Basi la Raha Leo lilivyosheheni abiria mpaka mlangoni!!

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,303
Hili ni basi la abiria la Raha Leo lenye namba za usajili T431 ARM linalofanya safari zake kati ya Dar Es Salaalam na Tanga likiwa limesheheni abiria mpaka mlangoni leo wakati likielekea Dar Es Salaam. Hizi picha zimechukuliwa leo leo. Picha kwa hisani ya Michuzi Blog (MICHUZI: Basi la Abiria liendalo mikoani linapojaza abiria mpaka mlangoni). Hili basi likipata ajali (Mungu epusha mbali) tutaambiwa lilikuwa na abiria 65 tuu.

IMG-20110913-00232.jpg

IMG-20110913-00231.jpg
 
Na barabara nzima toka Tanga mpaka Dar wamejaa askari wa Usalama barabarani jee wanafanya nini huko barabarani na hali kama hii tunaiona?
 
Na barabara nzima toka Tanga mpaka Dar wamejaa askari wa Usalama barabarani jee wanafanya nini huko barabarani na hali kama hii tunaiona?

Yep. Zaidi abiria waliokuwepo ndani ya basi waliona ni sawa tuu.
 
Na barabara nzima toka Tanga mpaka Dar wamejaa askari wa Usalama barabarani jee wanafanya nini huko barabarani na hali kama hii tunaiona?

Wanakusanya mia mia, ili wapate cha kugawana jioni.
 
Mitanzania hiyo, haijali maisha yao, inachagua crap for their leaders, inapanda malori na magari yaliyojaa, meli zilizozidisha cargo, halafu tunategemea kuomboleza kutakwisha?
 
Mitanzania hiyo, haijali maisha yao, inachagua crap for their leaders, inapanda malori na magari yaliyojaa, meli zilizozidisha cargo, halafu tunategemea kuomboleza kutakwisha?
Tutapeperusha bendara nusu mringo kwa sana tu
 
Ile sheria ya level seats bado ipo au walishaifanyia amendments? Huwa nashangaa hata najishangaa mwenyewe, tunapenda shida au tumezoea shida kiasi kwamba hata haki zetu tunaamua kuachana nazo na kuona hazina maana? Kama huna haraka, yanini kujibana sana kwenye mabasi kama ndizi?
 
lakini uchumi nayo unachangia mtu unakuta kapunguziwa 2000 kutoka kwenye nauri halisi akaona bora apande hivyo hivyo...
 
Mitanzania hiyo, haijali maisha yao, inachagua crap for their leaders, inapanda malori na magari yaliyojaa, meli zilizozidisha cargo, halafu tunategemea kuomboleza kutakwisha?

Ndio maana nchi hii mimi sishituki ajali zikitokea kwani matendo yetu kwenye vyombo vya usafiri kutokutarajia ajali ni uwendawazimu mtupu. Infact mimi ajali zetu zilizo nyingi nahisi ni makosa kuziita accidents kwani accident maana yake haizuiliki lakini hizi zetu aslimia kubwa zinazuilika ila serikali inasubiri watu wafe ndio watuambie wamejipanga kuzika na kuhudumia majeruhi walikuwa wapi kuzuia hizo ajali in the first place? Mungu atusaidie ila we are not serious hata kidogo na maisha yetu.
 
hivi watanzania tuna matatizo gani, gari imejaa lakini bado tunapanda mpaka kwapani kwa dereva hii ni hatari sana hii.

Afande Mpinga amka
 
Mitanzania hiyo, haijali maisha yao, inachagua crap for their leaders, inapanda malori na magari yaliyojaa, meli zilizozidisha cargo, halafu tunategemea kuomboleza kutakwisha?
<br />
<br />
Halafu wakipata ajali wakafa safari hii watailaumu......nadhani Airtel kwa kutoomboleza.
 
...........nikijaribu kuwaza kuna chek points ngapi mpk imalize safari,nashindwa kushangaa kabisa!!moyoni nasikitika sana ajali zinapotokea nakuua ila pia nafarijika kuona sisi wenyewe ndio tunajitakia....hii ilibidi iwe sawa na mtu akitaka kujiua,akipona anashtakiwa na akifa anakuw amepona mashitaka!!
 
mabasi haya ya tanga si ndio maji moto aliyasema mengine yanatoka kuzimu kujaza mapipa ya damu duniani, kazi kweli!
 
mi huwa nawasemelezea wa hivi kwa askari gari ikisimama kukaguliwa. afu dereva ananunaaa hadi tunafika. ajabu ni kuwa kuna abiria wengnie wapuuzi wanalalamika unamuudhi dereva kapunguza mwendo tutachelewa kufika. i tell them mi sina safri za zima moto,leo ndo siku ya kuwa barabarani,driver kwa raha zako hata 50kms/hr sawa tu!
Haohao abiria ndiyo wa kwanza kulalamika pindi ajali ikitokea
 
Ile sheria ya level seats bado ipo au walishaifanyia amendments? Huwa nashangaa hata najishangaa mwenyewe, tunapenda shida au tumezoea shida kiasi kwamba hata haki zetu tunaamua kuachana nazo na kuona hazina maana? Kama huna haraka, yanini kujibana sana kwenye mabasi kama ndizi?
Tanzania unauliza sheria?
 
Cha ajabu wakienda kupewa ruti SUMATRA wanahesabiwa kwa leverseat, alafu ndio wa kwanza kulalamika wanapata hasara.
 
Hiii jamani tunako elekea wapi,meli iliyo zama ni kwasababu ya kujaza abiria na mzg,sasa huyu dereva alikwa akisikiliza matangazo ya ajali kupitia masaburi yake nini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom