Basi la Classic kutoka Kampala lililopata ajali Shinyanga lilikuwa limebeba Wazanzibari tu?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
46,911
2,000
Kupitia taarifa ya habari ITV wameonekana abiria waliopata ajali ya basi la Classic kutokea Kampala kuja Dar es Salaam wakielezea namna ajali hiyo ilivyotokea.

Majeruhi wote waliohojiwa ni Wazanzibar na abiria watatu waliofariki ni Wazanzibar.

Naibu waziri wa mambo ya ndani ambaye ni Mzanzibar ndiye aliyewatembelea majeruhi na kamishna wa maafa kutoka SMZ.

Ndio sijaelewa kama ajali hii ilihusisha Waunguja pekee ama?

Mliofuatilia tafadhali!
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,310
2,000
Karne ya 21 middle class wa kitanzania anakuja na uzi kama huu wa kibaguzi, kweli nchi hii sijui nani katuloga why until now tuna colonial hangovers? Why mpaka leo hii kitu bado tunayo?

Waliopata ajali ni binadamu kama sisi na ni watanzania!na watambuliwe hivyo huku Lingusenguse tuna watanzania sio wandendeule au wangoni au wamanda etc etc.
 

Msangarufu

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,626
2,000
Karne ya 21 middle class wa kitanzania anakuja na uzi kama huu wa kibaguzi,kweli nchi hii sijui nani katuloga why until now tuna colonial hangovers? Why mpaka leo hii kitu bado tunayo? Waliopata ajali ni binadamu kama sisi na ni Watanzania na watambuliwe hivyo huku Lingusenguse tuna watanzania sio wandendeule au wangoni au wamanda etc etc
Una matatizo wewe kisa kuuliza ni Wazanibar basi umepanic.
 

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,271
2,000
Mkuu kwa kuwa Zanzibar ni sehemu ya JMT, ingetosha tu kutujuza kuwa Watanzania wenzetu wamepata ajari mkoani Shinyanga wakitokea nchi jirani ya Uganda.
 

Darius RR

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
304
1,000
Mara wazanzibar mara waunguja sasa tukueleweje?
Kwanza tunahitaji kujua kama ni Wazanzibar, then tunatakiwa kujua ni Wapemba au Waunguja.

Baada ya kujua hilo ndo tunaangalia kama ni wa-Unguja tunawapa huduma bora, kama ni wapemba tutaenda nao hivi hivi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom