Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,806
- 11,968
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa ameelezea mafaniko ya Serikali ya awamu ya sita katika kwenye kada ya elumu ambapo amesema mwaka 2021/22 walimu wapya 24749 wameajiriwa huku malimbikizo ya mishahara pamoja na ulipaji wa pesa za pensheni kwa wastafu vikifanyika kwa wakati.
Pamoja na uwepo wa mafanikio haya, kumekuwepo na changamoto tano kubwa zinazo wakabili walimu ambazo ni
- Kutokulipwa stahiki za uhamisho, likizo na mazishi
- Kutokupewa vibali vya kwenda masomoni pamoja na malipo ya mafunzo hayo
- Uwepo wa mawasiliano hafifu kati ya walimu na viongozi wao
- Kutokupandishwa madaraja
- Upungufu wa nyumba za kuishi
Kuhusu uwepo wa mawasiliano mabovu miongoni mwa walimu na viongozi wa ngazi ya halmashauri, kata na shule, Waziri amewaagiza viongozi hao kushirikiana vizuri na walimu, pia ameelekeza viongozi wanaohudumia walimu waache tabia ya kukaa maofisini, badala yake waende kwenye shule kufuatilia ufundishaji pamoja na kusikiliza kero zao wakiwa huko.
Katika kutatua changamoto ya upandishwaji vyeo na madaraja, Waziri Bashungwa ameagiza Tume ya Utumishi wa walimu kuziwesha kamati za tume za utumishi za wilaya kuwapandisha walimu madaraja pamoja na kuwapandisha vyeo kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
Aidha, amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanawasimamia watendaji wanaotoa huduma kwa walimu kwa kuhakikisha kuwa wanawafuata waalimu mashuleni huku akipiga marufuku kuwaacha walimu wakipita kila ofisi ya halmashauri wakitafuta huduma kwani wanapaswa kupelekewa huduma shuleni badala ya watoa huduma kukaa maofisini.
Pia, mwalimu akiandika barua kwenye mamlaka ya Serikali za mitaa akitafuta huduma anapaswa kujibiwa kwa maandishi ndani ya siku saba.
Kuhusu upungufu wa nyumba za walimu, Serikali imeanza kushughulikia jambo hili kwa kutenga bilioni 55.57 kwa kuanzia ili kujenga nyumba kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi na itaendelea kuboresha kila mwaka.