Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,682
- 149,883
Mohamed Bouazizi,kijana wa kitunisia, ndie chanzo cha mapinduzi katika nchi kadhaa za kiarabu(Arab Spring), mapinduzi yaliyaonza mwaka wa 2011 katika nchi ya Tunisia na baadae kusambaa katika nchi zingine za kiarabu..
Mohamed Bouazizi alikuwa ni street vendor (Mmachinga) katika mji mmoja mdogo wa Sidi Bouzid huko nchini Tunisia.Alikuwa akifanya biashara ya kuuza matunda na mboga za majani kwa kutumia mkokoteni ambapo alikuwa anatembeza mitaani.
Ilikuwa ni December 17 mwaka 2010,kijana huyu alipokumbana na nguvu ya dola kwa kufanya biashara bila kibali ambapo alinyang'anywa mkokoteni na kibaya zaidi alipigwa kibao na askari polisi wa kike kitendo kilichomuumiza sana.
Baada ya kutendewa vivyo sivyo,kijana huyu aliamua kwenda katika ofisi za Gavana wa Jimbo kulalamika ila kwa bahati mbaya hakuruhusiwa kuonana na Gavana jambo liliomuongezea hasira na machungu.
Kutokana na hasira alizokuwa nazo, kijana huyu aliamua kwenda sheli na kununua petroli katika kidumu na kurudi katika Jengo la ofisi ya Gavana ambapo aliamua kujimwagia petroli hiyo na kisha kujitia kiberti mbele ya Jengo hilo na kuungua vibaya.
Alikimbizwa hospitalini akiwa na majeraha makubwa ya moto ambapo alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili na ilipofika January 4 mwaka 2011, Bouazizi aliaga dunia.
Kitendo cha Bouazizi kujilipua ndio kilichoamsha hasira za wananchi wa Tunisia na kuanza maandamano ya kupinga utawala wa Raisi wa Tunisia, Dikteta Zinel al-Albidine Ben Ali ambae nae aliamua kutumia mabavu kujaribu kumaliza uasi wa wananchi lakini vikosi vyake havikuweza kufua dafu mbele ya nguvu ya umma na hatimae wananchi walimn'goa madarakani na ndipo uasi wa namna hiyo ukasambaa katika mataifa mengine ya kiarabu kama vile Misri, Libya na Yemen.
Funzo tunalopata hapa ni kuwa,mtu mmoja tu anaweza kusababisha nchi ikavurugika au kuleta mabadiliko ya kiutawala katika nchi yake kwa kuwafanya watu kuwa majasiri, kusahau tofauti zao na kuamua kuunganisha nguvu kudai mabadiliko ya wanayoyataka.
Kama ilivyokuwa kwa Bouazizi,Daudi Bashite anaweza akafanya wabunge waungane na kuwa kitu kimoja bila kujali tofauti zao za kiitikadi na kuamua kutumia njia ya kikatiba kuandika historia ambayo hakuna mtu alieitarajia kama inaweza kuja kutokea.
Sometimes watu kama kina Bashite /Bouazizi hutumiwa tu na Mungu kutimiza makusudio yake kwa watu wake.
Hata hivyo,story hii pia ina faida moja tu nayo ni kuweza kusaidia/kuwakumbusha watawala kuchukua hatua mapema kabla mambo hayajaharibika.
Ni mtazamo tu.