Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo haraka limewasili nchini

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
3,211
987

Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo haraka limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.

Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.

Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao.

06-dec-basi.jpg

Source: ITV TANZANIA
 
Last edited by a moderator:
Sio mchezo MAN?Me nilidhani wataleta Yutong,spare parts sio mchezo za mjerumani
 
kidogo nikuulize picha plz.angalau umeambatanisha moja.teh teh teh.
 
Sio mchezo MAN?Me nilidhani wataleta Yutong,spare parts sio mchezo za mjerumani

mkuu mbona ukitazama kwa haraka haraka halina tofauti na haya magobore ya kichina tunayopanda kila siku hapa dar?!ni kweli la mjerumani hilo.mmh!
 
Yanafanana kidogo na magobore haya ya kichina ila lazima kuwe na tofauti, kwa ninavyojuwa mabasi haya ni full AC hivyo haitakiwi kuona vioo vya madirisha vipo wazi namna hii, pili mabasi haya huwa hayawi na kondakta, ni dereva tu ndiye anakuwemo humo na kwa tiketi zitatakiwa kuuzwa dukani kama unavyonunua vocha madukani ukifika mlangoni una-validate tu tiketi hiyo kwa machine maalum yenye alarm, kama ukitaka kununua tiketi kwa dereve mlangoni tiketi itagharimu mara 2 zaidi ya bei ya dukani, tatu abiria hatakiwi kupiga kelele nashuka kituo gani, hapana pembeni yako kuna button ya alarm ukiona kituo kinachofuatia unashuka unaibonyeza tu na dereva anasimama next, pili kunakuwa na ratiba ya basi linatoka kituo A saa fulani itapita kituo B saa fulani mpaka mwisho pasipo kuchelewa wala kuwahi hata dakika moja.

JE YATAKUWA NDIYO HAYA? Tusubiri.
 
Mbona linafanana na lile la airpot.pia hii serikali ni kweli haina hela na kufanya hii barabara ikajengwa mpaka kibaha.
 
Yanafanana kidogo na magobore haya ya kichina ila lazima kuwe na tofauti, kwa ninavyojuwa mabasi haya ni full AC hivyo haitakiwi kuona vioo vya madirisha vipo wazi namna hii, pili mabasi haya huwa hayawi na kondakta, ni dereva tu ndiye anakuwemo humo na kwa tiketi zitatakiwa kuuzwa dukani kama unavyonunua vocha madukani ukifika mlangoni una-validate tu tiketi hiyo kwa machine maalum yenye alarm, kama ukitaka kununua tiketi kwa dereve mlangoni tiketi itagharimu mara 2 zaidi ya bei ya dukani, tatu abiria hatakiwi kupiga kelele nashuka kituo gani, hapana pembeni yako kuna button ya alarm ukiona kituo kinachofuatia unashuka unaibonyeza tu na dereva anasimama next, pili kunakuwa na ratiba ya basi linatoka kituo A saa fulani itapita kituo B saa fulani mpaka mwisho pasipo kuchelewa wala kuwahi hata dakika moja.

JE YATAKUWA NDIYO HAYA? Tusubiri.
dah I wish iwe hivyo huwa naumia sana kuona watu wamesimama tena wana safari ndefu
 
My brother hayo hapo juu unataka uya implement Dar ? thubutu. Dar lazima makonda wawili na baunsa au polisi kuzuia wizi na uharibifu ndani ya gari. Hapa kuna wamasaai. wagogo. wakwere. wasukuma na wamakonde ambao hata kuflash choo tu ni kazi. itakua hayo uliyoandika ?
 
Teh teh wacha wenyewe wakusikie....
 
  • Ni kweli tusubiri time will tell
 
kama ni hivyo mbona tutapotea wengi, sisi wengine ni wageni kwenye baadhi ya vituo..... kelele za kondakta ndio mwongozo wetu itakuaje sasa.?
 
My brother hayo hapo juu unataka uya implement Dar ? thubutu. Dar lazima makonda wawili na baunsa au polisi kuzuia wizi na uharibifu ndani ya gari. Hapa kuna wamasaai. wagogo. wakwere. wasukuma na wamakonde ambao hata kuflash choo tu ni kazi. itakua hayo uliyoandika ?

Hao uliowaandika (kwa kumaanisha wa kutoka shamba) wala hawana maneno, ni wastaarabu wa kuzidi, tabu iko kwa watoto wanaojifanya wa mjini, wanajiona wajanja wajanja na wanajua kila kitu...hao ndio tatizo hasa, hawachelei kutokea dirishani, kuchora siti kwa markerpen, kumtukana dereva, kugonga bodi badala ya kubonyeza button na vituko kibao, hao unaowasema hawawezi hata kufungua kioo cha gari, anahofia kumuudhi jirani aliyekaa naye!! Watao haribu mambo ni hawahawa wasomi wa vyuo vya kata, lakini nadhani yatakuwa na camera ndani dereva ataona kinachoendelea, kuwe na utaratibu tu wa kupiga fine wajingawajinga kama hao!
 
kama ni hivyo mbona tutapotea wengi, sisi wengine ni wageni kwenye baadhi ya vituo..... kelele za kondakta ndio mwongozo wetu itakuaje sasa.?

Hata mimi niliwaza hilo, mgeni hawezi kujua vituo. Nadhani kutakuwa na led display inayoscroll majina ya vituo, kila basi linapoondoka kituo kimoja display inaonesha kituo kinachofuata!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom