Basi gani zikitoka Mwanza zinafika Dar bila kulala Morogoro?

Abood ya Dar- Mwanza ni la kawaida tu
mwendo wake hauzidi 80KPH
Magari yake yana Speed Gavana..
Magari yanayovuta mwendo ndo..
KISBO
KISESA
ZUBERI
na kuna basi linaitwa MJ
Bodi limechokachoka lakini linapepea hatari..akitoka harudi kushoto..
 
Hapa ndo umenena, na hawaingii Stend ndogo ndogo za wilayani, mfano Wakitoka MWZ hawaingii Misungwi ni hadi SHY, Nzega ni Lazima coz ndo njia wakitoka hapo Igunga hawaingii ni hadi Singida pale kwenye mgahawa, kwa kifupi wanajali sana muda, halafu Hizi Gari zote nimezipanda Kisbo Kahm_Dar, Tabora_Dar, MWZ_Dar, niliwahi kuongea na konda mmoja Kipindi Niko kahama Coz wao kwa sasa licha ya kutokuendesha speed zaidi ya 80, wanafika Kahama saa5 kamili usiku, somtym 4:45, DarLux na RedBelt wanafika saa6:30 kahama, na Mabasi mengine ya Bukoba yanalala Nzega, Akasema kampuni huwa imetenga kila safari moja Sh Laki 1 na NUSU kwa kila gari kwa ajili ya Torch kwa hiyo hata siku1 hawapigwi torch. Now ndo wababe wa njia za Dar_Tbr, Dar_Khm na Dar_MWZ

Mkuu michongo mingine uvunge tu..si unajua mambo ya biashara! Utawatia jamaa matatani..
 
e5097892369e251df90a91f41b2cb8ec.jpg

Kisbo safari
Dar-Mwanza (1152 km)
Scania 94D_310
Nauli=Utaiweza tu!


Mbona Kisbo unaweka picha za ajali walizowahia pata kipindi cha nyuma? Lakini hayo makampuni mengine japo yameshawahi pata ajali kadhaa tu lakini huweki picha zao..
 
563c6253d8c6cf3b9853a8baab446db4.jpg

Mm mwenyewe nikitafutia watoto ugali
Macho mbere kodo,usukani nashika kwa mkono mmoja tu dar mpaka mwanza!!! Mkono mwingine napangua gia tu!!!
 
Magari ya mwanza dar asilimia kubwa ni mabovu ambayo yalishafanya kazi barabara za dar arusha na dar mbeya yakaonekana vimeo ndo yanaletwa mwanza. Mm naishi mwanza ila kila nikipanda basi siku hizi lazima mizinguo kibao njiani
Acha uongo ww ni mtu mzima,

Niambie dar lux, Zuberi au Kisesa, Super Sami, Kisbo, JM, Falcon, Leo luxury zimefanya kazi wapi?
 
Wapi City BOY, Kisbo haina mpinzani Mkuuu
Ligi ilikuwa ni Ally's sports na Lucy star, hapo miaka ya 2009.

Saa moja kamili chuma zimemwaga upepo Nyegezi, leo Ally's akiwa wa kwanza luck star wa pili, luck star wa kwanza Ally's wa pili
 
Ligi ilikuwa ni Ally's sports na Lucy star, hapo miaka ya 2009.

Saa moja kamili chuma zimemwaga upepo Nyegezi, leo Ally's akiwa wa kwanza luck star wa pili, luck star wa kwanza Ally's wa pili
Ilikua ligi ya hatari sana,bus hizo zilikua zinatembea ile mbaya hasa Ally's sports.
 
Watanzania watu wa ajabu sana eti wanamshauri mtu panda gari hii unafika haraka.Wakiona gari inakimbia sana dereva anasifiwa na wanashangilia.Ajali ikitokea hawakawii kusema dereva alikuwa mwendo kasi.Tubadilike watanzania kama mtu una haraka si upande ndege?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom