Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
Basi la Adventure toka Mwanza kwenda Kigoma lililoondoka Mwanza leo asubuhi saa 11.30 alfajiri, limepata ajali ya kuungua moto katika kijiji cha Nyantakara, karibu na Runzewe.
Hakuna mtu aliyepoteza maisha, ila kuna watu wana majeraha ya moto, na wengine wamevunjika viungo kutokana na kuruka toka kwenye basi kujisalimisha. Abiria wote wamepoteza mali zao zote walizokuwa nazo ambazo zimeteketea kwa moto.
Chanzo cha moto hakijajulikana, lakini basi lenyewe lilikuwa chakavu sana, na huenda ni hitilafu za umeme wa basi.
Kwa sasa abiria wamekwama na hawajui wataendeleaje na safari yao.