Bashiru Ally: Mabalozi wa mashina wasipange foleni katika ofisi za Serikali

mwakajingatky

JF-Expert Member
May 30, 2018
555
909
Ofisi ya mganga mkuu imepokea barua yenye kumb. MCC/M.80/2/10 kutoka ofisi ya mkurugenzi wa jiji yenye agizo kutoka kwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa mh.dr Bashiru Ally Kakurwa kuhakikisha mabalozi wa mashina hawapangi foleni katika ofisi za serikali

Kwa barua hii mnaagizwa kuzingatia agizo hili kuwapa kipaumbele kwa kuwahudumia mabalozi wa nyumba kumi ili waendee kuwahudumia wananchi muda wote na kwa ufasaha zaidi

Nawatakia utekelezaji mwema

KAIMU MGANGA MKUU WA JIJI,
Sophia Kiluvia
IMG-20190823-WA0020.jpg
 
Vip kuhusu mama wajawazito na wazee???Wonders shall never end😭
 
hii ni kinyume na taratibu, katibu mkuu wa chama asiye na wadhfa wowote serikalini hana mamlaka yoyote katika utumishi wa umma, haya mawazo yake alipaswa kumpa mwenyekiti wake ambaye ni kiongozi wa serikali pia, kisha yeye angeyashusha kwa waziri husika na mtiririko ungeendelea hivyo.
Tumetenganisha chama na serikali na msomi kama bashiru nilitegemea alijue hilo lakini CCM ni ileile, viazi watupu.
 
Ni sahihi mjumbe wa nyumba kumi ni.kiongozi mkubwa wa serikali.Zimamoto,polisi simu wanazoziamini ni za wajumbe wa nyumba kumi kukiwa na tukio la ujambazi ,Moto nk..Sababu zinatambulika na zimesajiliwa ofisi za serikali za mitaa na polisi .Ni watu muhimu.Tukio lolote likitokea baya mtaani wa kwanza kuhojiwa Ni mjumbe wa nyumba kumi
 
Kwenye Chams chetu, hatikosi hela hata siku mmoja. Tukisema tuu , tuna shida, basi utawaona akina Subash, Manji, Mo, Bakhresa na Matajiri wote wenye Asili ya ki Asia, Uarabu, Wasomali wakifunga foleni Lumumba kujitolea.
NDUGU SS, umegafilika ulidhani tunazungumzia CHADEMA, apana ndungu, tunazungumzia ile machine kubwa.
Mishahara vipi hawatalipwa hadi lini!?
 
Swali, Jee kama uongozi wa mtaa uko chini ya Chadema ama Upinzani nao watapewa huduma sawa na viongozi wa CCM???????
Serikali ya mtaa huwategemea wajumbe wa nyumba kumi hata wawe chadema .Serikali ya mtaa kazi mwisho mchana usiku likikukuta la kukukuta mjumbe ndie wa kukusaidia.Wewe hujawahi vamiwa na majambazi au nyumba kuungua Moto ndipo waweza jua umuhimu wa mjumbe wa nyumba kumi.Utapiga Simu weee polisi na zimamoto hawaji ukienda kwa mjumbe akipiga tu simu Hawa hapa sababu wanazo .
 
Hivi mabalozi nyumba kumi ni viongozi wa serikali ama ni mfumo wa ccm pekee!? Kama ndivyo basi huu ujinga utapita tu.
 
hii ni kinyume na taratibu, katibu mkuu wa chama asiye na wadhfa wowote serikalini hana mamlaka yoyote katika utumishi wa umma, haya mawazo yake alipaswa kumpa mwenyekiti wake ambaye ni kiongozi wa serikali pia, kisha yeye angeyashusha kwa waziri husika na mtiririko ungeendelea hivyo.
Tumetenganisha chama na serikali na msomi kama bashiru nilitegemea alijue hilo lakini CCM ni ileile, viazi watupu.

Lakini hata kama kiongozi wa serikali angetoa kauli hiyo bado si sawa kwasababu mabalozi wa nyumba kumi sio watumishi wa serikali bali ni watumishi wa chama.
 
Ni sahihi mjumbe wa nyumba kumi ni.kiongozi mkubwa wa serikali.Zimamoto,polisi simu wanazoziamini ni za wajumbe wa nyumba kumi kukiwa na tukio la ujambazi ,Moto nk..Sababu zinatambulika na zimesajiliwa ofisi za serikali za mitaa na polisi .Ni watu muhimu.Tukio lolote likitokea baya mtaani wa kwanza kuhojiwa Ni mjumbe wa nyumba kumi

Hata pale kwenye ajali ya tanker Morogoro tuliwaona zaidi ya kumi walikuwepo katika kuwajibika na bila ya wao maafa yangekuwa makubwa zaidi. Na wao ndio walioisaidia tume katika kuujuwa ukweli wa kilichotokea exactly!
 
Ofisi ya mganga mkuu imepokea barua yenye kumb. MCC/M.80/2/10 kutoka ofisi ya mkurugenzi wa jiji yenye agizo kutoka kwa katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa mh.dr Bashiru Ally Kakurwa kuhakikisha mabalozi wa mashina hawapangi foleni katika ofisi za serikali

Kwa barua hii mnaagizwa kuzingatia agizo hili kuwapa kipaumbele kwa kuwahudumia mabalozi wa nyumba kumi ili waendee kuwahudumia wananchi muda wote na kwa ufasaha zaidi

Nawatakia utekelezaji mwema

KAIMU MGANGA MKUU WA JIJI,
Sophia Kiluvia
View attachment 1188527
Sasa hapo kuna shida gani,hao ni watu muhimu sana,hawatakiwi kupanga foleni.
 
Back
Top Bottom