Basi la Taqwa toka Zimbabwe lapata ajali mbaya sana Mikumi

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kuna ajali mbaya sana hapa kona ya Mikumi ikilihusisha basi la Taqwa.

Basi lililosaidia kubeba Majeruhi kupelekwa Mikumi hospital ni Princess Muro.

Basi lilikuwa ikijaribu ku overtake Lorry.

Ukiangalia vizuri utaona Mbao zimeingia kwenye basi hapo mbele.

Bado majeruhi wengi wanahitaji msaada bado wanatolewa taratibu.

Hadi sasa wamekufa watatu - 2 women 1 man.

Abiria aliyekuwepo anasema dereva aliyepatisha ajali si dereva. Madereva wawili walikuwa pembeni aliekuwa anaendesha ni msimamizi wao (Yaani Boss).
 
Attachments

  • 1388581742264.jpg
    1388581742264.jpg
    57.4 KB · Views: 4,658
  • 1388581761327.jpg
    1388581761327.jpg
    69.8 KB · Views: 6,346
Poleni sana wafiwa na poleni sana majeruhi mungu mwenyezi awape nuru mpate kupona haraka na azihifadhi nafsi zilizotangulia kwa amani..ameen.
 
Poleni wandugu...Poleni insikitisha kupoteza maisha...inahuzunisha kupatwa na mejruhi.
Waloomia wapone haraka, na walotangulia Mwenyeezi mungu awakirimu pema.AMIN
 
Bora hilo Tagwa nalo lifungiwe kama wenzao wa Buruhani ya korogwe
 
Poleni sn wafiwa na mungu awasaidie majeruhi ,jamani mwaka unaanza na ajali tena? Ni bora hilo basi lifungiwe na hao madereva wachukuliwe hatua kali na si faini,ili iwe fundisho haiwezekani wacheze na roho za watu namna hiyo
 
Poleni wafiwa na.majeruhi!!!!!!

Hawa watu wa mabasi wameyazoea sana kiasi kama wewe ni dereva ukikaa siti ya mbele unaweza pigana bure,makonda,tingo na wengine wakishamaliza kazi ya ukaguzi hurundikana kwa dereva kupiga stori,sasa simu kuongea,sms, mirungi wengine na mastori yaani hatari tupu!!!!
 
Kuna ajali mbaya sana hapa kona ya Mikumi ikilihusisha basi la Taqwa.

Basi lililosaidia kubeba Majeruhi kupelekwa Mikumi hospital ni Princess Muro.

Basi lilikuwa ikijaribu ku overtake Lorry.

Ukiangalia vizuri utaona Mbao zimeingia kwenye basi hapo mbele.

Bado majeruhi wengi wanahitaji msaada bado wanatolewa taratibu.

Hadi sasa wamekufa watatu - 2 women 1 man.

Abiria aliyekuwepo anasema dereva aliyepatisha ajali si dereva. Madereva wawili walikuwa pembeni aliekuwa anaendesha ni msimamizi wao (Yaani Boss).

Asante kwa taarifa mkuu, dah inasikitisha sana!
 
Back
Top Bottom