka gesti na mchepuko ungekimbia bila kujali
80464460_2200910173547664_32770544633905152_o.jpeg
 
Kwa maana hiyo mkuu ikitokea ku fail kwa break ni no way inabidi uchague mti wa kusimamia?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuchukua hatua haraka ni jambo la msingi sana inapotokea break zimefeli. Kuchagua soft landing area kwenye hatua za awali hupunguza madhara. Pia kulijua gari unaloendesha husaidia kujua ni wakati gani na aina gani ya emergence procedure ya kufuata
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
Ni nini kinachosababisha break ku fail?

Ni uzembe wa mmiliki wa gari na dereva.

Kwanini hawapeleki magari service regularly Kama inavyotakiwa?

Kwanini hawakubadilisha break pads?

Ni uzembe na uzembe lazima wawajibishwe wote dereva na mmiliki wa gari!

Waache kucheza na maisha ya watu!

Na iwe mfano kwa wengine wajifunze

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unausafiri yani gari usiseme ivyo... Izo ni technical issues brother unatakiwa kujua gari inatumia umeme kwenye mfumo wa break kwaiyo inaweza kutokea tatizo hata kama gari ina service mkuu... Kikubwa ni dereva yupo vizuri kupambana.... Subiri uwe na gari afu ifeli break utakuja apa kutuadisia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu ni mkuu sana...just imagine hao jamaa wa bajaji hapo round about yaani ni kama walisubirishwa...basi likaenda kuparamia magari...

Kama Mkuu wa Nchi, Jeshi la polisi na uongozi wa Manispaa na Halimashauri zote wana ya kujifunza basi hapa nadhani kuna somo zuri, ile kauli ya waacheni wapange biashara zao pembezoni mwa barabara msiwasumbue....💪👀👂
 
Watu 15 wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi nchini Tanzania kwa ajili ya kupata matibabu, baada ya basi la kampuni ya Harambee kudaiwa kufeli Breki na kuparamia magari mengine saba katikati ya mji wa Moshi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Salum Hamduni, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo jioni Jumanne Desemba 17, 2019 na kueleza imehusisha magari saba likiwamo basi la hilo la Harambee.

"Ni kweli kuna ajali imetokea jioni hii eneo la Benki ya NBC, iliyopo katikati ya mji wa Moshi na kwa sasa nipo Mawenzi hospitali, ambapo majeruhi wapo 15 na mmoja ndiye aliyeumia sana lakini wengine wamepara majeraha madogo ya kawaida na mishtuko na wanaendelea kupewa huduma ya kwanza," amesema Kamanda.

Kamanda Hamduni amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika na kwamba uchunguzi unaendelea na atatoa taarifa rasmi pindi utakapokamilika.

"Ni mapema sana kuelezea chanzo cha ajali, kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea, lakini pia sijapata taarifa ya idadi ya abiria waliokuwepo kwenye basi na magari mengine madogo yaliyohusika katika ajali hiyo" amesema.

Tukio hilo la kuogofya lilinaswa na camera za CCTV, zikionyesha namna basi hilo lilivyoshindwa kuzunguka katika mzunguko huo wa magari na kuparamia magari saba kabla ya kusimama.

View attachment 1295572

Halafu hilo eneo kuna bank kadhaa imagine lingechichoa kwenye moja ya hizo banks
 
Back
Top Bottom