Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,819
- 13,582
Bashungwa ametoa onyo hilo, leo Septemba 04, 2024 jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili masuala ya mazingira katika utekelezaji wa miundombinu nchini.
“Kuna Makandarasi mnaochukua zabuni za Ujenzi wa Majengo lakini baada ya kusaini mkataba, uswahili unaanza mpaka aliyekupa kazi anajiuliza hawa ndio Wazawa ambao Serikali inawatengenzea mazingira ya kuwapatia fursa mara dufu, sasa niwaombe kabla hatujachukua hatua mjirekebishe” amesisitiza Bashungwa.
Kadhalika, Bashungwa ameeleza kuwa dhamira ya Mheshimiwa Rais ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kuwawezesha Makandarasi Wazawa ambapo tayari Wizara ya Ujenzi imesharekebisha masharti na kutoa fursa za ushiriki wa utekelezaji wa miradi kwa Wakandarasi nchini.
Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi itaendelea kuhakikisha usimamizi wa ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara, madaraja pamoja na majengo yanaenda sambamba na utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Chemba ya Sekta ya Ujenzi na Miundombnu Tanzania, Bw. Steven Mkomwa ameeleza kuwa mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali kuziangazia Sera, Sheria na Teknolojia zitakavyoweza kusaidia Sekta ya Ujenzi na kuweza kutoa mchango chanya katika masuala ya mazingira pamoja na uwepo wa miundombinu ya kijani.