Basi la Kampuni ya Classic Coach inayofanya safari zake Uganda na Tunduma wananinyanyasa sana naombeni ushauri wenu

Mlemi

Senior Member
Mar 24, 2017
161
91
Habari wadau wote wa jukwaa hili. Iko hvi mnamo tarehe 12/1/2018, nililikata tiketi ya basi hyo tajwa hapo juu. Nililipia pia mizigo ya furushi nne zenye nguo na viatu na nikahakikisha zimeshapakiwa kwenye basi ndo nikaondoka.

Gari ilikuwa inaanza safari alfajiri ya tarehe 13/1/2018 na ikumbukwe mizigo yangu ilipakiwa kwenye basi usiku wa tarehe 12. Na mimi nilikuwa nashukia singida ili nichukue basi ingine niingie ma home town Arusha.

Basi basi ikaanza safari hyo alfajiri ya tarehe 13, na tulipofika boda ya Mtukula basi ilikaguliwa na baadae nilielekezwa na kondakta kwa mtu wa tra ili nikalipie kodi ya mzigo wangu. Nikakadiriwa mafurushi manne na nikalipia, baada ya kulipia yule kondakta akanifuata na kuniambia furushi langu moja halipo.

Baada ya kuhoji kulikoni wakadai huenda lilishushwa bahati mbaya na huenda limesahaulika kampala. Basi ikabidi wapige simu kampala na wakaniambia kuwa furushi lipo na lingetumwa kesho yake na basi ya Falcon. Mimi kwa kutumia busara nikakubaliana nao, kesho yake ikabidi nisubirie mzigo wangu Singida bila mafanikio.

Nilipompigia kondakta akaniambia walinizuga tu ili niwaache waendelee na safari ila ukweli n kwamba mzigo haujaonekana na haujulikani ulipo.

Akadai kuwa siku akirudi Uganda atafuatilia mwenyewe ili ajue ulipo, aliporudi Uganda akaniambia kuwa ameuona na akaniuliza ulikuwa umeandikwa jina gani nikamjibu, na akauliza una nini ndani nakamjibu, akaulizia pia thamani ya mzigo nikamjibu.

Nilipompa thamani ya mzigo akaanza kusema nimeweka tamaa na yakwamba huo mzigo hauna thamani na kuwa yeye hawezi tena kufuatilia na kama nataka nifuatilie mwenyewe Uganda.

Mzigo una thamani ya Tsh 2,186,000/= sawa na Ugs 3,279,000/=. Wakuu naombeni ushauri nifanyeje ili nipate haki yangu? Na pia kama kuna mtu anamjua mmiliki wa haya mabasi anipe hata namba zake. Nasikia n mwarabu na makao makuu yao yako Ilala Dar es salaam.
 
Pole mpendwa haki haipotei fuatilia tu
Yataka moyo tumia tu gharama maana haina jinsi
 
Back
Top Bottom