UZUSHI Bashiru asema Ndugai aliwekwa kizuizini na kulazimishwa kujiuzulu

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Naona mambo ni moto kweli kweli, inasemekana Ndugai aliwekwa kizuizini na barua yake ya kujiuzulu Uspika hakuiandika yeye ni kwa mujibu wa hii tweet.

Sisi yetu mambo, maana malipo ni hapa hapa. Hakika muosha huoshwa.

1669462736845.png

Tunachokijua
JamiiForums imefatilia taarifa hii na kubaini kuwa mnamo Desemba 4, 2018 Dkt. Bashiru alihojiwa kuhusu uzushi uliovuma katika mtandao wa Twitter dhidi yake ambapo alikana kutumia mtandao wowote wa kijamii.

Dkt. Bashiru alisema:

“Watu wanaonijua wanafahamu jinsi ninavyotumia simu, sipo huko na sina Instagram, Twitter, WhatsApp, Facebook wala mfumo wa barua pepe kwenye simu yangu, ni wazushi hao puuzeni hizo habari”

Kwa mantiki hiyo, Uvumi huo ulioenea kwenye mtandao wa Twitter ni uzushi kwa sababu akaunti inayoeneza ujumbe huo imesajiliwa mwaka 2014.

Bashiru Ally Kakurwa alizaliwa Wilaya ya Bukoba Vijijini Januari 1, 1968, alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Mei 31, 2018.

Kabla ya kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Bashiru alikuwa mhadhiri katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Februari 26, 2021 aliteuliwa na Rais wa awamu ya 5, Hayati John Magufuli kuwa katibu mkuu kiongozi kisha baadae Machi 31, 2021 aliteuliwa na Rais wa awamu ya 6, Samia Suluhu Hassan kuwa Mbunge kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naona mambo ni moto kweli kweli, inasemekana Ndugai aliwekwa kizuizini na barua yake ya kujiuzulu Uspika hakuiandika yeye ni kwa mujibu wa hii tweet.

Sisi yetu mambo, maana malipo ni hapa hapa. Hakika muosha huoshwa.

View attachment 2427980
Huyu anatafuta umarufu lakini njia anayotumia hatamsadia zaidi ya kujishusha thamani na kupotea katika uwanja wa siasa
 
Naona mambo ni moto kweli kweli, inasemekana Ndugai aliwekwa kizuizini na barua yake ya kujiuzulu Uspika hakuiandika yeye ni kwa mujibu wa hii tweet.

Sisi yetu mambo, maana malipo ni hapa hapa. Hakika muosha huoshwa.

View attachment 2427980

View attachment 2431352
Halafu mazuzu humu ndio wengi nimeamini!

Umeishaambiwa kwa maandishi kwamba ni FAKE

Lakini bado umekomaa kuwalisha watu matango pori yako!

Au wewe umeona imeandikwa "FEGI"badala ya"FAKE"?¿
 
Halafu mazuzu humu ndio wengi nimeamini!

Umeishaambiwa kwa maandishi kwamba ni FAKE

Lakini bado umekomaa kuwalisha watu matango pori yako!

Au wewe umeona imeandikwa "FEGI"badala ya"FAKE"?¿
Hamna cha ufake hapo. Alivyokuwa na kibri unafikiri angejiuzulu kifala hivyo!
 
Bashiru hana account twitter ila ujumbe ni kweli... though proving needs kichwa cha uwenda wazimu, na naishia Hapa nadhani Pascal Mayalla unaelewa kwanini nimesema tuishie hapa
Mkuu britanicca , nimeelewa sana tuu!, I wish wana if wote wangekuwa na uelewa wa hivi, kwa vile watu hatufanani uelewa ningeomba wana if wenye uelewa wa ziada wa jambo lolote muwe mnawaelewesha na wengine wasio na uelewa huo ili sote tuelewe, mfano mzuri ni ule uelewa wako kumhusu Katto, ile siku nabandika bandiko hili Elections 2015 ile 2014 kumhusu Katto, you should have said everything you know kumhusu mtu huyu', you never know, yale majinga kule mahali, may be would have done something to prevent him!.

JF ukijua kitu, kama sio cha hatari kukuhatarishia maisha yako, kama Ben Saanane, just share!.
P
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom