Uchaguzi 2020 Bashiru, Polepole na Kabudi hamna maneno ya kumjenga mgombea wa CCM. Pia mshaurini ya kuongea

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,824
35,822
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Treni la uchaguzi linapozidi kuchanja mbuga si haba kukumbushana tunapojikwaa hapa na pale ili miradi tuweze kufika salama. Katika harakati kama hizi ni vizuri kuirejea historia ili kuweza kusonga tukiwa kifua mbele zaidi. Ndiyo maendeleo hayo ati!

Miaka ya nyuma, Mzee ruksa akiwa mgombea mpendekezwa wa CCM aliwahi kusema, "mimi mgombea wa chama ni kama mwali anayetaka kuolewa. Si sahihi sana kwangu, kujipigia mno debe." Maneno ya hekima kabisa.

Akiendelea mzee ruksa alisema, "mwali anayetaka kuolewa akiulizwa, eti unataka kuolewa? Yeye hucheka cheka tu na hiyo ndiyo dalili kuwa amekubali huyo!" Akamalizia, "akishabikia kwenye kuolewa huko - mchimvi huyo, mchimvi huyo!" Maneno kuntu kabisa.

CCM, mbona huyu mwali wetu wa sasa anatuacha hoi na midomo ikiwa wazi? Ama kwa hakika kuna mengi anasema ambayo kwa kweli ni bora angeshauriwa angalau akakaa kimya tu. Kujikweza mno hadi kudhani na kutaka kutuaminisha ati tusipomchagua yeye kama taifa tutakuwa tumepata hasara isiyo mfano ni kuvuka mipaka kusiko kwa lazima hata kidogo.

Tumshaurini kama anasikia. Inahitaji busara ndogo sana kuona walakini mkubwa kwenye kujipigia debe huku. Hawakukosea waswahili kunena kuwa: "chema chajiuza na kile kingine chajitembeza."

Upande mwingine ni katika ITV dak. 45 majuzi. Katika kipindi hicho, amenukuliwa Dk. Bashiru akitamka kuwa hawa wasanii wakubwa wakubwa katika mikutano ya mgombea wetu huyu wapo kuwa kwa kujitolea zaidi.

Kuwa wasanii hawa hawalipwi chochote na wanafanya show zote kwa kumpenda mno mgombea wetu na chama chetu. Kuwa wasanii hawa ni wanachama wetu kama tulivyo wengine wakiwamo kina nchukuma na kina vibajaji.

Bashiru alionyesha kuwa hata kwa nyomi la vyombo vya habari (vya umma na binafsi) vinavyomfuatilia vilivyo mgombea wetu na chama chetu ni mapenzi tu ya moyo kutokana na kukubalika kwake. Hayo hayo kama ya kina kiba, diamond na kina konde boy.

Yote kheri. Hivi bashiri anawafanya watanzania wajinga kiasi hicho? Kuwa hayapo maslahi binafsi ya wazi au ya hisani sasa au baadaye kwa taasisi na watu wa namna hii wakiwamo wasanii wetu hawa?

Vipi misukosuko zikiwamo kesi za kubambikiziwa na hata zile pendwa za kutakatisha pesa kwa wale wanaojaribu kujitokeza pande zile zingine?

Kwamba, watanzania hawanazo kumbukumbu hai za kufungiwa zikiwamo biashara, bambikizi bambikizi zikwamo kodi na mashinikizo lukuki yenye mrengo wa kushinikiza kutengwa kwa vyama vya upinzani ili kujiwekea ukiritimba wa fursa zote? Hii mbona itakuwa kujidanganya wenyewe?

Ndani ya CCM hatuna budi kutofautisha kauli za wanaojinasibu kuwa ni kina darasa la saba. Hasa wale ndugu zetu wapendwa akina vibajaji na kina nchukuma.

Bashiru, pole pole, Kabudi na hata Kafulila hamna maneno mazuri kweli ya kumjenga mgombea wetu huyu ili asiendelee kuwa kituko zaidi machoni mwa watu na hata kwa watoto wadogo?

Nchukuma na vibajaji kutokuona umuhimu wa midahalo ni sawa. Lakini hata nyinyi wakuu?

Jitendeeni haki basi ili angalau usomi wenu ukaweze kuwa na mchango wa maana japo kidogo kwenye nchii hii?

Jamani tu wamoja:

Kwa pamoja tuwasaidie watia nia wetu kukubalika kwa wananchi

Uchaguzi huu na usitufanye kujitoa hadi ufahamu wa kawaida tu.

Niombe kuwasilisha.
 
Naona unazungumza kinyume, mshaurini Tundu, sijui la wapi, aache kubwabwaja
 
Naona unazungumza kinyume, mshaurini Tundu, sijui la wapi, aache kubwabwaja

Mkuu nazungumza kimbele. Haiyumkiniki ni bandiko lina ukweli na kutakuwa limekugusa.

Yote kheri.

Ila usikonde mkuu hii ni tathmini moja tu. Tutawafikia wote hadi mzee Spunda tutapokuwa tumefika kwenye ubwabwa.
 
Mkuu nazungumza kimbele. Hii ni tathmini moja. Tutawafikia wote hadi mzee Spunda.

Tathimini yako haiko huru inapotosha. Unless wewe umezaliwa 1990s, kwa tuliokuwepo hizi awamu 5, nakuapia hakuna wa kulingana na JPM katika kutafuta maendeleo ya Tanzania.

Siyo mwanasiasa wa kulimiliki jukwaa kama akina Kikwete bali ni mthubutu na hakuna wa kujilinganisha naye. Najua wengi (walofisadi nchi hii) wana kinyongo naye, lakini Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Ni uchuro kusema ati mtu unataka maendeleo ya watu si vitu - Hivi huyo mtu anayesema uharo huo ana akili? Maendeleo yanaanzia kwa vitu ndipo watu wanatumia hiyo miundombinu kujiletea maendeleo. Stop cheating people na siasa uchwara zenu
 
Tathimini yako haiko huru inapotosha. Unless wewe umezaliwa 1990s, kwa tuliokuwepo hizi awamu 5, nakuapia hakuna wa kulingana na JPM katika kutafuta maendeleo ya Tanzania. Siyo mwanasiasa wa kulimiliki jukwaa kama akina Kikwete bali ni mthubutu na hakuna wa kujilinganisha naye. Najua wengi (walofisadi nchi hii) wana kinyongo naye, lakini Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Ni uchuro kusema ati mtu unataka maendeleo ya watu si vitu - Hivi huyo mtu anayesema uharo huo ana akili? Maendeleo yanaanzia kwa vitu ndipo watu wanatumia hiyo miundombinu kujiletea maendeleo. Stop cheating people na siasa uchwara zenu
JPM ni bonge la kiongozi. Tungepata mtu kama yeye kwenye awamu ya 2,3,na 4 tungekuwa mbali sana. Hawa kina Lissu, kuwajadili ni kupoteza rasilimali muda tu maana najua hakika hawawezi shinda.
 
Mzee kupenda kubaya Chongo anaitwa Makengeza Manunuzi makubwa bila bunge ni sawa? Museveni juzi bila baraka za bunge sawa?
 
JPM ni bonge la kiongozi. Tungepata mtu kama yeye kwenye awamu ya 2,3,na 4 tungekuwa mbali sana. Hawa kina Lissu, kuwajadili ni kupoteza rasilimali muda tu maana najua hakika hawawezi shinda.
Utakuwa unajitambua wewe. Mkapa alijaribu ila mwishoni aliharibu.
 
Mzee kupenda kubaya Chongo anaitwa Makengeza Manunuzi makubwa bila bunge ni sawa? Museveni juzi bila baraka za bunge sawa?
Hivi unadhani kila uamuzi lazima utoke bungeni? Na wabunge wenyewe ni wenye akili mbovu kama Tundu Lissu?
 
Jiwe hatukutaki. Jiwe out, jiwe aibu na fedheha vikufikie popote ulipo

Wanasema mjini - "jiwe, kimenuka!"

Vizuri ukatokea mwenyewe kusafisha hali hii chafu ya hewa na mapema iwezekanavyo.

Midahalo ni fursa tusiikimbie mkuu.

Mbona una mengi ya kujivunia na kujifunza pia?
 
Nasema Hivi Nileteeni Mwijage
Huyu Ni Rafiki Yangu Hata Kama Nilimtumbua. Mbona Simbachawene Na Mwigulu Niliwatumbua Baadaye Nikawapa Uwaziri Tena!!

Nasema Mkijichanganya Tu Mtajuta
Msema Ukweli Ni Mpenzi Wa Mungu
Uongozi Haujaribiwi

Mkinipa Mimi Niyatengeneza Barabara
Mgombea Urais Wa Ccm
 
Hahaha ha haaa!

Haya sasa si ndiyo vituko vyenyewe hivi?

Propesa mpara magamba, bashiri, mpole mpole na wengine. Hatuna la kumjenga mgombea wetu huyu?
 
Hahaha ha haaa!

Haya sasa si ndiyo vituko vyenyewe sasa?

Propesa mpara magamba, bashiri, mpole mpole na wengine. Hatuna la kumjenga mgombea wetu huyu?
Aibu Gani Hii
Yaani Haa 😁😂
Tutavaa Magunia Kuomboleza
 
Back
Top Bottom