Wakuu habari ya wakati huu.
Naomba kujua ni basi gani zikitoka mwanza zinaweza kufika Dar moja kwa moja bila kulala Morogoro maana nimeambiwa kwamba gari nyingi zinalala Morogoro.
Lakini pia nimeambiwa kama gari inafika Morogoro kabla ya sa 4 usiku hua zinaruhusiwa kuendelea na safari, naomba kujua ni basi gani zinaweza kufika Dar siku hyo hyo hata kama ni sa 8 usiku toka mwanza.
Ahsante.
Hazihusiki maana wanalenyeza rupia mapemaZenyewe hazihusiki na speed 50?
Halaf ndo kiboko yao njia nzima,sio dar mwanza tu hata dar tabora panda kisbo kwa usafiri wa harakaHivi Kisbo ana Gari za kichina kweli? Naona yote masufuria!
Mkuu, mwendo wa kasi ndo chanzo kikubwa cha ajali za barabarani; ni afadhali kwenda pole na kufika salama.
Dar- Mwanza basiIla hyo kisbo ni hatari asee,,niliwahi kuipanda mara 1 tu kutokea dom,,ile gari haikupitwa na gari hata 1 mpaka inaingia ubungo,jmaa alikua anaovertake mpaka ubungo maji
Kisbo mkuu....ile company sijui wanatumia engine gan
Hio bus ya kuitwa Kisbo hio..weka mbali na watoto!
Kibo na kisbo mkuu darlux kimeo
Ukitaka kusafiri kwa aman bila presha...mwendo safi na unafika ubungo kabla ya sa sita usiku panda Zuberi au kisesa...hzi gar hazilali njiani...na mwndo ni friendly sana...achana na ksibo utavunja miguu
Hahahahahah kama Ulaya vileNi hatar mkuu full kipupwe hata mwl jk nyerere haioni ndan
airbusWakuu habari ya wakati huu.
Naomba kujua ni basi gani zikitoka mwanza zinaweza kufika Dar moja kwa moja bila kulala Morogoro maana nimeambiwa kwamba gari nyingi zinalala Morogoro.
Lakini pia nimeambiwa kama gari inafika Morogoro kabla ya sa 4 usiku hua zinaruhusiwa kuendelea na safari, naomba kujua ni basi gani zinaweza kufika Dar siku hyo hyo hata kama ni sa 8 usiku toka mwanza.
Ahsante.
Update:
Ahsanteni kwa ushauri, nilifuata ushauri wenu wakuu, mgeni wangu kafika na gari ya Kisbo. Ahsanteni sana.
Wana bajeti ya faini tayari.Hizo ni taarifa nzuri kwa traffic police. Wataanza na hiyo Kisbo kwani itakuwa inahatarisha roho za watu kwenda peponi au motoni.
UKIOAMBIWA KITU JF LAZIMA UONGEZE NA YA KWAKO MKUU HAKUNA BASI INAYOACHA KULAALA MOROWhat's the difference? Kisbo saba usiku, Zuberi sita usiku. Ndio "mwendo friendly" huo?
Kamanda Sirro, na wenzako SUMATRA, leo mchana uligombezwa kama mtoto mdogo pale bandari kavu kwa kusubiri Rais avamie sehemu ndio mjue kuna tatizo.
Haya, mshaambiwa hapa kwenye ulinzi shirikishi wa JF, mabasi ya Kisbo, Darlux, Kibo, Kisesa, Zuberi etc. ni roho mkononi, hayazimi engine saa nne usiku. Usisubiri Magufuli avamie Ubungo saa saba usiku kubishana na madereva wa Kisbo. Fanya kazi yako, achana na siasa.
Tutasikia karibuni zinafanyiwa figisu na kupigwa faini za kutoshaMission accomplished, Sumatra wameshakusanya 'data' zao kwa hisani ya wafukunyuku wa Jeiefu...
Hii ndio moja ya sababu Jeiefu haiwezi kufungwa na 'sirikali'...