basi hili la tahmeed (pichani) lmetushusha njiani

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
221
431
Tarehe 24/05/2019 nilipanda basi tajwa nikielekea mombasa nchini kenya kwa shughuli maalum basi liiliondoka ubungo saa sita mchana, kufika Tanga ilisimama kidogo kisha kuendelea na safari baada ya kutoka nje kidogo ya jiji la Tanga alitokea muhudumu mmoja shombeshombe na kutuomba tiketi zetu bila kujua lengo lake, basi lilisimama na tukapewa maelekezo kuwa tunahamishiwa kwenye coaster ambalo kiuhalisia lilikuwa limejaza sana mizigo na abiria pia, abiria wengine walipanda tukabaki wanne ambao hatukuwa tayari kupanda kwani gari lilikuwa limejaa mno tulisisitiza turudishwe Tanga mjini na tupewe tiketi zetu yule muhudumubwa basi alikataa katakata ndipo nilipoomba msaada wa RTO Tanga maarufu kama afande Solomon (alijizolea umaarufu kwa kupambana na majambazi ubungo na kuokoa hela za benki miaka ya nyuma) nilipiga picha ya gari husika, yule muhudumu baada ya kuona hali hiyo alinifuata kwa vitisho "hata sisi pia tunajua watu usitafute shari hutaiweza" huyu kaka huwa anakata tiketi kwenye ofisi ya tahmeed Tanga kisha kuyasindikiza magari na kuongea na simu muda mrefu akiwapa maelekezo wahudumu wa basi ntaitafuta picha yake pia, alikuwa anajiandaa kuondoka na kutuacha pale usiku ule, nilimkamata na kumbeba tayari kumrusha kwenye mtaro alipiga mayowe kiuhalisia nilikuwa tayari kwa lolote, ndipo alipompigia simu bosi wake kumueleza hali halisi ambapo iliamuriwa gari iondoke na kuendelea na safari....hili gari lina namba za usajili za kenya kama inavyoonekana ila wanatakiwa kuhesimu utu wetu (social media for social justice)
 
Attachments

  • 20190524_202253.jpg
    20190524_202253.jpg
    91.2 KB · Views: 55
Umezidi mikwara kwenye story yako. Ulivyompigia huyo Solomon hata hausemi nini alikuelekeza. Halafu mtu uliyembeba kutaka kumtupa kwenye mtaro anapataje nafasi ya kukumbuka na kupiga simu kwa bosi wake, na baadaye wanaafikiana kukuacha njiani kiboya huku unaona!?
 
Pombe kali.... umelewa? Mbona hatuoni kilichoendelea? Ama unataka kuwavurugia wakenya biashara?
 
Baada ya amri ya bosi, safari iliendelea au la?
 
Umezidi mikwara kwenye story yako. Ulivyompigia huyo Solomon hata hausemi nini alikuelekeza. Halafu mtu uliyembeba kutaka kumtupa kwenye mtaro anapataje nafasi ya kukumbuka na kupiga simu kwa bosi wake, na baadaye wanaafikiana kukuacha njiani kiboya huku unaona!?

Alichonijubu RTO sikutaka kukiandika ili mambo yasiwe mengi, nilitegemea watu wenye akili kujua chanzo cha mimi kujichukua sheria mikononi inaitwa fasihi ndugu.
 
Yale ni magari ya kubeba mirungi,siku hizi ziyapandagi ,yanachelewa sana njiani sababu uhamiaji na polisi wa madawa ya kulevya huyasimamisha sana.
Na usiku ndio muda wa hao mabosi na wWeka madawa kwenda kuyapanga ndani ya basi.
Pole sana,ila ulipofunga ndipo sijaelewa waliambiwa waendelee na safari wamekuacheni mnashangAA a tiketi wamesepa nazo au basi liendelee na safari na ninyi watu wanne tu.
 
Umezidi mikwara kwenye story yako. Ulivyompigia huyo Solomon hata hausemi nini alikuelekeza. Halafu mtu uliyembeba kutaka kumtupa kwenye mtaro anapataje nafasi ya kukumbuka na kupiga simu kwa bosi wake, na baadaye wanaafikiana kukuacha njiani kiboya huku unaona!?
Umewaza sawia na mimi.
 
Yale ni magari ya kubeba mirungi,siku hizi ziyapandagi ,yanachelewa sana njiani sababu uhamiaji na polisi wa madawa ya kulevya huyasimamisha sana.
Na usiku ndio muda wa hao mabosi na wWeka madawa kwenda kuyapanga ndani ya basi.
Pole sana,ila ulipofunga ndipo sijaelewa waliambiwa waendelee na safari wamekuacheni mnashangAA a tiketi wamesepa nazo au basi liendelee na safari na ninyi watu wanne tu.
Tuliendelea safari watu wanne tu.
 
TAHMEED inaenda kufa soon, wajinga sana

Juzi tarehe 27 May walikuwa wanatoka Tanga, kwenda Arusha..Kufika KIA pale mbele ikafia pale. Tukaone gari imesimama imepaki pembeni, dreva na conductor wakashuka, abiria tuko kwenye gari, hatujaambiwa kitu..ikabidi nasi tushuke tuulize. Ndio dreva akasema amemtuma Konda kwenda kuchomelea chuma.

Tukakaa wee zaidi ya Lisaa, Ikaja TAHMEED ingine..ikasimama na hawakuchukua abiria...ilisimama 5 minutes wala hawakuongea na wenzao

Pia customer care ni mbovu sana, hawana care...

Mabasi ya kupanda na yenye kujali abiria ni haya hapa chini

kutoka Tanga ni RAQEEB

Kutoka Morogoro ni LIM na BM

Kutoka Dar ni Kilimanjaro Express, Dar LUx, Extra luxury, KIDIA one na Dar express
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom