Basi la Princes Muro latekwa, abiria wavuliwa nguo, waporwa

My take - ma bus yafanye service kabla ya kuanza safari ........basi bovu ...... halafu wanachukua mahela yetu
hao majambazi aka vibaka ........... ndio bomu linaanza kulipuka la vijana wasio na ajira wala maadili chini ya
raisi wao ... dhaifu ..........

Jamani - naomba procedure ya kununua silaha ......... manake ukisafiri mara majambazi .......... mitaani mara polisi wanaua
ahhhhhhhhhhhhhhhhhhhh :confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2::confused2:
 
Poleni waathirika wote, ila naanza kuamini mabasi ya Princess Muro ni mabovu, hasa ya njia hiyo.
Mwishoni mwa June nilisafiri na hilo basi, kufika Dom, mbele kidogo yastendi kuu yaani tunaanza kuuacha mji gari ikabuma.
Tulikaa hapo kwenye gereji yao kwa muda kama saa 2 hivi ndio tukaondoka.
 
Mfumo wa ulinzi wa wa-TZ kwasasa hautuhakikishii usalama wetu. Nani hutawala usiku mpaka majambazi wanateka mabasi hadi serikali itoe maelekezo ya kutokusafiri usiku?? Huo ni mwanzo wa kushindwa kutawala. Kitakachofuata niwatu kujimegea eneo lao na watawala wabakie mijini! watu tunahitaji uhakika wa usalama wetu kwa masaa 24 ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa TZ vinginevyo waachieni hao majambazi wapandishe bendera yao usiku na serikari iseme usiku tunalala usalama wenu utategemea huruma ya wanaotawala usiku!
Na Abdallah Amiri, Igunga

BASI la Kampuni ya Princes Muro, lenye namba za usajili T 551 BQP, ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Kahama, mkoani Shinyanga, limetekwa na majambazi usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Igogo, Wilaya Igunga, mkoani Tabora.
[/COLOR]
Akizungumza na gazeti hili, abiria wa badi hilo ambaye alijeruhiwa na majambazi hao kichwani, Bw. Brayandi Sangatwa (67), alisema wakiwa njiani kabla ya kufika Kijiji cha Igogo, basi hilo liliharibika ambapo mafundi walianza kulitengeneza hadi saa saba usiku.

“Baada ya matengenezo kukamilika, tulianza safari na baada ya kufika kijijini hapo, tulikuta mawe makubwa yakiwa yamepangwa katikati ya barabara na kuanza kushambuliwa kwa mawe.

“Hawa majambazi walikuwa na fimbo, mapanga pamoja na mawe, abiria wote tuliamuriwa kushuka mmoja mmoja, kuvua nguo zote
na kulala kifudifudi, majambazi walichukua fedha zetu na simu
za mkononi,” alisema Bw. Sangatwa.

Aliongeza kuwa, yeye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya
miguu hivyo aliwaomba majambazi hao ashuke pole pole
kutoka ndani ya basi hilo.

Alisema jamabazi hao hawakukubaliana na ombi hilo hivyo waliamua kumvuta kwa nguvu, kumtoa ndani ya basi na kumwamuru atoe fedha zote.

“Niliwajibu sina fedha zozote wakaamua kunipiga fimbo kichwani, kuchukua sh. 80,000 na kuniachia simu ya mkononi ambayo nilikuwa nimeilalia katika mkono wa kushoto,” alisema.

Alidai baada ya majambazi hao kufanya unyama huo, walitokomea kusikojulikana wakiwa na simu pamoja na fedha walizopora kwa abiria na kuwaacvhia nuo zao.

Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Wilaya ya Igunga, Godfrey Kisila, alisema walipokea majeruhi watano saa 10 usiku ambao walikuwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.

Alisema kati ya majeruhi hao, wanne walitibiwa na kupewa ruhusa, lakini Bw. Sangatwa, bado anaendelea kupatiwa matibabu na amelazwa katika wodi namba nane hospitalini hapo.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Elibariki Kingu, alithibitisha kutekwa kwa basi hilo na kudai kuwa, kiwango cha fedha na simu zilizoibiwa na majambazi hao bado hakijajulikana na juhudi za kuwasaka wahusika waliofanya kitendo hicho zinaendelea.

Aliwaomba wananchi kutoa ushirtikiano kwa Jeshi la Polisi ili wahusika waweze kukamatwa na kufunguliwa mashtaka. Basi
hilo lilikuwa linaendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina
la Bw. Makiselu Madi.

Aliliagiza jeshi hilo wilayani humo kuhakikisha mabasi yote hayatembei usiku ambapo dereva yoyote ambaye atakiuka
agizo hilo akamatwe na kuchukuliwa hatua.
[/SIZE][/FONT][/QUOTE]
 
Hilo basi la wezi niliibiwa vifaa vyangu vyote ndani ya basi kukiwa na watu kama wanne kwenye basi na mlangoni kukiwa na anayeangalia watu wanaoingia na kutoka,hilo ni basi la wezi
 
Igunga hali ngumu ya uchumi kumbuka walihongwa wali maharage kipindi cha uchaguzi nalichama
 
mheshimiwa Baba V naunga mkono hoja,rejea mchango wangu wa maandishi hapo juuu

polisi hapana. Ni afadhali mtekwe mkijua hamna ulinzi kuliko mlinzi kuwachongea dili la kutekwa. Hivi jwtz siku hizi si hawachukui wahuni wa mitaani? Nadhani hawa wangefaa zaidi. Nakumbuka hili jeshi kuna miaka lilibeba vibaka wote mitaani na kuwakabidhi bunduki, acha walivyoanza kuiba !,! Loh!
 
Last edited by a moderator:
Sijui sisi Watanzania kwa sasa tunajivunia nini. Si muda mrefu sana tulikua tunajivunia amani. Je, leo hiyo amani bado ipo?
 
Bora wamewaachia uhai wenu.,hyo michina waliochukua haitawafika mbali..Mbaya vile wamewadhalilisha kuwavua nguo ila nafuu pia kwakuwa hawakuwapa mtihani wa kuchagua kuolewa au kufa.,maana tungekuwa tunaongea mambo mengine hapa.
Mzee Sangatwa unavyoonekana ulikuwa m-bishi kidogo bila shaka ungechagua kifo.,ila nikukumbushe usiwe unawaomba majambazi wakuonee huruma,usitarajie watakuelewa katika matatizo yako kwakuwa wanayoyawaza kichwani mwao ni kuua kama watakutana na kizuizi mawazo hayo huwapa hasira kwa mtu yoyote anayejaribu kuwaongelesha kwa muda mrefu maana wanamuoa kuwa anawachelewesha.

Hapo kwenye red umenikumbusha kuna jamaa waliharibikiwa gari ,wakati wanatengeneza "wazee wa kazi" wakafika, miongoni mwa watekwaji alikuwemo mwanamke, "wazee wa kazi' wakataka "wafaidi "kidogo.Kuna jamaa alifanya kosa kubwa sana, alijifanya kumtetea yule mama, "wazee wakazi" wakasema kama unamhurumia tunakula 0713 yako,aisee jamaa "akaliwa" badala ya yule mama.Kweli hawa jamaa ni kuwaacha na maamuzi yao!
 
Na mara nyingi abiria ndio wenye kulazimisha safari za usiku wa manane, ila ikitokea shida yoyote lawama zinaenda kwa wenye mabasi. Poleni sana mliotekwa.
 
majambazi walikuwa na fimbo, mapanga pamoja na mawe
Kwa nchi ambayo ina guns rights pana kushinda hata USA (kuna very strict gun laws Marekani kuliko Tanzania - ndo maana mtu anaweza kubeba bastola kwenye mkutano wa wazi wa CCM na akaachiwa) nashangaa basi zima linatekwa kwa kurushiwa mawe. Nchi kama Marekani huwezi kuteka kwa mawe gari la watu hata 10 ukakuta hakuna hata mmoja yuko "packing!" abiria watakumwaga utumbo in seconds....kudadadadeki

Hakuna wafanyabiashara wanaotembea na vyuma vya moto? Inakuaje kama mtu unalianzisha, the minute you see them coots throwing stones wakisogelea dirishani unampa mmoja kubwa ya kichwa, waliobaki wataingia kwenye basi?
 
Back
Top Bottom