Basi kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Nchi imegubikwa na majonzi
Dunia inatetema
Wenye huzuni na furaha
TAA IMEZIMIKA na kuacha giza totoro

Ila imeandikwa:

Mathayo 25
1 Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.

2 Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.

3 Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao;

4 bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.

5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.

6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.

7 Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.

8 Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika.

9 Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.

10 Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.

11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.

12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.

13 Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
 
Hakika tunatakiwa kukesha kwa kutenda mema hapa duniani maana hatujui siku wala saa!

Ukiburi, majivuno, ubinafsi, ukatili, ukaidi, uonevu, dhuluma! Vyote hivi vinatuondolea historia nzuri ya kuviachia vizazi vyetu vya baadae.
 
Je hamkupaswa kukesha nami,alipokwisha kuyasema hayo akapita kati yao akaenda bustanini kuomba.
 
Back
Top Bottom